Kocha ampange Gadieli Maiko nafasi ya Kapombe. Shamte mbele ya Yanga hawezi kumudu.
Kuumizwa kwa Kapombe huenda ulikuwa ni mpango mkakati uliotekelezwa na Yanga, nje ya Uwanja.
Kwani aliyemuumiza Kapombe katika mechi ileile alitaka kumwumiza Chama katika majaribio mawili lakini Chama alimruka.
Wakuumizwa walikuwa ni Kapombe na Chama na huyo Mamluki.
Hakuna namna Jumapili lazima wapigwa, liwe Jua iwe Mvua.
Tumpangie kikosi Kocha wa Simba, nina uhakika Matola atasoma hapa.
Hawa waanze.
1. Manula (azungumze na wachezaji)
2. Gadieli ( akabe sana na kushambulia)
3. Hussein (atulie alijifunga goli la pili ile 2,2)
4. Nyoni ( afanye mazoezi ya spidi ni mzito)
5. Wawa (awapange mabeki)
6. Mkude ( awe makini aache rafu, alitukost)
7. Dilunga ( akabe pia)
8. Fraga (akabe pia)
9. Bocco ( ajiamini aache mchecheto ktk dabi)
10. Chama (atake kufunga anaweza)
11. Kahata ( pasi za mwisho na kufunga)
NB. Wachezaji wote wakabe na kushambulia, wakifika langoni kwanza lazima watazame goli au wenzao ili kuamua kupiga golini au kumpasia mfungaji mwenye kukaa ktk nafasi nzuri ( Mzamilu alitukost kwa kumsindiza Barama kwa macho)
Mabeki haraka warudi nyuma baada ya kunyang'anywa mpira.
Mabeki wahakikishe wanaondoe mipira yote ya juu Kross na Kona.
Yanga watakuja na Mbinu ya kulinda goli pasi ndefu na kushambulia kwa haraka kwa kustukiza, na kujiangusha kwenye mita kuanzia 25, ili wapate faulo au penati apige Morrison.
Mpira uchezwe kasi mwanzo mwisho Simba wana pumzi kupita Yanga. Mchezaji akiwa nje ya mchezo ifanyike Sub haraka.
Bocco achangamke, anacheza kwa woga na Yanga, anawaogopa mabeki wakati anawazidi nguvu na ujanja.
Wachezaji wacheze kwa kujituma dakika zote na sio kutembea uwanjani, ukichoka lala chini utolewe iingie nguvu mpya.
Sub
1. Beno
2. Kagere
3. Maquissone
4. Kenedi
5.Mlipili
6. Shibob
7. Kanda
8.Shamte
Karibu kwa maoni na ushauri