Zamani watu walipokuwa wakiandika kuwa pengine Mange ana shida ya akili nilikuwa nawapuuzia kwa kuwa sikujua sana ukweli wa yale aliyokuwa akilumbana na wenziye...
Lakini sasa baada ya vuguvugu hili la mabadiliko kuanza na yapo mambo mengi ya kisiasa niyajuayo pengine zaidi yake, nina uhakika kabisa huyu mwanamke anahitaji ushauri...
Ni mtu anayeandika tu kila linalomjia akilini pasipo kupima ukweli, madhara n.k ya hicho aandikacho...
Kuwa mwanasiasa tena mpinzani na kundi jingine haimaanishi ndio uanze kushambulia hadi personality ya mpinzani wako....
Anaandika mambo machafu sana juu ya watu kama Lowassa ilihali hao watu ni wakubwa kuweza kuitwa baba au mama zake...