UTABIRI: Argentina huenda ikatwaa Kombe la Dunia 2022 Qatar

Utabiri unaoweza kwenda kutimia,japo hapo kwenye namba 3 ndio umepuyanga,hivi Argentina ya Sasa unaweza kuita ni kizazi Cha dhahabu,yenye majina,vipaji na muunganiko wa timu kuliko zilizopita na kushindwa kuchukua kombe la dunia??
Hivi Argentina hii ya kina Molina,Tagliafico,De Paul,Alex Mcallisster ni kizazi Cha dhahabu? Utalinganisha na ile ya 98-2002 ya kina Carlos Roa, Nestor sensini, Roberto Ayala,Javier Zanetti,Diego Simeone,Juan veron,Mattias Almeyda, Marcello Gallardo,Abel Balbo, Gabriel Omar, Batistuta,Hernan crespo,Claudio Lopez na Ariel Ortega,?
Au ile ya 2006-2010 ya kina Walter Samuel,Nicolas Burdisso,Julio Cruz, Gabriel milito, Diego milito,Gabriel heinze,Esteban Cambiasso !!
Hauko serious wewe,sehemu zote umepatia Ila kwenye kizazi Cha dhahabu ndio umepuyanga! Ungesema kizazi Cha Messi sawa Ila sio Cha dhahabu
 
Utabiri unakaribia kutimia
 
Hongera!,kuonyesha umahiri katika utabiri usio na chenga,umetumia vigezo vyenye mashiko kuipata timu inayostahili kuwa bingwa wa dunia.
 
Hongera
 
Ndugu nilimaanisha ni kizazi cha dhahabu chenye majina, vibaji na muunganiko wa kitimu. Kama huamini hilo tazama vizuri utaligundua.

Yes, Messi ana kipaji na jina kubwa, ulishawahi kujiuliza na mara ngapi ameshiriki world cup huku timu yake ikikosa muunganiko wa kitimu?

Kupata kizazi chenye sifa zote tatu muhimu ni nadra sana. Kwa mwaka huu Argentina wamepata sifa zote tatu.


Argentina ya msimu huu imekuwa na Kipa bora, Mchezaji bora na Chipukizi bora wa world cup.
 
Yametimiaaa kabisaaaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…