Najma Omary
Member
- Jul 18, 2022
- 5
- 14
USTAHIMILIVU KWA WAKULIMA DHIDI YA MABADILIKO YA TABIA NCHI.
Utangulizi
Mabadiliko ya Tabia nchi ni jumla ya mabadiliko ya hali ya hewa ya eneo fulani. Kilimo ni jumla ya shughuli zinazohusisha uzalishaji wa mazao mbalimbali kwa ajili ya chakula ama biashara. Shughuli za kilimo zimekua na mchango mkubwa katika kukuza uchumi wa wananchi na taifa kwa ujumla kama chanzo cha mapato.
Mabadiliko ya tabia nchi inahusisha kubadilika au kupotea kwa majira na vipindi vya mvua, ongezeko la joto, mlipuko wa wadudu hatarishi kwenye mazao na hali ya ukame zimekua ni changamoto kubwa zinazowakabili wakulima.
Hivyo, hatua za haraka zimekua na umuhimu mkubwa katika harakati za kukabiliana na mabadiliko hayo, zifuatazo ni kati ya nyenzo thabiti zinazowezesha kujenga ustahimilivu kwa wakulima dhidi ya mabadiliko ya Tabia Nchi:
Elimu juu ya mabadiliko ya tabia nchi
Elimu juu ya uwepo wa mabadiliko ya tabia nchi ni nyenzo kuu kwa ajili ya kuimarisha ustahimilivu kwa wakulima. Endapo wakulima na jamii kwa ujumla watakua na uelewa juu ya sababu zinazopelekea mabadiliko ya tabia nchi, elimu hiyo itakua ngao bora itakayowezesha kukabiliana na mabadiliko hayo, pamoja na kukuza ustahimilivu kwa wakulima, kupelekea uhakika wa mavuno bora, hivyo kukuza uchumi binafsi na uchumi wa taifa kwa ujumla.
Uchaguzi sahihi wa mazao kwa kulima
Uchaguzi sahihi wa aina ya mazao yakulima ni moja ya hatua muhimu ya awali inayoweza kufuatwa na wakulima ili kupelekea mavuno yaliyo bora. Wakulima hawana budi kuchagua ama kubadilisha aina ya mazao wanayolima kutokana na mabadiliko ya tabia nchi. Uchaguzi sahihi wa mazao kulingana na kiwango cha mvua na joto huchochea mavuno yaliyo bora zaidi na hukuza ustahimilivu kwa wakulima dhidi ya mabadiliko ya tabia nchi. Kwa mfano, kuhamia kwenye kilimo cha alizeti badala ya mtama, kutokana na takwimu za hali ya hewa katika kipindi husika. Takwimu hizi zinahusisha taarifa za wingi wa mvua, kiwango cha joto na kiwango cha upepo katika eneo husika.
Uchaguzi wa mbegu chotara
Idadi kubwa ya mazao hukumbwa na changamoto mbalimbali zinazotokana na mabadiliko ya tabia nchi. Kupungua kwa kiwango cha mvua, mvua kutonyesha katika kipindi kilichotarajiwa pamoja na ongezeko la wadudu hatarishi wakiwemo panzi na viwavi jeshi ni sababu zinazopelekea mavuno hafifu.
Wakulima wanapaswa kuchagua mbegu chotara zinazokua na kuzaa kwa muda mfupi,zinazostahimili ukame na magonjwa zilizo bora zenye uwezo wa kukabiliana na changamoto za mabadiliko ya tabia nchi.
Matumizi ya zana za kisasa za kilimo
Wakulima wanapaswa kutumia zana za kisasa zinazotumia teknolojia iliyo bora ili kukuza uzalishaji, kipato na mavuno. Kilimo kinaweza kuimarika kutokana na chaguo la kutumia pembejeo za kisasa na za gharama nafuu kama mashine za kulimia, kupalilia, kuvunia Pamoja na kusafirishia mazao, kwa mfano matumizi ya pawatila yanaweza kusaidia upatikanaji wa mazao kwa wingi. Hivyo kupelekea kilimo kuwa na tija kiuchumi kwa mkulima na taifa kwa ujumla.
Kilimo cha umwagiliaji
Kutokana na mabadiliko ya majira ya mvua, kupungua kwa kiwango cha mvua ama kukosekana kabisa kwa mvua, kilimo cha umwagiliaji kimekua ni suluhisho ya changamoto zote hizi. Kilimo cha umwagiliaji huwezesha uhakika wa maji kwa mazao kipindi chote cha kilimo, hivyo husababisha uhakika wa mavuno. Hii huimarisha kilimo dhidi ya uwepo wa mabadiliko ya tabia nchi na kumsaidia mkulima kuzalisha mazao katika kipindi chote cha mwaka pasi na kujali kiwango au upatikanaji wa mvua.
Matumizi ya mbolea na dawa za wadudu
Milipuko ya wadudu kama panzi na viwavi jeshi imekua ni changamoto inayotokana na mabadiliko ya tabia nchi. Wakulima wanapaswa kutumia dawa mbalimbali za wadudu ili kukabiliana na changamoto hiyo. Matumizi ya mbolea yamekua na umuhimu katika kilimo kwa kuwa mbolea hustawisha mazao na kupelekea mavuno yenye ubora, yanayowezesha kilimo kuwa na tija.
Matumizi ya takwimu na taarifa za kisayansi
Mamlaka ya hali ya hewa imekua ikitoa taarifa za kitaalamu zinazohusu hali ya hewa na tabia nchi. Taarifa hizo zimekua zikiambatana na takwimu zinazotoa tahadhari kwa wakulima dhidi ya madhara yanayoweza kusababishwa na mabadiliko ya tabia nchi. Endapo wakulima watatumia taarifa hizi ipasavyo, basi kilimo kitaimarika na mavuno yaliyo bora yatapatikana na kumnufaisha mkulima kiuchumi.
Matumizi ya vishiria asilia vya mvua
Miti ya matunda kama maembe yamekua yakitoa maua kuashiria kumea kwa matunda. Endapo miti hiyo ikitoa maua miezi ya mapema kuliko kawaida imekua ishara ya kuwa mvua zitawahi kunyesha kuliko kawaida. Kwa ishara kama hii, wakulima wanaweza kuandaa mashamba mapema kwa ajili ya kupanda mbegu, ili kujilinda na athari za ukame ama mabadiliko ya majira ya mvua.
Kuambatanisha kilimo na shughuli nyingine za kiuchumi
Ustahimilivu dhidi ya mabadiliko ya tabia nchi huweza kuimarika endapo wakulima watajumuisha shughuli mbalimbali pamoja na kilimo ili kukuza uchumi na kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi. Ufugaji wa nyuki imekua ni moja kati ya shughuli bora kwa wakulima kwani mbali na asali itokanayo na ufugaji wa nyuki, nyuki wamekua wakitoa ulinzi asilia kwa mazao dhidi ya Wanyama pori.
Matumizi ya nishati mbadala
Kati ya harakati thabiti ya kutunza ustawi wa mazingira, matunzo ya misitu yamekua na umuhimu mkubwa, hivyo basi wananchi wanapaswa kutumia nishati mbadala ikiwemo matumizi ya majiko banifu, ili kupunguza kiwango cha mkaa ama kuni kinachotumika kwa matumizi ya kila siku. Hii husaidia ustawi wa miti na uoto wa asili, unaowezesha kutunza mazingira na vyanzo vya maji venye umuhimu mkubwa katika kilimo.
Hitimisho
Licha ya mapambano dhidi ya mabadiliko ya tabia nchi, harakati za kumuinua mkulima kiuchumi zimekua zikikumbwa na changamoto mbalimbali kama, kukosekana kwa masoko ya uhakika na mitaji midogo. Ustawi wa kilimo huambatana na uhakika wa masoko na upatikanaji wa mikopo yenye riba nafuu kwa wakulima.
Aidha ya yote, jitihada za serikali zimekua na mchango mkubwa katika kujenga ustahimilivu kwa wakulima zikiwemo, tafiti za kisayansi zinazofanywa na taasisi mbalimbali kama; Tanzania Pesticide Research Institute (TPRI), Tanzania Agricultural Research Institute, Desert Locust Control Organisation na Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) zimekua zikitoa mchango chanya katika kilimo hapa nchini.

Attachments
Upvote
24