Utafiti: Maji yaliyoko chini ya ardhi ni mara 20 ya maji ya mito na maziwa

Utafiti: Maji yaliyoko chini ya ardhi ni mara 20 ya maji ya mito na maziwa

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Bara la Afrika lina maji ya chini ya ardhi ya kutosha na hivyo kupelekea kila mtu kupata maji ya kunywa ya kutosha ili kukabiliana na ukame kwa angalau miaka mitano, na hata katika baadhi ya maeneo, hadi miaka 50.

Hii ni kwa mujibu wa utafiti mpya uliofanywa na shirika la utafiti wa Jiolojia la nchini Uingereza na shirika la hisani, Water Aid, utafiti ambao uliwasilishwa kwenye kongamano la mkesha wa siku ya maji duniani mjini Dakar, Senegal.

Shirika hilo la Uingereza la utafiti wa Jiolojia(BGS) na shirika la Water Aid, baada ya utafiti wa miaka 10 yaligunduwa kwamba Afrika ina akiba ya kutosha ya maji ya chini ya ardhi kuweza kugawa maji kwa watu wote. Hata katika maeneo yenye ukame, kulingana na mtafiti mkuu wa BGS Alan MacDonald, kunaweza kuwa na maji ya kutosha chini ya ardhi.

“Unapogundua rasimali za maji ya chini ya ardhi ni labda mara 20 ya maji tuliyo nayo katika mito ya maziwa ya Afrika. Basi ni ukweli wa kustaajabisha sana, lakini kwa sababu umefichwa mara nyingi huwa hauonekani na husahaulika”, amesema.

Hali hii pia ipo huko Turkana nchini Kenya, mojawapo ya maeneo yenye ukame zaidi barani Afrika, ambapo misafara ya ngamia huonekana kati ya vyanzo vichache vya maji.

Ni mojawapo ya maeneo yaliyoathiriwa zaidi barani Afrika, kulingana na mfumo wa tahadhari ya mapema ya njaa.

Lakini hata huko Turkana, inaonekana kuna maji chini ya miguu ya wafugaji wa ngamia. Kwa mujibu wa ripoti ya 2013, Turkana ina maji ya kutosha chini ya ardhi kuweza kuhudumia Kenya kwa kipindi cha miaka 70. Hata hivyo, utafiti wa serikali umeonyesha maji hayo yana chumvi nyingi.

Hata hivyo, kuna afueni kwa Turkana na Afrika tangu utafiti mwingine wa hivi karibuni wa shirika la BGS, kupendekeza kuwa asilimia 80 ya maji ya chini ya ardhi yanaweza kutumiwa na watu wakayanywa

Chanzo: VOA
 
Ni kweli chini ya ardhi maji ni mengi sana, tatizo linakuja katika uwezo wa mtu mmoja mmoja kuifikia hii water table na hata serikali zenyewe zimeshindwa kuzifikia hizi water table huku wameng'ang'ana na maji ya mito na maziwa ambayo sio sustainable kama underground water.
 
Maajabu aiseee. Bado dhahabu iliyoko kati kati ya dunia
 
Sifa na utukufu viende kwa Muumba wetu. Muhimu kwa Wanadamu Ni kutumia maarifa na kuwa na Upendo. Bajeti silaha mataifa makubwa robo pekee, hakuna binadamu angekosa maji ya kunywa.
 
Ili kuhakikisha kunakuwa na upatikanaji wa maji yakutosha na endelevu katika maeneo yetu hapa nchini serikali na wadau wa maji wangetenga fungu la fedha za kutosha kwa ajili ya tafiti za maji ya chini ya ardhi(geophysical survey)ili kuongeza vyanzo vya upatikanaji wa maji kuliko kutegemea surface water pekee& rainwater harvesting.
 
Sasa kama ni hivyo ni kwa nini hawa wanaojiita mamlaka ya maji bonde mfano RUVU bassin na wengine wanadai haya maji ni yao na ukitaka kujimba kisima kirefu lazima uwaone na ulipie??
 
Sasa kama ni hivyo ni kwa nini hawa wanaojiita mamlaka ya maji bonde mfano RUVU bassin na wengine wanadai haya maji ni yao na ukitaka kujimba kisima kirefu lazima uwaone na ulipie??
Hakuna mtu/taasisi inayomiliki groundwater isipokuwa taasisi imepewa kibali na mamlaka ya kuratibu usimamizi wa groundwater(TANZANIA WATER ACT).ndo maana unatakiwa ufatute kibali Cha kuchimba kisima(drilling permit) na uanishe maji unataka uyatumie Kwa shunghuli gani(kilimo,matumuzi ya nyumbani au kiwanda.nk)
 
Back
Top Bottom