Utabiri wa Sheikh Yahya Hussein mwaka 2006 na Tanzania kuwa na Rais Mwanamke

Kichuguu

Platinum Member
Joined
Oct 11, 2006
Posts
17,048
Reaction score
22,790
Nimesoma hii article pale kwenya magazeti ya Shigongo, ikanishtua kwa vile inaoneka utabiri wake ulikuwa kweli kabisa. je ni coincidence tu au ni kweli alikuwa anajua kupiga mahesabu ya kuona mbele? Najua kuwa aliwahi kutabiri kuwa mtu yeyote atakayechukua formu kumpiga Kikwete mwaka 2010 angekufa ghafla, watu ndani ya CCM ambao walikuwa wameshapanga mkakati wa kumng'oa Kiwkete mwaka 2010 wakaa kimya kabisa.

ALIYEKUWA Mtabiri maarufu Afrika Mashariki, Shehe Yahya Hussein aliitisha mkutano wa wahariri na waandishi wa habari mwaka 2006 na kuzungumzia utawala wa Rais Jakaya Kikwete ukiwa na umri wa mwaka mmoja tu.

Baada ya kuzungumza hayo nilipata nafasi ya kumuuliza. Je Tanzania baada ya Kikwete inaweza kupata rais mwanamke?

Shehe Yahya alinijibu:

“Baada ya vipindi viwili vya Rais Kikwete atakuja rais ambaye ni mweusi mchapa kazi lakini mchekeshaji sana, hata hivyo atatawaka kwa kipindi kifupi tu hapo ndipo Tanzania itapata rais mwanamke.”

Wahariri na waandishi waliguna kuonesha kutokubaliana naye wakiwemo wahariri wakongwe Hemedi Kimwaga, Yasini Sadiki, Magnus Mahenge na wengine ambao siwezi kuwakumbuka.

Shehe Yahya baada ya kuona tunambishia alichukua ubao kama ule wa darasani na mkononi alishika kutabu kilichoandikwa Astrology: Monthly numerology, akaanza kufanya hesabu kwa fomula anazojua yeye na akatuambia kwamba kwa Jakaya inaonesha atamaliza muda wake wa miaka kumi na lakini ajaye ataongoza kwa kipindi kifupi.

Tulimuuliza ataongoza kwa muda mfupi kwa sababu gani, alisema hayo mengine yeye hawezi kujua lakini akasisitiza kwamba hivyo ndivyo itakavyokuwa. Tulitawanyika pale kila mmoja akiwa anaona kama amepigwa ‘changa la macho’.

Lakini sasa nimeng’amua kwamba kumbe alikuwa akimtabiria mama Samia bila yeye mama kujua tulichokuwa tunafanya.

HAKIKA SHEHE YAHYA ALIKUWA MNAJIMU WA KWELI.

Kumbuka haya yanatokea baada ya miaka 15 ya utabiri wake na mtabiri akiwa katangulia mbele za haki. Sheh Yahya alifariki mwaka 2011. Mungu ampe raha ya milele na amnusuru na adhabu ya kaburini.
 
Kwenye zama hizi za Corona yatasemwa mengi sana.

Kama hatua za makusudi hazitachukuliwa haraka kushughulika na hili gonjwa kisayansi mbona tutarajie kurejea uhuru tena?

Hata hivyo ashukuriwe kirusi wa corona kwa kuwa na mahaba zaidi kwa wanaume siyo wamama!
 
Mweusi, na mchapakazi. [emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]
 
Alishindwa kutabiri kifo chake na namna ambavyo angetimliwa toka kwenye ulaji BAKWATA.
kifo chake alitabiri, na ukitaka kujua hili alianza na kumuandaa mwanae kwa kumpeleka kwenye vipindi vyake radioni na pia alitabiri kifo chake kwa namna ya ajabu (isiyokubalika kidini) alisema: Tarehe fulani(alitaja jina) itakuwa kiama, kama si kiama basi mimi ntakufa, HILI HALIKUWA ZURI KIDINI

Nakweli ndio siku alokufa mwenyewe, jamaa alikiwa vizuri kwenye utabiri japo mimi sio muumini wa mambo hayo
 
Kuna mwamba hapa JF alitoa uzi akieleza kuwa Kuna kiongozi Sana wa ngazi ya juu atapoteza maisha.

Sikumbuki Ni nani maana niliupuuza tu kwa kuamini Ni story , kumbe hapana ilikuwa Ni kweli .

Rest in peace JPM, JIWE, JEMEDARI, COMMANDER, MJOMBA,

IMG-20210321-WA0002.jpg
 
Humu nishakuta uzi wa 2020 mtu akisema rais atakufa na vp atakua rais ila kwa muda mfupi kisha atakua mwingine.

Nishakuta uzi wa 2018 ukisema mtarudi hapa kukoment kwa furaha.

Leo bwana Yahya kuna uzi wake wa kutabiri uongozi wa kipindi kifupi.

Mbona kama vile watu walilijua hili kuanzia mwanzo? Was it so obvious?
Screenshot_2021-03-19-15-37-47-92.jpg
 
Back
Top Bottom