Rejea hizi tano ni muhimu kwa wanafunzi wahistoria ya siasa Tanzania; na kwa mtafiti yeyote anaetaka kujua chanzo chachuki baina ya Waislam na serikali na chanzo cha hisia kali za kidinizinazoikumba nchi yetu kuanzia miaka ya 1980.
Jan P van Bergen katika kitabu chake, Developmentand Religion in Tanzania, (1981) ametoboa siri kuhusu uadui aliokuwa naoNyerere dhidi ya Uislamu na Waislamu. Kitabu kinaeleza kwa ufasaha jinsiNyerere wakati alipokuwa madarakani alivyokuwa akifanya mikutano ya siri naviongozi wa Kanisa kuweka mikakati ya kuupa nguvu Ukristo. Katika mikutano hiyoNyerere aliwahakikishia viongozi wa Kanisa kuwa anaaunga mkono Ukristo. Kitabuhicho kinaeleza jinsi Nyerere alivyotimiza ahadi yake hiyo kwa Kanisa kwakuhakikisha kuwa anawapa Wakristo nafasi za juu katika serikali na chama. Kitabuhiki kilikuwa kikiuzwa Catholic Bookshop, Dar es Salaam. Lakiniilipokuja kudhihirikia Kanisa kuwa kitabu hiki kilikuwa kinatoa habari nyeti nasiri za Kanisa kuhusu njama dhidi ya Waislam, kwa haraka sana kikaacha kuuzwa.Hadi hivi sasa kitabu hicho ni marufuku kuletwa tena Tanzania.
Kitabu cha pili ni cha Dr John C. Sivalon, KanisaKatoliki na Siasa ya Tanzania Bara 1953 Hadi 1985 (1992). Kitabu hikikinaeleza njama ndani ya serikali kuuhujumu Uislam. Sivalon anafichua kuwakuanzia mwaka 1961 baada ya Tanganyika kupata uhuru, Kanisa lilikuwa na hofumbili. Hofu ya kwanza ilikuwa umoja wa madhehebu za Kiislamu kati ya Sunni,Bohora, Ismailia na Ithnasheri. Hofu ya pili ilikuwa kuhamishwa kwa makao makuuya EAMWS kutoka Mombasa kuja Dar es Salaam. Kanisa lilikuwa linahofu kuwa maliwalizokuwanazo Waasia Waislamu zikitiwa katika shughuli za Waislamu ambaowalikuwa na nguvu kubwa katika uwanja wa siasa zitaathiri maslahi ya Ukatolikikatika Afrika ya Mashariki. Kwa ajili hii Kanisa likatanganza kuwa Uislamu niadui wake na ikaanza mikakati ya hujma dhidi ya Uislamu ili kuudhoofisha.
Kuna kazi mbili zilizoandikwa na Waislamukuhusu uhusiano baina ya serikali na Waislamu. Kazi ya kwanza ni tasnifu yaKiwanuka, 'The Politics of Islam in Bukoba District' (1973); kazi yapili ni makala ya utafiti 'Islam and Politics in Tanzania' (1989) iliyoandikwana BWANA MOHAMMED SAID mwandishiambaye sasa hivi anaandika kitabu kinachoitwa "Mwalimu Julius K.Nyerere, Kanisa Katoliki na Uislamu: Dola na tatizo la Udini Tanzania"
Halikadhalika ipo 'Kwikima Report' (1968)ambayo imeeleza kwa ufasaha tatizo la EAMWS, chanzo chake na mchango waserikali katika kuhujumu umoja wa Waislamu. Taarifa hii inafaa kutumika leokama dira ya kuelewa tatizo la Waislamu wa Tanzania kama ilivyokuwa wakati uleilipotolewa kwa mara ya kwanza.
The Literature Reviews are the bases inresearch. Unapaswa usome matokeo ya tafiti tofauti zilizoandikwa juu ya kituunachotaka kukitafiti ili upate deep insight ya kitu hicho kabla hujaanzautafiti. Unatakiwa pia ufanye Critical Assessment and Analysis, sio tukukurupuka ukaandika kama mwanafunzi wa darasa la saba. Na tabia yaku stereotypejamii fulani ya watu kuwa hawakwenda shule isipokuwa ninyi tu hilo nikosa, watuwapo na vichwa vyao wametulia tu kwakuwa sifa ya kibri na ya majivuno ni yaMungu tu.