Zanzibar-ASP
JF-Expert Member
- Nov 28, 2013
- 12,151
- 44,120
Juhudi zozote za Simba kutaka kuipiku Yanga huenda zikawa ni mbio za sakafuni kwa sababu tu ya uswahiba uliopo baina Yanga na CCM.
Kuna namna mbele ya macho ya watawala wa kiCCM inaonekana ni fedheha kubwa pale ambapo Yanga inapozidiwa kimpira na Simba.
Kiburi chote cha Yanga kususia derby ya 15/6/2025 kilikuwa kimejificha kwenye kichaka cha kijani (CCM), viongozi wa Yanga kwa kujiamini kabisa walitoa tamko wakisema hakuna cha kanuni, bodi ya ligi au TFF wenye uwezo wa kuinyang'anya Yanga hata nusu point kwa kususia derby, na yoyote atakayejaribu hilo atakutana na kitu kizito. Na kweli baada ya muda mchache kupita TFF na bodi ya ligi wote wakasalimu amri, wakatema bungo!
Kwa jeuri, wanayanga kwa sasa wanatamba mtaani na mitandaoni wakisema wao hawaongee na mbwa bali wanaongea na mwenye mbwa.
Wanasimba huenda tukaendelea kupigika mpaka CCM siku moja itoke madarakani.