Kichwa Kichafu
JF-Expert Member
- Apr 13, 2017
- 44,855
- 189,385
Habari.
Hadi sasa zimebaki timu nne ambazo zitacheza hatua ya nusu fainali na ratiba:
Leg 1.
27 April 2021 Tuesday
Paris Saint Germain Vs Manchester City
Real Madrid Vs Chelsea
Leg 2.
04 May 2021 Tuesday
Manchester City Vs Paris Saint-Germain
Chelsea Vs Real Madrid
Hapo bila kupepesa macho mpira anaocheza Paris Saint Germain dhidi ya kocha wao Pochettino umekuwa na nidhamu ya kutafuta matokeo tu hakuna kingine.
Hivyo basiasi ubishe usibishe Paris Saint Germain atakuwa Champion wa ligi ya mabingwa ulaya.
Final itachezwa 29 May 2021 Ataturk Olympics Stadium.
Final itakuwa ni Paris Saint Germain Vs Real Madrid na bingwa atakuwa Paris Saint Germain.
Updates. 29/04/2021
Baada ya first leg matokeo yamekuwa yakishangaza kulingana na uzi wenyewe ila amini nawaambia wengi watashangazwa zaidi baada ya 2nd leg.
1st leg.
Real Madrid 1 - 1 Chelsea
✓Pulisic[emoji460]
✓Benzema[emoji460]
PSG 1 - 2 Manchester city
✓Marquinhos[emoji460]
✓De Bruyne [emoji460]
✓Mahrez [emoji460]
Hakika naendelea kuona PSG bado ana nafasi ya kusonga mbele vizuri kabisa kwa mpira niliyoona jana kwa zaidi ya dakika 50 alipiga mpira mwingi sana na hata Etihad nategemea wataweza kupindua meza vyema.
Real Madrid ana nafasi ngumu japo Chelsea waliweza kupambana na kucheza mpira mwingi ila pale darajani naona watalala na viatu pia naendelea kumpa nafasi Real Madrid kuendelea mbele.
Updates. 06/05/2021
Baada ya 2nd leg iliyochezwa tar 4th & 5th May 2021.
Hakika matokeo yamekuwa tofauti kabisa na maudhuhi ya huu uzi maana timu zote zikizopewa nafasi na huu uzi zimepokea kipigo cha mbwa mwizi yaani kipigo cha mtema-kuni.
Chelsea 2 - 1 Real Madrid
✓Timo Werner[emoji460]
✓Mason Mount[emoji460]
Manchester city 2 - 0 PSG
✓Mahrez[emoji460]
✓Mahrez [emoji460]
Hivyo kufanya vikongwe kutoka spain kulamba mwiko mkavu huku hawa wakulima kutoka ufaransa wakirudi na majembe pamoja na vifaa vyote vya shambani kwao wakiambulia patupu. Na kufanya marudio ya kuingia timu zote kutoka England.
Chelsea. Vs Manchester city
Tusubiri fainali hiyo ikiwa wengi wana prediction tofauti tofauti ila upande wangu hadi sasa sijui nani na sina prediction yeyote yangu ni macho kama ni usambuzi basi nimepiga F.
Nawasilisha Mzee Mkoloni.
Cc: Kichwa Kichafu