Phillipo Bukililo
JF-Expert Member
- Dec 29, 2015
- 18,487
- 13,611
Mzee Mwinyi ana miaka 96, ameishi juu ya ardhi kwa miongo tisa na miaka sita. Wenye kuishi mpaka kufikia umri huo ni wachache sana. Ni baraka kufikia uzee huo. Pia ni kielelezo cha karama mbalimbali zilizotumiwa kwa nidhamu ya kipekee wakati wa ujana wake.
Mojawapo ya karama hiyo ni ule unyenyekevu usioweza kulinganishwa na ule wa wanasiasa wengi wa vizai vilivyokuja baadae. Mwaka 1975 kulitokea mauaji kule Shinyanga. Waliohusika ni watu wa usalama wa Taifa na vifo vya watu vikatokea. Mzee Mwinyi aliyekuwa mbali wakati unyama huo ukitokea akaandika barua ya kujiuzulu kwa bosi wake Mwalimu Nyerere.
Huo ni uungwana wa hali ya juu, ni somo pia kwa hawa wenye vyeo wa leo hii. Ndege imeanguka baharini na kuua abiria 19, msiba mzito umelikumba Taifa. Tanzia mbalimbali zimeandikwa, wasifu wa marehemu umesomwa katika sehemu kadhaa za TZ.
Uhai wa vijana wenye matamanio na mipango mingi umekatishwa lakini hakuna hata mamlaka moja mpaka dakika hii iliyosimama mbele ya waandishi wa habari na kubeba mzigo wa lawama kwa kukubali kujiuzulu. Kila mwenye cheo anakilinda kama vile ajali ile haimhusu.
Tunaweza kusema ni kuchafuka kwa hali ya hewa ndio kumesababisha kifo, hivyo tukamsukumia Mungu kwamba hali ya hewa aliyoimba yeye ndio imesababisha kifo, huo utakuwa ni utetezi mwepesi tu wa kisiasa. Ndege mpaka kuweza kuruka angani zipo mamlaka nyingi ambazo zinasimamia taratibu zote zenye kuhusika.
Wamekaa tu kimya kama vile hawahusiki, kama vile urushaji wa ndege hauna uhusiano na mamlaka au taasisi za kiserikali. So sad. Watu makini na wenye kujitambua saa nyingi tu tangu ajali itokee wangekwisha kuwasilisha barua ya kujiuzulu, hata kama wao hawana uhusiano wa moja kwa moja na ajali yenyewe.
Mzee Mwinyi akiwa waziri wa mambo ya ndani alikuwa kazini kwake Dar pale karibu na Posta mpya wakati walio chini yake wakitesa na kuua raia wasio na kosa, hakukuwa na simu za kisasa hizi janja zenye kutunza na kurusha picha. Pengine hakuona kwa macho yake hata hayo matukio yalifanyika vipi, ilitosha kwake kupata taarifa na akazitumia kwa ajili ya kuachia ngazi.
Leo hii ni Mzee wa miaka 96 kabakiza miaka minne tu kama akijaaliwa na Mungu kufikisha miaka 100, karne moja kamili!.