Tetesi: Utabiri 1977: Waalimu wa UPE wanaenda kutengeneza Taifa la wajinga na sasa miaka 50 imepita. Je sisi tuna akili au sisi ni wajinga?

Ukitaka kuharibu future ya taifa lolote duniani huna haja ya kutumia bunduki au mabomu ya maangamizi Cha kufanya chezea mfumo wa elimu na mwisho utakuja kuona matokeo yake miongo kadhaa ni ajabu unakutana na kijana kahitimu kidato Cha Nne na kupata Cheti alafu hajui kuandika Insha sasa unajiuliza alifaulu vipi?
Una hoja, lakini wakati mwingine jitahidi kutumia alama za uandishi kama vile nukta (.), mkato (,), nukta pacha 🙂) n.k ili comment yako isomeke vizuri.

Vinginevyo na wewe utaonekana ni sehemu ya zao la huko kuchezewa kwa mfumo wa elimu.

Siyo kwa ubaya lakini mkuu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tatizo halikuwa failures wa darasa la saba tu. Ualimu ni profession kama profession nyingine yoyote ile. Hao walimu wa UPE hawakupata training hata sekunde moja. Mbaya zaidi wengi wao wakapewa kufundisha wanafunzi wa darasa la kwanza which was worse. Kibaya zaidi idadi
ya wanafunzi kwenye darasa haikuzingatiwa. Standard class size ya shule za msingi ni wanafunzi 45. Hii ilizidi kwa hata mara mbili sababu hakukuwa na vyumba vya kutosha vya madarasa. Kwa kifupi hakukuwa ba maandalizi ya kutosha kabla ya kuandikisha wanafunzi wengi wa darasa la kwanza. Ndiyo maana watu waliipa UPE maana yake halisi- Ualimu Pasipo Elimu. Hii yote ilisababishwa na ukweli kwamba wakati ule , lakini nafikiri mpaka sasa, ilkuwa ni one man show. Rais ndiyo anajua kila kitu. Hawezi kukosea. Lakini kinachosikitisha sana mpaka leo watu wanaamini hivyo. Ndiyo maana raus akikisolewa wapambe wake wanadai anatukanwa. Posts nyingi humu zinaonyesha hivyo.
Walimu wa UPE waliosoma miaka minne
 
Je sisi ni wajinga au tuna akili?
mjinga /mʄiŋga/ :

1.Mtu asiyejua kitu au jambo fulani.

2.Tamko la dharau au tusi kwa anayechukuliwa kutojua kitu.

akili /akili/:

1.
Uwezo wa kuelewa na kujifunza mambo.

2.Uwezo wa kufikiri na kuamua kwa busara.

Source: https://en.bab.la › dictionary › swahili-english

Tukianza na wewe mtoa mada , mada yako na uwezo wako wa kuwasilisha, unahisi ni mjinga au una akili?????
 
Kwani elimu ya msingi lengo lake ni nini wakuu?

Kwa ninavyofahamu mimi elimu ya msingi ni K-3.
-Kusoma
  • Kuandika
  • Kuhesabu

Maarifa mengineyo utayapata hata JF. Tatizo ni watu hawajui pa kuyapata hayo maarifa.

Mfano bora ni Prof. Lwaitama.
 
Samahani mleta mada, naomba unipe uhusiano wa wewe kufaulu na uhusiano wa kumfaulisha mwingine kwa kiwango kilekile. Namaanisha hivi:

Wewe umepata daraja la kwanza, kwa maana hiyo ukiwa mwalimu utakuja kuwafaulisha wanafunzi wako kwa kiwango kama chako!!!!!!!!!!

Namaanisha hivi tena:

Walimu wanaoajiriwa wawe wamepata ufaulu mzuri wa daraja la kwanza (mtazamo wenu) hivyo wanafunzi wao wote (shule za kata) watafaulu kama wao.

UDSM, SUA, MZUMBE na UDOM kwa Tanzania hivi ni vyuo vikubwa, kuna shahada mbalimbali za elimu zinatolewa huko. Katika vigezo vyao vya udahili unadhani walimu kutoka hivi vyuo wanaufaulu mdogo??? (mtazamo wenu)

Jibu kwa kutumia picha pana na siyo mhemko, papara na hasira!!!!!!!!!!!!!!

Nb: Walimu ni sehemu ndogo sana ya tatizo, nashangaa wanavyotupiwa mzigo wa lawama pamoja na kujitahidi kwao katika mazingira magumu ya kazi!!!!!!!!!!!

Eti wamefeli!!!!!!!!!!!Halafu ukipata watoto unampelekea akufundishie!!!!!!!!!!!!!!!!!Iwe shule binafsi au ya umma bado utawakuta!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

Ahsanteni sana walimu kwa mchango wenu!!!!!!!!!!!!
Kunakitu umekionesha mkuu ila Hawa walimu wa sasa hivi nao ni zao la walimu wa upe.
Hivi ule wimbo wa Nay hasa kwenye mistari inayohusu elimu na wa somi kutokujihusisha na bahadhi ya mambo si inaeleweka vizuri ile.

Ila pia najiuliza, sijui ni kwasababu hatuna nguvu kubwa ya pesa
 
Umetoa mada nzuri sana mkuu, tatizo itakua diluted na vihiyo ambao ndio wengi humu, yes UPE ulikua mpango maalum ili wajinga na wapumbavu wawe wengi, royal families watoto wao hakusoma chini ya sera hii ya UPE, miaka michache iliyopita kukaletwa shule za sekondari za kata, hizi nazo zimetuletea wapumbavu zaidi, aliyeanzisha hili hata kitukuu chake hakijasoma huko, President Mugabe pamoja na ushenzi wake ulioua uchumi wa Zimbabwe, education systems aliyoirithi hakuigusa ndio maana hadi leo wazimbabwe ni hot cake kielimu, President Kagame kafuata waalimu Zimbabwe katuluka sisi, UK hadi leo wazimbabwe (nurse's)wanapewa working visa kirahisi, hapa tuna Doctors wapo mitaani!wanakimbiza viajira uchwara
Umeandika togwa tu,walimu wa upe hawakuzalisha wanafunzi wasiojua hata lugha yao kwa kuandika na kuitamka,waliujua mtaala vizuri na walitoa zao murua,labda unadhani kiingereza ndiyo elimu,mtazamo ambao huakisi ujinga na uvivu wa kufikiri,hakuna div 1-3 toka shule za kata!?..hakuna division 3-0 shule za vipaji maalum na za binafsi zenye 'walimu wazuri'!?
 
Je hili ndio Taifa la wajinga lililotabiriwa mwaka 1977 wakati walipoanzisha sera ya Elimu ya Universal Primary Education UPE?

Katika sera ya nchi ya kutoa elimu kwa wote. Serikali ilipanga kutoa elimu kwa watanzania wote bila ubaguzi wowote. Serikali ilikuja na mpango elimu ya msingi iwe ni lazima kwa kila mtanzania.

Katika Bunge la wakati ule viligubikwa na wasomi wachache sana.
Wapinzani wa sera kipindi kile walionekana mwiba sana kwa Serikali.
Wasomi wengi walishauri kuajiri waalimu kutoka nchi ya Kenya na nchi kama uingereza na mataifa mengine Walikuwa tayari kutoa waalimu. Ili kufanikisha mpango huu.

Hatimaye Bunge likaja na mpango wa UPE (Universal Primary Education) yaani wahitimu failure wa elimu ya msingi kwenda kuwafundisha wenzao.
Wasomi chuo kikuu cha Dar es salaam waligomea huu mpango kabisa. Sababu ilikuwa Tanzania inatengeneza Taifa la watu wajinga sana.

Sasa hivi wale walioanza kufundishwa na walimu wa UPE wanamiaka 50 mpaka 55. Je Taifa letu ni la watu wenye akili ama wajinga kama ilivyotabiriwa?
Ni kweli 50 plus ni hao wezi
 
je sisi ni wajinga au ni sisi ni watu wenye akili?
 
Wajinga ni wengi kuliko walioelimika.
 
Taifa la wajinga limejaa Simba na yanga diamond na zuchu tu
 
Ukitaka kuharibu future ya taifa lolote duniani huna haja ya kutumia bunduki au mabomu ya maangamizi Cha kufanya chezea mfumo wa elimu na mwisho utakuja kuona matokeo yake miongo kadhaa ni ajabu unakutana na kijana kahitimu kidato Cha Nne na kupata Cheti alafu hajui kuandika Insha sasa unajiuliza alifaulu vipi?
Multiple choice

Multiple choice, bahati nasibu.
 
Hawa walimu wa sasa hivi nao ni zao la walimu wa upe.
Ndugu, wewe mwenyewe ni wa zao lipi???? Au mazao yanaangalia walimu????????Wahandisi, madaktari,waandishi wa habari, wanasheria, wahasibu, manesi, mafundi, wanasiasa n.k wao hawamo???????
 
Je sisi ni wajinga ama tuna akili mbona hamjibu swali langu
 
Je hili ndio Taifa la wajinga lililotabiriwa mwaka 1977 wakati walipoanzisha sera ya Elimu ya Universal Primary Education UPE?

Katika sera ya nchi ya kutoa elimu kwa wote. Serikali ilipanga kutoa elimu kwa watanzania wote bila ubaguzi wowote. Serikali ilikuja na mpango elimu ya msingi iwe ni lazima kwa kila mtanzania.

Katika Bunge la wakati ule viligubikwa na wasomi wachache sana.
Wapinzani wa sera kipindi kile walionekana mwiba sana kwa Serikali.
Wasomi wengi walishauri kuajiri waalimu kutoka nchi ya Kenya na nchi kama uingereza na mataifa mengine Walikuwa tayari kutoa waalimu. Ili kufanikisha mpango huu.

Hatimaye Bunge likaja na mpango wa UPE (Universal Primary Education) yaani wahitimu failure wa elimu ya msingi kwenda kuwafundisha wenzao.
Wasomi chuo kikuu cha Dar es salaam waligomea huu mpango kabisa. Sababu ilikuwa Tanzania inatengeneza Taifa la watu wajinga sana.

Sasa hivi wale walioanza kufundishwa na walimu wa UPE wanamiaka 50 mpaka 55. Je Taifa letu ni la watu wenye akili ama wajinga kama ilivyotabiriwa?
Hatimaye Bunge likaja na mpango wa UPE (Universal Primary Education) yaani wahitimu failure wa elimu ya msingi kwenda kuwafundisha wenzao.

Sio kweli miaka ya nyuma best grade seven leavers walikwenda ualimu. Mambo yalikuja kuharibika baadae
 
Back
Top Bottom