Utafanyaje mkeo au mumeo au mzazi wako akiwa na mambo ya Kishirikina? Hivi ñdivyo utakavyofañya

Dah , ukishaona akili yako ni ndogo kuthibitisha hilo tambua kabisa Mungu hayupo labda tu ni wewe ulishindwa kuelewa walio leta hiyo nadharia ya Mungu walimaanisha nini.

Nadharia ya Mungu haijaletwa
Ila miungu imeletwa.

Duniani kote Watu huamini Mungu yupo aliyeumba mbingu na nchi.

Lakini jamii nyingi ziliamua kubuni miungu inayoonekana ili kuthibitisha yule asiyeonekana
 
Mtu yoyote ambaye haamini katika uwepo wa Ushirikina nae ni mnafiki.

Soma mada uelewe.

Kuamini ushirikina ni jambo moja.
Kutambua uwepo wa ushirikina ni jambo jingine.
Unaweza kutambua jambo fulani lipo lakini usiliamini

Soma kwa ufahamu
 
Nadharia ya Mungu haijaletwa
Ila miungu imeletwa.

Duniani kote Watu huamini Mungu yupo aliyeumba mbingu na nchi.

Lakini jamii nyingi ziliamua kubuni miungu inayoonekana ili kuthibitisha yule asiyeonekana
Watu duniani kote kuamini Mungu yupo sio uthibitisho kwamba kweli Mungu yupo .

Kuna kipindi duniani kote waliamini ugonjwa wa tauni ni laana na tanzania na Africa nzima walishaamini ukimwi ni uchawi , je ilikua ni ukweli?
 
Ugonjwa wowote unaouona duniani ni laana.

Iwe Ukimwi, kisukari, mafua, kikohozi n.k.
Laana maana yake ni adhabu ya kuenenda kinyume na amri na maagizo ya Mungu(wanasayansi huita Nature)

Ndio nikakuambia miaka elfu ijayo Watu watakapotajiwa jina lako wengine wataamini ulikuwepo wengine watasema ni nadharia
 
Fikra zako ni huru mno, kwenye hiyo nadharia yako, na unauwanja mpana mno kwenye hii nadharia ya Mungu muweza wa yote na mwenye kupenda sifa na kuabudiwa .
 
Kwa nini useme ni adhabu na sio asili kwa sababu mwisho wa siku viumbe vyote hufa je ni nan asie pata hiyo adhabu?
 
Fikra zako ni huru mno, kwenye hiyo nadharia yako, na unauwanja mpana mno kwenye hii nadharia ya Mungu muweza wa yote na mwenye kupenda sifa na kuabudiwa .

miungu ndio hupenda kuabudiwa.
Kama Mungu muumbaji angekuwa na sifa ya kupenda kusifiwa na kuabudiwa angeúmba Watu kwa namna hiyo
 
Kwa nini useme ni adhabu na sio asili kwa sababu mwisho wa siku viumbe vyote hufa je ni nan asie pata hiyo adhabu?

Ukila uchafu ukaumwa hiyo ni adhabu ya kosa ulilofanya

Hapo kwenye kufa hapo ndio msingi mkuu wa wanaoamua kumsalimu Mungu ulipo.
 
miungu ndio hupenda kuabudiwa.
Kama Mungu muumbaji angekuwa na sifa ya kupenda kusifiwa na kuabudiwa angeúmba Watu kwa namna hiyo
Ila naona bado ume m single note katika personality katika neno asili au Mungu umetenganisha nadharia yako na binadamu ,ambapo binadamu na kila kitu mpaka mawazo yake nayo ni asili tu.
 
Ila naona bado ume m single note katika personality katika neno asili au Mungu umetenganisha nadharia yako na binadamu ,ambapo binadamu na kila kitu mpaka mawazo yake nayo ni asili tu.

Mawazo ya binadamu yapo ya asili na yapo ya kubuni
Mfano, kuwaza jambo lolote kinyume na matumizi ya asili pia ni ubunifu
 
Ila pia uchafu nao si asili pia kama nadharia yako inavyodai mkuu.
Uchafu ni asili kwa viumbe wachafu.

Ndio maana nikakuambia Mungu hakulazimisha wala sio mpenda sifa.

Tunapokunya Mavi ni uchafu lakini kwa viumbe wengine ni chakula.
Mwanadamu amepewa utashi(akili ya kufanya uchaguzi) wa kuamua kuwa mchafu/maovu au kuwa Msafi/Mwema.

Ushirikina ni uchafu na hufanywa na viumbe wachafu
Na wataishi katika ulimwengu wa viumbe vichafu.
 
Ndio maana nikakuambia Mungu hakulazimisha wala sio mpenda sifa.

Kwa mujibu wa hii sentensi yako unamaanisha Pia huyo Mungu ana personality?
 
Ndio maana nikakuambia Mungu hakulazimisha wala sio mpenda sifa.

Kwa mujibu wa hii sentensi yako unamaanisha Pia huyo Mungu ana personality?

Personality Unazungumzia Utu au haina?
Mtu ni mfano wa Mungu.
Utu ni tafsiri nyingine ya uungu
 
Mawazo ya binadamu yapo ya asili na yapo ya kubuni
Mfano, kuwaza jambo lolote kinyume na matumizi ya asili pia ni ubunifu
Ila huo ubunifu pia umetoka kwenye kiumbe cha asili yani ni sawa ule asali iliyobuniwa kutoka kwenye mali ghafi za asili.
 
Unaandika kwasababu hayajakukuta. My friend, mambo hayo ni mazito sana hasa yanapomhusisha mzazi. Yaache tu kama yalivyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…