Street brain
JF-Expert Member
- Oct 24, 2022
- 681
- 923
Mambo vipi wanajf jobless nakuja tena kutabiri,,,ukiangalia mwelekeo wa maendeleo ya taifa chini ya uongozi wa Rais Samia katika miaka mitano ijayo, ebu ngoja nigusie vitu vifuatavyo watu au wenye mfumo wanaenda kutengeneza vitu vifuatavyo kwenye mfumo wao👇👇👇
Huu ni utabiri tu na wala sijamsema mtu na hakuna anayejua kwamba yatatokea haya it's just UTABIRI,,, kwa wale wenye hoja ya kupinga, elewa kwanza utabiri na usije na hasira zako
Anyway jobless natafuta kazi angalau niepuke hii aibu,,, mfumo tutawaachia....
Huu uzi utunzeni,,,,,
- Watu watatengeneza mifumo yao binafsi. Biashara, taasisi, na majukwaa ya ushawishi yatatengenezwa na kutumiwa kujiimarisha
- Ajira nyingi zitatokana na mitandao ya watu.Si CV peke yake itakusaidia, bali uhusiano na nafasi unazojitengenezea sasa.
- Watabeba watu wao.Wanaojiandaa leo ndiyo watakaopewa nafasi, kazi, tenda na heshima kesho.
- Teknolojia itatenganisha waliokomaa na waliopuuzia. Waliojifunza skills za digitali, AI, coding, freelancing, nk ndio watatawala soko.
- Fedha zitaanza kuzunguka kwa wenye mitandao thabiti. Ukiwa nje ya mfumo, utazidi kuona dunia inakukimbia.
- Mikopo na fursa zitaenda kwa wenye taarifa sahihi.Na taarifa hizi ziko kwa wanaojihusisha sasa, si wa mwisho dakika za lala salama. Wengine watajenga ushawishi ndani ya serikali na taasisi binafsi Si kwa rushwa, bali kwa umahiri, uaminifu na kujituma.
- Taasisi za watu binafsi zitazidi kushika hatamu. NGO, Startups, forums, vyombo vya habari huru vitapanga mjadala wa taifa.
- Wanaoanza leo kuwa consistent wataonekana kesho. Sauti yao, brand yao na mchango wao vitaheshimiwa.
- Waliopuuza miaka hii mitano watajuta.Kwa sababu mfumo utakuwa tayari umejengwa, nafasi zitakuwa chache, na ushindani mkubwa.
Huu ni utabiri tu na wala sijamsema mtu na hakuna anayejua kwamba yatatokea haya it's just UTABIRI,,, kwa wale wenye hoja ya kupinga, elewa kwanza utabiri na usije na hasira zako
Anyway jobless natafuta kazi angalau niepuke hii aibu,,, mfumo tutawaachia....
Huu uzi utunzeni,,,,,