Usonji ni moja ya matitizo ya afya ambayo mtoto huweza kuzaliwa nayo .hii ni hali ya kudumu tangu kuzaliwa hadi mwisho wa mtu husika. Matatizo hayo hugundulika katika umri wa miaka miwili katika ukuaji wa mtoto tatizo hili huambatana na mabadiliko ya tabia za mtoto kama vile utendaji wa mtoto , uongeaji wake , namna anavyochangamana na watoto wenzie watoto wengi hujitenga na kushindwa kuchangamana na wengine kutokana na matatizo katika mfumo wao wa mawasiiano hivyo huleta ugumu katika kuelewana na watoto wenzao. Watu wenye usonji huwa na tabia hizo hizo hata pale wanapokuwa wakubwa. Usonji huadhimishwa kila tarehe 2 Aprili.
SABABU AU VICHOCHEO VINAVYOSABABISHA MTOTO KUZALIWA NA USONJI
1. Matumizi ya pombe kwa mama mjamzito
2. Maambukizi ya rubella
3. Matumizi ya madawa ya kulevya kwa mama mjamzito
4. Sababu za kimazingira
5. Kurithi kwa tatizo kutoka vizazi vya nyuma
6. Changamoto wakati wa kujifungua
CHANGAMOTO ZA USONJI ( CHANGAMOTO KATIKA KULEA WATOTO WENYE USONJI)
1. Watu wenye usonji hupata changamoto katika elimu kutokana na matatizo waliyo nayo hasa katika mfumo wa mawasiliano, uchanganuzi wao katika mawasiliano hukosa ushirikiano hivyo huwaletea ugumu kupata elimu apatayo mtoto asiyekuwa na matatizo kama yao.
2. Wazazi wasio na utambuzi juu ya tatizo hili hufungia watoto wao wakiamini ni mikosi au aibu. Wengine hutelekeza watoto wao ili kueukana na matatizo ya kulea watoto hao.
3. Upungufu wa wataalamu wa kuwaelimisha wazazi wa watoto wenye usonji, pia upungufu wa vituo vya kulelea watoto wenye usonji, tofauti na shule za awali ambazo watoto wadogo hupelekwa , watoto wenye usonji hukosa vituo maalum vya kuwalea watoto hawa. Vilivyopo no vichache na vingine huendeshwa kwa gharama kutokana na changamoto zilizopo katika uleaji wa watoto wenye tatizo hilo.
4. Muitiko wa jamii katika kuunga mkono watoto wenye usonji ni mdogo na hivyo kuelekea upungufu wa sehemu husika za kusaidia watoto wenye usonji . ijapokua vyuo mbalimbali hutoa elimu ya mahitaji maalumu lakini vingi vimelenga vipofu, viziwi na mabubu kuliko usonji , hivyo kupelekea wataalamu kubobea katika kusaidia vipofu, viziwi na mabubu kuliko wahusika wa usonji.
NINI KIFANYIKE?
Kutokana na tatizo hili kuwa la kudumu ,hakuna tiba kamili ya kuondoa tatizo hili lakini zipo njia zinazoweza kusaidia watoto wenye usonji kukabiliana na hali aliyokuwa nayo , kwanini watoto na sio watu wazima wenye usonji? Ni rahisi kusaidia watoto weye usonji ni rahisi kuliko waliokwisha kua wakubwa . hii ni kutokana na uraisi wa mtoto kukua katika njia anazoelekezwa kuliko kumbadilisha aliyekwisha kuwa mkubwa.
Zifuatazo ni njia ambazo zinaweza kusaidia watoto kukabiliana na tatizo la usonji
1. Kuelimishwa kwa wazazi juu ya tatizo la usonji . sio kosa wala kitu cha aibu kuwa na mtoto aliyezaliwa na usonji. Hivyo waelimishwe namna ya kulea watoto wenye usonji na mahitaji wanayotakiwa kupata ili kukabiliana na hali hizo. Elimu kwa wazazi itawasaidia kupata ujasiri wa kuwalea watoto wao bila kuwaficha wakiogopa maneno au mawazo ya watu wengine .
2. Elimu maalum itolewe vyuoni juu ya kulea watoto wenye usonji kama moja itolewayo elimu kwa watu wenye mahitaji maalumu. Itasaidia kuongeza wataalamu waliobobea katika kulea watu wenye usonji. Wataalamu hawa ambao watachukuliwa kama walimu kwaajili ya kuwafundisha watoto hao namna ya kukabiliana na tatizo hilo. Watoto hao wakipewa elimu maalum kama vile namna ya kujihudumia wao wenyewe
(kujiandalia chakula, kuoga,kuvaa n.k)
3. Serikali ijenge vituo vya kulelea watoto hao wenye usonji bila kusahau kuajiri wataalam wa kulea watoto hao. Kutenga sehemu maalumu kwaajili ya watoto hao kutawasaidia kukua na watu wenye matatizo kama yao hivyo kuwapelekea kuzoea hali zao na kukabiliana nazo. Pia itaepusha kuchekwa na watoto wengine wasio na hali kama zao.
4. Wazazi wapeleke watoto wao kliniki mara kwa mara ili waweze kutoa maendeleo ya mtoto panapo umuhimu. Taarifa za maendeleo ya mtoto zinaweza kusaidia waganga katika hospitali kugundua tatizo lolote ambalo mtoto anaweza kuwa nalo . Kwa mfano mtoto akiwa hawezi kufuata muongozo wa mkono wa daktari anapoupitisha mbele ya mtoto inakuwa ni kigezo mojawapo cha kuashiria kuwa mtoto huyo anaweza kuwa kipofu. Vivyo hivyo ka mtoto mwenye usonji , maendeleo ya ukuaji wake na mabadiliko ya tabia huweza kuwa njia muhimu ya kutambua ugonjwa huo. Mahudhurio hafifu ya wazazi hasa katika kupeleka watoto wao kliniki husababisha kupuuza kwa mabadiliko ambayo yanaweza kuwa kiashiria cha tatizo hilo.
5. Wananchi waelimishwe juu ya tatizo la usonji , ufahamu juu ya tatizo hilo utasaidia wazazi wengi kulea watoto wao kwa uwazi bila kuwaficha. Uwazi na ufahamu juu ya hali za watoto wao utasaidia Serikali kutoa msaada kwa urahisi. Pia utasaidia wananchi kutoa misaada kwa urahisi iwapo hali za wazazi hao ni duni.
6. Vituo vilivyopo vya kulelea watoto wenye usonji vipewe muitikio hasa vinavyolea watoto yatima wenye usonji na walio telekezwa . Muitiko huo unaweza oneshwa na Wananchi na Serikali kwa ujumla kwa kutoa msaada hasa kwa wa vitu mbalimbali vya kukidhi mahitaji yao bila kusahau kwa kuwaunga mkono watu wanaojitolea kulea watoto hao. Kuwapa moyo kutawasaidia watu hao kutokata tamaa kutokana na ugumu wa kazi hiyo.
Picha : by google

Upvote
7