UTAFITI: 55% ya wananchi wanaukubali utendaji wa Rais Magufuli 2018 toka 96% ya 2016

UTAFITI: 55% ya wananchi wanaukubali utendaji wa Rais Magufuli 2018 toka 96% ya 2016

Umaarufu umeshuka hiyo ni fact, just swallow it Mkuu, umeshuka kwa 41% ndani ya miaka 2 na nusu. kwa kasi hiyo ya kushuka mpaka ikifika 2020 nadhani unajua itakua asilimia ngapi?
 
1200 kwa 30000000
Umehoji watu 12000 kati 30000000 tena watu wazima, Alafu unaitwa utafiti wa watu walioenda shuleni!
Kwa dumpling ipi hiyo!
 
1200 kwa 30000000
Umehoji watu 12000 kati 30000000 tena watu wazima, Alafu unaitwa utafiti wa watu walioenda shuleni!
Kwa dumpling ipi hiyo!
Unajua maana ya sampling?..... Mfano hapa Tanzania maeneo yaliyofunikwa na misitu na misitu mataji wazi ni takriban hekta milioni 40 plus, sasa ikitakiwa uhesabu miti yoote iliyomo humo ndani, urefu wa kila mti na unene wa kila mti utafanyaje? Utavamia kila pori kufanya hiyo kazi?
 
Mod One Mod Two Moderator futeni huu uzi maana hauna ukweli wowote. Ni kipande tu mtu kakaa na kukitengeneza maana hakuna pahala huu utafiti ulipofafanua njia waliyotumia kufanya utafiti, hakuna validity wala reliability ya variable/data zao. Huu ni upotoshaji mkubwa sana, futeni haraka sana!
Tembelea website ya twaweza kwenye section ya "Sauti za wananchi" acha kuropoka ovyo kwa mihemko, utafiti hupingwa kwa utafiti.
 
Twaweza hawaaminiki wanajaribu kutuvuta sisi wa upinzani ili tafiti zao zianze kukubalika na wananchi wengi
 
Twaweza toka alipoondoka Rajani hakuna tafiti tena zenye manufaa kwa nchi..hivi msomi aliyeelimika anatafiti kukubalika kwa kiongozi akilinganisha na viongozi waliopita anafikiri sawa sawa kweli..? ni sahihi kulinganisha miaka mitano ya mwanzo ya urais wa Mwl. Nyerere na miaka mitano ya urais wa Kikwete? kila zama na kitabu chake hata Mzee Mwinyi alikumbusha juzi...Twaweza watafiti mambo mapya yenye faida kwa nchi kama ilivyokuwa wakati wa Rajani, naona kama Twaweza imedumaa sasa.
 
Sasa sisi tufanye nini? basi tusubiri box la kura liseme

Hilo lingekuwa kipimo maridhawa kama lingeheshimiwa, lakini huko ndio upuuzi wa muafrika unapodhihirika. Unakuta ccm wanatoka na mabox ya kura vituoni kibabe kisha wanayajaza na kuyarudisha yakiwa na kura za chama chao. Kisha bila aibu unakuta wanashangilia ile mbaya eti wanakubalika na wananchi! Kibaya zaidi unakuta kwenye wanaoshangilia huo ushindi wa kipuuzi wako mpaka ma professor, PhD holders nk. Katika mazingira hayo wazungu wakituita manyani watu wanakasirika.
 
Sasa sisi tufanye nini? basi tusubiri box la kura liseme
Hivi jiulize wewe tangu uwasikie hao Twaweza je uliwahi kuhojiwa? Au hata angalau ulipita sehemu ukawakuta vijana wao wanaendesha zoezi hili la kuhoji watu?

Mimi kinachonishangaza nchini Uingereza na South Africa nimewahi kukutana na group za research na nikahojiwa lakibi nchini mwangu sijawahi kumsikia mtu akitowa ushuhuda wa kuhojiwa na hawa researchers uchwara

Mimi kwa dhati kabisa naamini tafiti hizi huwa zinaandaliwa mezani na kwenye mtandao tu na kinachotengenezwa hapa ni kutafuta uhalali wa kumpandisha Rais kukubalika kwake muda sahihi ukifika ili hizi tafiti magumashi ziwe kama reference.

Tunakubali sisi ni wajinga lakini si kiwangi hicho wanachorudhania, tunaelewa sana malengo yao ni nini.

Nchi ambayo bunge limetiwa mfukoni hakuna taasisi nyingine yenye ubavu wa kufurukuta.

Haya ni maagizo maalum ya kuwalaghai watu na wafadhili kwamba Tanzania kuna uhuru wa kutoa maoni.
 
Tafiti hupingwa kwa tafiti lema akafanye yake aje kutupa mrejesho hapa vinginevyo porojo tu mnapiga.
 
Back
Top Bottom