UTAFITI: 55% ya wananchi wanaukubali utendaji wa Rais Magufuli 2018 toka 96% ya 2016

Hivi walipata kibali cha kufanya utafiti, na nani kawapa kibali cha kuchapisha huo utafiti?? Ningekuwa mimi NBS basi ningewashitaki hawa . Utafiki wa kiongo kabisa huu
Ahahahahaaaaa just hahahaaaa nimecheka kwa dharau, toka nje ya box uione dunia
 
Kuna tafiti zilisema Lowassa atashinda lakini akapigwa chini subirini 2020 ndiyo mtajua ukweli
Utafiti upi mkuu. Hakuna utafiti hata moja uliwahi kuthibitisha hilo.
 
Sample ya 1200 ndio iwakilishe 50 milioni,hayo masikhara,hiyo Sauti ya Umma ni kampuni/taasisi gani,je sample split ya uwakilishi wa mjini na vijijini ni ngapi,hizi tafiti zingine mhoji anakuwa mhojiwa mwenyewe,zikifanywa pale Ufipa
 
Elimu yetu ni mufilisi kabisa, taasisi inafanya utafiti maswali ni yale yale kila inapofanya huo utafiti wao, hakuna jipya, hakuna utafiti mpya, sijui umaarufu wa Rais, utendaji wa Rais nk..kwa nini hawaleti maswali mapya kwenye utafiti km kwa nini rushwa awamu iliyopita ilikuwa kiwango cha juu sana, kwa nini udanganyifu awamu iliyopita uliongezeka sana kila mahali hewa, kwa nini biashara haramu(madawa ya kulevya), ukwepaji kodi nk vilishamiri awamu iliyopita, kwa nini nidhamu ya kazi na kupenda kazi vilipungua sana awamu iliyopita, kwa nini mabaa na nyumba za starehe viliongezeka sana awamu iliyopita, kwa nini watanzania walipenda sana starehe na anasa awamu iliyopita..na nini athari ya mambo haya kwenye uchumi kwa muda mfupi na muda mrefu kwa taifa...
Ni wazi kabisa huwezi tarajia umaarufu wa Rais uongezeke kwenye jamii iliyokuwa imetopea kwenye lindi la rushwa, wizi, anasa, starehe, udanganyifu, ubaguzi nk.walete mambo mapya yanayotoa fursa ya nchi kujifunza na kutorudia makosa, mambo mepesi mepesi km haya wanayorudia rudia mtu anaweza akakaa mwenyewe akapika matokeo..wanapoteza nguvu na raslimali kurudia rudia mambo ambayo hayajengi chochote kwa nchi.
 
Reactions: UCD
Nadhani hadi 2020, kukubalika kutakuwa kumeshuka hadi 0.5%. Tutaelewana tu!
 
Wazee tu na wasio na elimu ndo wanamkubali. Inaonyesha wazi kabisa yeye ni mtu wa aina gani. Ovyo kabisa
 
Wala usishangae zingatia tu matokea ya tafiti na wala si maoni ya washereheshaji hapa.

Kila mtu anafurahia upande wake, wakati ule namba zilikuwa.upande wao, sasa ni upande wetu na wao wameanza kuwa wapinzani.

Hahahaaaa...numbers don't lie.
 
Nadhani hadi 2020, kukubalika kutakuwa kumeshuka hadi 0.5%. Tutaelewana tu!
Endeleeni na tafiti zenu uchwara ila 2020 atashinda kwa asilimia 98% ndo mtakapoanza kulalamika mmeshindwa! Sample ya watu 1200. This is hopeless utafiti.
 
Nchi hii ni wazee,kina mama hasa wa vijijini na wajinga ndo wanaendelea kumkumbatia shetwani CCM kwa kumpa kura ,ila kiukweli Magufuli ni rais wa ovyo sana ni wajinga pekee ndo wanamkubali huyu jamaa
 
Swali ni kwamba kama 55% ndio wanamkubali na hiyo ni katika mazingira haya ya uoga je wananchi wangetoa maoni haya katika mazingira huru ingekuwaje
 
Hivi walipata kibali cha kufanya utafiti, na nani kawapa kibali cha kuchapisha huo utafiti?? Ningekuwa mimi NBS basi ningewashitaki hawa . Utafiki wa kiongo kabisa huu
Wangesema anakubalika kwa 98% ungesema haya?
Jibu kama muungwana
 
Hawa Twaweza tafiti zao hufanyia wapi make sijawahi kutana na toka nizaliwe! Au mamluki?
 
Mbona ccm mkiwa juu hamulizi utafiti ulifanywa vipi. Mwisho kila moja atabaki bila chama kama mimi hapa!
 
Unajua ujinga ni pamoja na kuamini kuwa Ukimwi haupo ukidhani hiyo itakufanya usipate ukimwi. Wewe ni Kati ya vilaza ambao wanaamini Jiwe ni malaika labda kwa sababu anakupa chance ya kusulubu wengine. Mbona wakati hao hao Twaweza waliposema anakubalika kwa 96% mlishangilia na huku toa hizo kasoro?? Basi kwa taarifa yako hii ilikuwa Mwezi Apr nakuhakikishia ikifanyika leo yupo kwenye 20% au 10%
 
In my own opinion, in tanzania people are now living in fear,and in that atmosphere NOTHING CAN THRIVE,in an atmosphere where fear rules even investors dont want to came and invest,The problem with magufuli is simple, HE THINK HE KNOWS IT ALL, and thats impossible, even us prezo D J TRUMP has advisors.Magufuli thinks development means killing opposition and buying opposition figures,In a country where freedom of speach is not allowed that country is courting disaster.i think the rating of magufuli today is not more than 15%, PERIOD
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…