Zanzibar 2020 Utabiri: Samia Suluhu kuwa Rais wa Zanzibar, Dkt. Mwinyi kuwa Makamu wa Rais wa Tanzania

Inawezekana upo sahihi hasa kwa kufuata trend ya viongozi waliopita.Si Waswahili husema maji hufuata mkondo?!!!.
 
Mama Samia hatagombea uraisi Zanzibar, (i) Kwa sababu cheo alichonacho sasa ni kikubwa kuliko uraisi wa Zanzibar; & (ii) Watanzania wa Zanzibar kama ilivyo bara hatuko tayari kuongozwa na mwanamke katika madaraka ya uraisi.
Shein je hakuwahi kuwa Makamu WA Rais wa TZ?.
 
Asante P!
 
Kwa utabiri humu JF ni noma,Pascal Mayalla aliwahi kutabiri miaka hio rais ajae yawezekana akawa Magu kipindi hicho hata CCM bado mchakato wa kuchukua form za urais haujaanza na ikawa hivyo,kuna njemba inaitwa Magamba matatu huko 2012 iliwahi kutabiri style ya uongozi utakavyokua wa awamu ya 5 na imekua 99% kama mjomba alivyotabiri,kuna uzi humu watu walikua wanabishana balaa kwamba nani atakua ni mkuu wa majeshi baada ya Mwamunyange njemba 1 ikakomaa humu lazima awe Mabeyo tu na ikawa hivyo.

So JF ni kichaka kikubwa,unaweza kuta aliyeleta huu uzi ni kigogo huko Nec na walishafanya maamuzi yao wanatupima tu reaction wana Nzengo.
 
Haitawezekana
 
Suala la zile hotuba za siku za idd..
Je, mama samia atasimama kwenye mimbari ya wanaume?
Tafakari
 
Mkuu kwa Zanzibar bado sana hawako tayari kutawaliwa na mwanamke,lakini pia sioni kama mama samia yuko tayari kuchukua fomu,ila kwa rais huenda akawa mwinyi , vuai nahodha au Makame mbalawa,hawa watatu wana asilimia ,80% ya kuukwaa urais wa zanzibar

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ngoja tusubiri.
Time will tell!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Katika list yako namba 16 ndie atakaechaguliwa na CCM kugombea kiti Cha uraisi wa Zanzibar..

Wazanzibari Kama kawaida Yao hawatomchagua mtu kutoka CCM kuwa Raisi wao,sababu ziko nyingi za kutoichagua CCM

Kama uchaguzi utakuwa wa haki Kama Magufuli alivyosema Basi ACT-Wazalendo itaiongoza Zanzibar..

Mungu ibariki Zanzibar,Tanzania na Afrika yote

Time alone time will tell,let's wait and see
 
Kwa hiyo hiki chama kinachoimarika kuliko wakati wowote ule kwa kukimbiwa na wanachama wake bado hakina nafasi ya kushika dola 2020?
 
Mama Samia alishaweka wazi hana mpango na urais wa Zanzibar kwa sababu ni cheo kidogo ukilinganisha na cheo alichonacho.
Japo ni kweli ki protokali VP ni mkubwa kuliko rais wa Zanzibar, ila kimamlaka, VP ni just a ceremonial position as a standby, in case something happens to the president, lakini hana mamlaka yoyote, hana powers zozote za kufanya chochote na hata akikaumu urais hawezi kusaini chochote, zaidi ya kutembea na mikasi na kumwakilisha rais kwenye events, lakini rais wa Zanzibar ni rais kweli wa nchi ndani ya nchi, ana dola, ana nguvu na ana mamlaka, hivyo kiutendaji Rais wa Zanzibar ana madaraka na mamlaka kuliko VP.

P.
 
Samia Suluhu amekosana na Wana CCM Zanzibar. Nlisikia aliwaambia alieshinda apewe tu, CCM Zanzibar wakamcharukia. Na ile misemo ya yeye Namba 2 na sio 3 si bure.

Kuna ile CCM iliomtaka Gharib Bilal kipindi cha Shein, ivi ile imeegemea wapi?
 
Zanzibar itakuwa nchi ya kwanza duniani rais anachaguliwa kwa kigezo cha ukimya na upole.
sio itakuwa, ishakuwa tayari, huyu aliepo saivi unaweza kaa miezi usimsikie kabisa na ukafikiri Balozi Seif au RC Ayoub ndo anaongoza nchi
 
Hussein mwinyi ndo atakuwa mgombea, mengine Ni mbwembwe
Huyu jamaa ni kwasababu ya baba yake alwahi shika kiti hivyo ni nyota tu inang'aa kupitia baba yake? Anakitu gani cha kipekee mpaka apewe nchi?
 
Binafsi kwangu Balozi Amina Salum Ali ni presidential material. Tatizo gender.

[emoji2398]ᵃʳᵉᵉᵐ [emoji769]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…