Kuna hivi vifungashio vya bidhaa mbalimbali ambazo zinatengenezwa nchi jirani kama Zambia, Afrika kusini, Kenya, Uganda nk.
Wanatumia lugha ya kiswahili lakini sio fasaha na haileti maana ukisoma.
Kwanini wasi wasiliane na mamlaka husika au kupata mtafsiri awe anatoa tafsiri halisi ya maelezo yao kwenye vifungashio vya bidaa zao.
Niliwahi jaribu kuwaandikia email na kuwaonyesha jinsi ambavyo wametumia lugha lakini haileti maana ipasavyo lakini hawajajibu.
Mfano maziwa ya Parmalat ya Afika kusini na bidhaa za Trade kings companies za Zambia na Kusini mwa afrika kiujumla.