Utafiti: Mwanaume mmoja huweza kuwapa wanawake tisa mimba kwa siku wakati mwanamke hubeba mimba moja kwa miezi tisa

Utafiti: Mwanaume mmoja huweza kuwapa wanawake tisa mimba kwa siku wakati mwanamke hubeba mimba moja kwa miezi tisa

Suley2019

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2019
Posts
2,203
Reaction score
5,628
MBUNGE wa Viti Maalum (CCM), Khadija Nassir, ameitaka serikali kuanzisha programu za uzazi wa mpango kwa wanaume kwa kuwa utafiti mbalimbali unaonyesha wana uwezo wa kuwapa mimba wanawake tisa kwa siku moja.

Akiuliza swali la nyongeza bungeni jana, Mbunge huyo alisema utafiti mbalimbali duniani unaonesha kwamba mwanaume mmoja ana uwezo wa kuwapa mimba wanawake tisa kwa siku moja, wakati mwanamke mmoja ana uwezo wa kushika mimba moja kwa miezi tisa.

“Je, serikali haioni sasa kuendelea na program za uzazi wa mpango ni uharibifu wa rasilimali badala yake programu za uzazi wa mpango zifanyike kwa akina baba?”alihoji.

Akijibu, Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk.Faustine Ndugulile, alisema ni dhana potofu kwamba uzazi wa mpango ni wanawake peke yao.

“Suala la uzazi wa mpango linawahusu wanaume vile vile na sisi kama serikali tunahamasisha kinababa na mama kushiriki kwenye uzazi wa mpango salama,” alisema.

Katika swali la msingi, Mbunge wa Viti Maalum (CHADEMA), Zubeda Sakuru, alihoji serikali ina mkakati gani wa kuwawezesha wakunga wa jadi ili kupunguza vifo vya mama na mtoto hasa maeneo ya vijijini.

Akijibu, Dk. Ndugulile alisema Tanzania iliridhia mkataba wa Uzazi Salama mwaka 1994, katika mkutano uliofanyika Misri.

“Mkataba huo unaelekeza kwamba kila mama anayejifungua atahudumiwa na mtaalamu mwenye ujuzi, kwa kutilia maanani kwamba matatizo yatokanayo na uzazi hayatabiriki na yakitokea uhitaji kutatuliwa na wataalamu wenye ujuzi katika kuokoa maisha na mama na mtoto mchanga,” alisema.

Alieleza kuwa Wizara inawatambua wakunga wa jadi kama watu muhimu katika jamii, hivyo Wizara kwa kutambua umaarufu wao katika jamii, inawatumia kufanya uhamasishaji wa wajawazito kujifungulia katika vituo vya kutolea huduma na ikibidi kuwasindikiza.

Chanzo: Nipashe
 
Kwa hiyo kwa mwezi mwanaume atakuwa na mimba ngapi? na mwanamke mimba mmoja,je, kwa miezi tisa atakuwa na vichanga vingapi? wanaume hebu pangeni uzazi bwana msitutanie.
 
Mwanaume gani atakubali kufanyiwa vasectomy?anayepanga uzazi ni yule anayezaa akishirikiana na na mzazi mwenzake
 
Back
Top Bottom