UTAFITI: Nusu ya Wamarekani wanatamani kufuta akaunti zao mtandaoni

UTAFITI: Nusu ya Wamarekani wanatamani kufuta akaunti zao mtandaoni

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Utafiti uliofanywa na NordVPN umeonesha kuwa 55% ya Wamarekani wanatamani kufuta kabisa akaunti zao mtandaoni. Huku 18% wakitamani kusingekuwa na internet kabisa.

60% wanatamani kufuta taarifa binafsi. Robo yao wanatamani kufuta picha, video na akaunti zao kwenye mitandao ya kukutana na wapenzi(dating sites).

3% wapo tayari kulipa hadi Tsh. Milioni 2.3 ili wasijulikane mitandaoni (wabaki kuwa anonymous).

===
Over Half of Americans Want to DELETE Themselves from the Internet

55% of people in the US would remove their online presence completely if they could - according to a new survey from NordVPN - with 18% responding they wished there was no Internet at all.

60% wanted to erase personal data, around a quarter wanted embarrassing moments, photos, videos or dating profiles erased, while 3% would pay over $1,000 to be anonymous online.
 
Nitakuja niombe JamiiForum wafute taarifa zangu. 😂
 
Utafiti uliofanywa na NordVPN umeonesha kuwa 55% ya wamarekani wanatamani kufuta kabisa akaunti zao mtandaoni. Huku 18% wakitamani kusingekuwa na internet kabisa

60% wanatamani kufuta taarifa binafsi. Robo yao wanatamani kufuta picha, video na akaunti zao kwenye mitandao ya kukutana na wapenzi(dating sites)

3% wapo tayari kulipa hadi Tsh. Milioni 2.3 ili wasijulikane mitandaoni (wabaki kuwa anonymous)

===
Over Half of Americans Want to DELETE Themselves from the Internet

55% of people in the US would remove their online presence completely if they could - according to a new survey from NordVPN - with 18% responding they wished there was no Internet at all.

60% wanted to erase personal data, around a quarter wanted embarrassing moments, photos, videos or dating profiles erased, while 3% would pay over $1,000 to be anonymous online.
Uzi mzuri ila ungetoa sabb kwanini wanatamani ku futa akaunti zao, na kwanini walijiunga in the first place
 
Mkuu itakua ni sababu za kisaikolojia zaidi [emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]

Privacy ni kitu muhimu sana
 
Uzi mzuri ila ungetoa sabb kwanini wanatamani ku futa akaunti zao, na kwanini walijiunga in the first place
Sababu kubwa ni kwamba teknolojia inaishi, na inafika wakati mtu anatamani mambo yake ya nyuma yafutike kwasababu ya mabadiliko ya umri na maisha ya kilasiku. Na pia wakati hufika mtu anatamani usiri kwenye maisha yake.
 
Kufuta sio tatizo bali habari zako zikishaingia kwenye internet aziwezi kutoka.
mfano ccm na viongozi leo wanaongea alafu kesho wanakuja kujuta kuwa yameshaingia na hakuna pakufutia
 
Sababu kubwa ni kwamba teknolojia inaishi, na inafika wakati mtu anatamani mambo yake ya nyuma yafutike kwasababu ya mabadiliko ya umri na maisha ya kilasiku. Na pia wakati hufika mtu anatamani usiri kwenye maisha yake.
Mwanzoni hawakujua kwamba wata zeeka, na technolojia itaku vile vile mbona wengi wana andika vitabu vya biography zao.
 
Kwa kweli ni utumwa sana achana na hizo za kutafuta wapenzi .. hizi tu facebook na instagram na zinginezo ukizichunguza vizuri ni za ovyo sana .

Wachache sana ndio wanazitumia kwa manufaa ila wengi wao wanazitumia ovyo kabsa .

Nimeamua kuachana na mitandao mingi sana na naona akili yangu inatulia sasa maana kuna kajiutumwa fulani hivi.. mara uingie mtandao huu mara ulee utoke uchungulie huku.. inachosha sana na kujizubaisha bure ..

Nimepanga kama sio nataka nifanye biashara sifungui account ni kupoteza mda tu na hakuna kingine , site za kujifunza zipo tu ukizitaka utazipata.
 
Hii ni kwa sababu ya kuweka mambo mengi ambayo yalitakiwa kuwa private kwenye mitandao.
Naamini hata hapa bongo wengi wanajutia kujiachia sana kwenye mitandao na wanatamani nyakati zirudi nyuma ila ndo haiwezekani wakae kwa kutulia tu watakuwa somo kwa wengine.
Ni limbukeni ya media tekinolojia kwa Wazungu kuna watu wanashinda kutofautisha maisha yao private na yapi ku share na jamii hili nimeliona sana kwa wasanni vipukizi, na watu wenye pesa ila wametoka from poor economic background, hawajui kuchuja habari za kushare na jamii
 
Makonda atakuwa kama hao Wamrekani kufuta mambo ya zamani

hasa ile clip anamkaripia Daniel Chongolo alipojaribu kumtetea Mtumishi aliekuwa anatingishwa na yeye akiwa Amiri jeshi wa Dar as salaam mstaafu

nyingine ile ya kuokota Dada wa Kigamboni na kulazimisha ni mtoto wa nje wa Lowassa ili kuleta mtafaruku kwny familia ya yule Mzee muungwana
 
Dah Haji Manara wa Simba angependa kufuta clip zake zote alizokuwa akisema ukweli na kubakiza hizi za sasa za kutetea ugali.
Amemrudia mtalaka wake licha ya kuoa mke mwingine ni uthibitisho kwamba maamuzi yake hayafanywi kwa kutulia.
 
Back
Top Bottom