Utabiri: Simba bingwa wa CAF 2023

Utabiri: Simba bingwa wa CAF 2023

Mpaka sasa sijaona mtu anayepinga kuwa Simba ina squad ya wapambanaji 15 wa kuleta ushindani wa kweli CAF. Uto mnajichekesha chekesha tu.
Hebu tuwekee majina ya hao wapambanaji 15 wa Simba watakaoleta ilo kombe la Afrika acha kubwabwaja sana
 
Mmepigwa jana na timu ya mwisho kwenye ligi ya kwao..!!
Tunajenga timu. Hatuna pressure za unbeaten kama nyie Uto. Lengo lingekuwa kupata ushindi kwa namna yoyote ile tungekuwa tunaongea tofauti sasa hivi.
 
Natoa utabiri huu nikiwa na akili zangu timamu na upeo wa kutosha kuhusu mpira wa miguu.

Mwaka huu 2023 ndiyo mwaka historia mpya inaenda kuandikwa kwa Simba kuchukua kombe la CAF Champions League.

Najua kuna wapenzi wa Simba bado wanalilia kuona usajili mpya ili kuboresha timu ila ngoja nikwambie kitu. Inashangaza watu wanalilia wachezaji waondolewe ambao hata siyo tegemeo kwa timu.

Championship team katika mashindano yoyote, vilabu, taifa inahitaji wachezaji 13 hadi 15 tu wa kutegemea, yaani first 11 na sub 2 hadi 4 zinazoweza kuongeza nguvu pale inapohitajika. Simba timu hiyo wanayo.

Ambacho mimi ningefanya ni kuangalia jinsi ya kuboresha upande wa beki wa kushoto, mipira mingi inapotea kutokea kule. Ikibidi nngemsogeza Zimbwe mbele kama winger anaweza kufanya vizuri zaidi position hiyo. Kwa kuongezea tu Outtara ni mchezaji mzuri ni suala la kuangalia tunamtumiaje.

Ila wachezaji 15 wa kusumbua CAF tunao.
Tawire baba! Tawire! 😩
Na pia kati John Boco, Habibu Kiyombo, au Kibu Dennis; mmoja wao ataibuka kuwa mfungaji bora!!

Tawireee!! 😩
 
Nilitegemea Simba Ili wafike Angalau Nusu failani ya CAF.
Lazima uachane na wachezaji wafuatao.

Nelson Okwa.
Victor Akpan.
Sadio Kanute.
Mohamed Ottara.
Peter Nada.
Okra.

Wachezaji wa Nyumbani.

KIBU Denis.
Habib Kyombo.
Erasto Nyoni.
John Boko. Na
Gadiel Michael.

Hawa wachezaji Kwa sasa hawana Hadhi ya kuwa Simba.
Hawawezi kufika Nusu Fainali.
Hahahahaa... alaf waje kinanani kwenye hizo nafasi?
 
Unaitikia amina kwani ni dua hiyo mkuu?


Then yaani mkuu nawe umemuelewa na kumuunga mkono mtoa mada au kwa sababu wote mbumbumbu?
Amina maana yake na iwe hivyoo...kwa imani yangu..
Mbona mmepanick hapo bado je tukichukua ndo mtawehuka kabisa 😆 😆 😆...
Mimi sio mbumbu maana najua Simba ikiamua kuchukua ubingwa ipo siku itachukua inaweza isiwe leo...
 
Hebu tuwekee majina ya hao wapambanaji 15 wa Simba watakaoleta ilo kombe la Afrika acha kubwabwaja sana
Manula, Kapombe, Inonga, Outtara, Kennedy, Zimbwe, Nyango, Chama, Phiri, Okra, Putin, Punda, Sakho, Saido, Mkude, Israel, Bocco.

Nihesabie hao kama hawajafika nikuongezee.
 
Sijaelewa zvr. Kwa hiyo utabiri wako utategemea na mapendekeezo yako, au iwe isiwe simba ni bingwa?
 
Madunduka FC hebu tulieni kwanza, mbona mnaota ndoto nyingi kwa mpigo?
Ya Dubai hayajapoa, mnaota na ubingwa wa CAF. Amkeni kwanza usingizini.
Kukukumbusha tu game ilichezwa Abu Dhabi. Dubai kule tunalala tu 😎😎
 
Sijaelewa zvr. Kwa hiyo utabiri wako utategemea na mapendekeezo yako, au iwe isiwe simba ni bingwa?
Iwe isiwe ndugu msikilizaji. Mimi nimesema, nani wa kupingaa?
 
Back
Top Bottom