Utabiri Wangu: Bingwa wa Ligi ya NBC 2023/24 ni Azam FC

Unadhani ni rahisi namna hiyo??endelea kuota
 
Azam FC wanaondoka na kombe la NBC PL baada ya kulikosa kwa kipindi kirefu.

Sisi kazi yetu ni kuquote na panapo majaaliwa ya uzima na afya, tuurejelee huu uzi mwaka kesho...
 
Hili swala lipo kihisia zaidi. Ni mapema mno kuweza kutabiri.

Kwanza, hujajua uzito na ujazo wa vikosi husika. Usajili ndo kwanza unaanza. Azam haina hata kocha bado. Haijasajili bado mchezaji mpya.

Pili, Ligi yetu ya NBC wenye kuonyesha kiu ya kulitaka haswa ni wawili. Wanachukua kwa kupokezana, Lunyasi na Utopolo. Azam bado haijajijenga kuwa mtafuta Ubingwa.

Hata kama Azam atachukua, si kwa sababu uliona kiutaalam bali hisia zako zilikuongoza kuropoka.
 
"....Azam haina hata kocha..."

Mkuu upo sawa kweli, ama upo upo tu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…