Utafanya nini utakapogundua wazazi wako na ndugu waliokuzunguka wote hawakupendi?

Utafanya nini utakapogundua wazazi wako na ndugu waliokuzunguka wote hawakupendi?

Mi nimewahi kuishi najua kabisa sipendwi na yeyote ndani hiyo ilikua mwaka 2003 nilikua mdogo sana si baba wala mama wa kambo au wadogo zangu wote hawakunipenda hata baba yangu mzazi nilifanyiwa manyanyaso mengi niliitwa kila jina la kibaguzi
 

Yeremia 17:5​

BWANA asema hivi, Amelaaniwa mtu yule amtegemeaye mwanadamu, Amfanyaye mwanadamu kuwa kinga yake..

Ukikomaa mwenyewe (with God beside you) unatoboa tu!
 
Mi nimewahi kuishi najua kabisa sipendwi na yeyote ndani hiyo ilikua mwaka 2003 nilikua mdogo sana si baba wala mama wa kambo au wadogo zangu wote hawakunipenda hata baba yangu mzazi nilifanyiwa manyanyaso mengi niliitwa kila jina la kibaguzi
Pole sana mkuu kwa yaliyowahi kukutokea, ulichukua hatua gani vp Unawasiliana nao vizuri kwa sasa?
 
Ndugu yangu kupendwa na binadamu au kujaliwa na binadamu siyo kitu cha maana sana.Jitahidi kuwa na mahusiano ya karibu na Mungu tu utaipata amani ya kweli si kama amani wawezayo kukupa wanadamu.Hallo hujajifunza tu kuhusiana na mahusiano ya karibu yaliyo kuwepo kati ya Makonda,Musiba,na mataga wengineo na Magufuli?Hivi kwa kifupi hujaona tu kuwa mtu yoyote amtegemeaye mwanadamu na kumfanya nguzo yake ana laana?Na ataishi duniani kwa shida sana siyo ndugu tu,haitakiwi hata kuumiza kichwa kama sijui mahusiano yako yanatetereka jaribu kuwa imara kwenye nafsi yako usipende furaha yako ije kwako kutoka kwa watu wengine furaha yako jaribu kuitengeneza kutoka kwako na HAPA NDIYO UTAKUJA KUONA UIMARA WA INTROVERTS HUWA HAWAJALI KABISA KUPATA ATTENTIONS ZA WATU WENGINE YAANI HAZINA MADHARA KWAO KABISA
 
Utafanya au ulifanya nini ulipo tambua kwamba msaada wa wazazi/ ndugu zako kwako ni wakukuchimbia kaburi na kukuzika?
Nitamshukuru Mungu kwa kunipa maatifa ya kutambua hilo.

Nitasonga mwenyewe. Tumeumbwa kukua na kujitegemea.

Watu wema wako wengi sana zaidi ya ndugu uwaaminio kuwa wako sawa na wewe. Fungua box na tazama nje, ishi vizuri tu.
 
Jifunze kuishi bila kutegemea attention za watu au kusikiliza wanajadili nini kuhusu wewe. Hii dunia itakuwa ngumu sana kwako ukiishi kwa kuangalia hisia za watu wengine.
 
Back
Top Bottom