i agree with you: Binafsi pia usomi mwingi nao unakuaga tabu kwa watu, nchi hii imejaa wasomi wanaojua kupost matatizo mitandaoni kila siku na sio kuleta masuluhisho: Wananchi wa kawaida ndo wamekua wakifanya mambo makubwa nchi hii, wakati ambao wanaonekana hawajasoma waeshaenda kupiga kazi zao wasomi wetu wamekua mstari wa mbele kwenye uchochezi sana tunaelekea pabaya
Mmm,kwa kiasi fulani uko sahihi, ila nadhani tuhuma zako hazihusu wasomi wote.Mimi huwa naamini kwamba wasomi wameliletea taifa hili maendeleo makubwa.Hawa unaosema hawajasoma na wameliletea taifa maendeleo kumbuka kwamba wanatumia tekinolojia za wasomi!Na hata hivyo sidhani pia kwa upande mwingine kama
commment yako ni sahihi sana,vingenevyo kusingekuwa na haja ya kusoma.Sasa sijui bila shule madaktari,mainjinia,
wafamasia,wahasibu,wataalam wa kilimo,
tehama,mawasiliano nk.nk.tungepata wapi.
Na kuhusu wasomi wanaoleta uchochezi,aah,sijui kwako uchochezi ni nini,mawazo mbadala?Maana isije ikawa mawazo mbadala kwako ndio uchochezi.Najua wapo wasomi wanaotoa mawazo chonganishi,na nikiri kwamba hiyo ni tabia ya mtu mwenye ufahamu mkubwa!Hata hivyo hawa sio wengi na wangeweza kudhibitiwa kwa matunda ya kiutendaji yaliyo wazi na yenye tija kwa wananchi.Matumizi ya nguvu hayasaidii sana,na yatawaongezea tu nguvu na umaarufu.
Labda nizungumzie hawa wanaojiita wasomi waliojiingiza kwenye siasa.Hawa si wawakilishi wa wasomi hasa.Hawa either ni opportunists wenye nia tu ya kujineemesha au wana "kazi maalum." Msomi hasa hana maneno mengi,he deals with mostly experimentation and data.