UTABIRI: Kocha wa Simba Fadlu Davids hana maisha marefu ndani ya klabu, atafukuzwa ghafla kabla ya Pasaka

Acha ramli mkuu,mnyama anatafuna kimtindo huku akiwinda big prey!!.....lembelaga nkoi,dulekelage eSimba ise!
 
Babu mjanja sana kuna siku niona umevaa saa Og ya Audemars piguet royal oak nikaogopa🤔🤔🤔
Huenda uliona picha yangu ya Mwaka 47

Enzi hizo za kufukuzia mchumba, unakaa unamvizia akienda kuchota Maji kisimani ndiyo umwagie mistari hadi akuelewe 😜
 
Kama uliangalia mpira WA Jana basi elewa Fadlu bado yupo yupo Sana! Pamoja na kukamia Sana Pamba wamshukuru Sana Refa, kwani Ile faulo ya aliyofanyiwa Ateba ilitakiwa pamoja na penalty lakini pia na kadi nyekundu ilitakiwa itolewe. Kwa maana iyo wangekuwa 10 Pamba wangeoga mvua ya magori.
 
Mnajipa moyo mnashindwa kutambua Simba wamejitoa mhanga kufanya kile ambacho Yanga wamekiogopa. Kucheza mechi wakati una mechi kubwa ya kimataifa huwezi kujitoa kikamilifu kwa sababu ya kuogopa majeraha,Kipindi cha kwanza Simba walicheza kwa kushambulia vizuri, walipopata goli kipindi cha pili wakapumzisha wachezaji wao muhimu.Halafu unaizungumzia timu iliyoshinda na sio kufungwa au draw
 
Umechambua mbinu vizuri, huenda akafukuzwa ama asifukuzwe ila umechambua vizuri mno, watu wa mpira watakuelewa.
 
Mmehamisha goli?! Si mlisema hafiki Krismass..ameondoka Gamond kabla ya Krissmass na ungekuwa na Akili zinazochemka ungeandika Saed wa Utopolo hafiki Pasaka.
 
Huko yanga yasemekana engineer alimlazimisha mzize kubadili dini, KUNA UKWELI?
Kwa asili Mzize ni Muislamu. Hapa mtaani alipokuwa anapaki boda boda yake anajulikana kwa jina la thabiti

Sidhani kama Iringa kuna ukoo wa kina Mzize. Kwa ivo Hersi asitwishwe zigo lisilo lake.

Ila Yanga wanajua hilo jina la Clement Mzize wamelitoa wapi.
 
Mnajipa moyo mnashindwa kutambua Simba wamejitoa mhanga kufanya kile ambacho Yanga wamekiogopa. Kucheza mechi wakati una mechi kubwa ya kimataifa
Hiyo mechi ilikuwa na faida kubwa sana kwa Simba.

Kwanza, ilikuwa ni kurudisha spirit ya ushindani kwa wachezaji baada ya kalikizo kafupi.

Pili ni kuongeza pressure kwa utopolo. Pamoja na kwamba wana game moja mkononi, ushindi dhidi ya Pamba umeiongezea pressure zaidi utopolo. Wakifanya mchezo watazidi kudondosha point. Hii ni changamoto ambayo Simba ilikuwa inakumbana nayo misimu hii miwili ya nyuma, kujaribu kumfukuzia utopolo. Lengo sasa ni kutoshuka kutoka kileleni.
 
Lakini utabiri wa Gamondi ukakushinda au miwani haikuona?Au utabiri wako ni special kwa Simba tu.Isije ikawa wewe ni wale watabiri uchwara wakujaribu kuona kilichopo kilomita 100 wakati sebuleni kuna kinyesi hawasikii harufu wala kukiona.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…