UTAFITI: 55% ya wananchi wanaukubali utendaji wa Rais Magufuli 2018 toka 96% ya 2016

Halafu unakuta hao waliohojiwa wote ni Wanachama wa vyama vya upinzani pamoja na viongozi wao, kwahiyo ukijumlisha sasa na wale ambao wanamuunga mkono ila hawakuhojiwa unakuta percentage ipo around 96%.
😀😀😀 dah nimecheka sana kwakweli hya cjui niite mahaba niue ama...u made my nyt
 
mkuu kuna taasisi huwa zina heshimika likija swala la utafiti ,hii ni summary ila ukitaka full report nenda kwenye website yao Sauti za Wananchi :: Twaweza.org ina page kama mia na kidogo detail zote utapata inafanywa na ma phd holder wakishilikiana na vijana wenye ufaulu wa juu ngazi za diploma na degree ,mimi nimewahi fanya field pale walikuwa wakitaka kutoa ripoti wanatoa bila kupepesa macho funders wao wengi sio watanzania hawana cha kuhongwa mishahara yao ya nguvu,mkuu ni kweli watu wa kawaida leo hawana mbele wala nyuma ,kampuni zinafungwa ,muulize hata mkeo kaduka kake mauzo yameshuka,vijana ndoto za kujenga walisahau k,kampuni za cement zinathibitisha mauzo kushuka chini ya 40% ,woga umezidi hata baa tunaangaliana kwa machale na nywaji mapombe ya bei rahisi makali kama konyagi,kiroba origina,banana yenye ubora duni yameongezeka ,ulevi wa kukata tamaaa ndo usiseme ,shule za kishua wazazi walikuwa wapiga dili,sasa kama walikuwa wanauza nguo leo ananunua nani?
 
Hopeless
 
Ila awamu hii imetugawanya sana wa Tz. nashangaa kwanini wastaafu hawakusema hili. Ukabila na ukanda ni wa wazi na mleaji tupo.
 
hamna lolote na atashinda kwa kishindo 2020.
 
Ama ni sahihi au sio sahihi, takwimu ni kitu muhimu sana katika kufanya maamuzi. Naamini, kwa takwimu hizi, zitakuwa na manufaa zaidi kwa CCM kuliko vyama vingine kwa kuwa CCM itafanya jitihada ili kujisahihisha kuliko vyama vingine vitakavyobweteka kwa kufikiri takwimu zitaendelea kushuka!
Natamani utafiti kama huu ufanywe tena kwa kipindi kama hiki mwakani (2019).
 
si alisema sishauriki sikuchaguliwa na wafanyabiashara na ukinishauri ndio unapoteza kabisaa!![emoji12] [emoji83] [emoji201]
 
Kuanzia sasa ni vyema CCM ijitafakari sana. Kitakachoangusha CCM ni hali ya maisha huku vijijini. Kila kona wananchi wanalalamika. Fika kwa Watumishi mambo ni yale yale. Huku kwenye Halmashauri ndo basi. Hawana mapato. Afisa Ugani atamfikiaje mkulima kilomita 60 kama hana usafiri. Vivyo hivyo Afisa Elimu, Uvuvi, Mifugo etc. Fika kwa Wahe.Madiwani malalamiko juu ya hali ya maisha na uendeshaji wa Halmashauri ni malalamiko matupu.
 
Rais katika nchi unamlinganisha na nani?

Kwani Tanzania kuna marais wawili ili tulinganishe kati ya Magufuli na huyo rais mwingine?

Kila siku 'live' wewe tu halafu umaarufu wako unashuka? Ajabu!
 
Kama hujui akili yako ni ndogo kuliko mbuzi wa Dar. Maana inahitaji tu akili ya kuvuka barabara kutambua hilo
 
hakuna aliyefaidika ila aliyetarajia kuwa maarufu lengo lake halijatimia na haliwezi kuja kutimia asilani kwani umaarufu ndiyo kwanza bado unazidi kuporomoka kwa speed ya roketi!

[HASHTAG]#2020njooharaka[/HASHTAG] chini ya [HASHTAG]#NEChuru[/HASHTAG]
 
Mmeanza kuhangaika sasa....kwani umaarufu wake ukiporomoka lazima wa mwingine uwe umepanda?? Ndio mjue kuwa watu walishamchoka...mtafuteni Dr Bana wenu afanye utafiti wake fake ili aonyeshe kuwa umaarufu wa jiwe lenu umepanda juu...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…