Utabiri: Simba bingwa wa CAF 2023

Utabiri: Simba bingwa wa CAF 2023

Huu utabiri wako, ulimaanisha msimu huu 2023/24 au uliopita 2022/23?. Maana maneno Yako ya wakati ule ni kama ulimaanisha msimu uliopita. Ila maneno ya Leo ni kama umehamia msimu huu.
Utabiri ulikuwa unahusu msimu wa 2022-2023 ndiyo maana post yangu ya leo ikakumbushia kuwa kama niliweza kutabiri vile bila kuwa na Che Malone, Fabrice Ngoma, Benchikha na maboresho yatakayofanyika hili dirisha dogo, waza itakuwaje msimu huu unaoendelea.
 
Utabiri ulikuwa unahusu msimu wa 2022-2023 ndiyo maana post yangu ya leo ikakumbushia kuwa kama niliweza kutabiri vile bila kuwa na Che Malone, Fabrice Ngoma, Benchikha na maboresho yatakayofanyika hili dirisha dogo, waza itakuwaje msimu huu unaoendelea.
Kwa unavyoiona timu Yako, kuna dalili zozote njema zinazoashiria utimiaji wa bashiri zako?
 
Natoa utabiri huu nikiwa na akili zangu timamu na upeo wa kutosha kuhusu mpira wa miguu.

Mwaka huu 2023 ndiyo mwaka historia mpya inaenda kuandikwa kwa Simba kuchukua kombe la CAF Champions League.

Najua kuna wapenzi wa Simba bado wanalilia kuona usajili mpya ili kuboresha timu ila ngoja nikwambie kitu. Inashangaza watu wanalilia wachezaji waondolewe ambao hata siyo tegemeo kwa timu.

Championship team katika mashindano yoyote, vilabu, taifa inahitaji wachezaji 13 hadi 15 tu wa kutegemea, yaani first 11 na sub 2 hadi 4 zinazoweza kuongeza nguvu pale inapohitajika. Simba timu hiyo wanayo.

Ambacho mimi ningefanya ni kuangalia jinsi ya kuboresha upande wa beki wa kushoto, mipira mingi inapotea kutokea kule. Ikibidi nngemsogeza Zimbwe mbele kama winger anaweza kufanya vizuri zaidi position hiyo. Kwa kuongezea tu Outtara ni mchezaji mzuri ni suala la kuangalia tunamtumiaje.

Ila wachezaji 15 wa kusumbua CAF tunao.
Aisee.....
 
Back
Top Bottom