Babu
Asprin umenichekesha sana lakini pia ulipotaja Mtakuja akili yangu ikaenda mbio kwa ile familia ya kufikirika ya Mr. and Mrs. Daud. Kwa hakika ile familia ilinihamasisha sana kusoma ikiwa pamoja na kuipenda lugha ya malkia. Japo sikuijua.
Babu Asprin, mi ni wa wakati wa 'original' "ninaye ndege mzuri mrembo wa kupendeza" (naskia siku hizi kuna remix kama kweli) "wengine mnawakanyaga", " heri mimi sijasema" tetemeko la ardhi, mkisi mmoja kavuka ziwa nyasa, heka heka mtoni. Enzi ambayo wanafunzi tulikuwa tukipenda elimu japo elimu haikutupenda (shule zilikuwa chache hivyo kufaulu sjui kuchaguliwa ilikuwa kimbembe). Tofauti na sasa hivi, elimu inawapenda wanafunzi lakini wenyewe hawaopendi elimu. Si zamani sana lakini kiasi kuitwa babu now.
Huu utafiti pamoja na mapungufu yake kadhaa, lakini naweza kusimama na kuutetea na hata kuthibitishwa na members.