Mzozo wa Urusi na Ukraine: Sheria tata ya Putin ya kutorudisha zaidi ya ndege 500 za kibiashara kwa nchi za Magharibi
17 Machi 2022
Urusi inalipiza dhidi ya vikwazo vilivyowekwa na nchi za Magharibi.
Rais Vladimir Putin alitia saini sheria Jumanne kuzuia makampuni ya kigeni yaliyokodisha ndege zao kutoka Urusi kuzichukua tena.
Uamuzi huo umekuja baada ya makampuni kadhaa kuitaka Moscow kurudisha ndege walizokodi, ikiwa ni sehemu ya vikwazo vilivyowekwa na nchi za Magharibi baada ya uvamizi wa Urusi nchini Ukraine.
Na ni kwamba karibu 75% ya ndege zinazotumiwa na mashirika ya ndege ya Kirusi hukodishwa, kulingana na data rasmi, kwa jumla ya ndege 515 zenye thamani ya zaidi ya dola za Marekani milioni 10,000. [emoji1787][emoji1787][emoji1787]