Utafiti: Wana JF na Avatar zao

Utafiti: Wana JF na Avatar zao

Nimekuwa nikifanya utafiti kwa miaka miwili sasa juu ya tabia za wana JF kwa kutumia aina za avatar wanazotumia. Mpaka sasa nimekutana na members zaidi ya 30 humu.

Kiukweli avatar wanazopendelea kuweka zinafana sana na maisha yao halisi au vile walivyo nk. Au kwa lugha nyingine zinatoa preliminary background ya jinsi walivyo. Ukiona member kaweka avatar ya mrembo mkali, asee ni mrembo kweli si mchezo. Ukiona member kaweka picha la jamaa lina hasira, basi ujue yuko hivyo. Ukiona jamaa kaweka picha ya ya kiroho-mbaya ujue anakaribiana na sifa hiyo. Ukiona kaweka avatar ya kituko fulani hivi, naye ni kituko. Kadhalika na wenye avatar za ki hekima hekima, ni kweli kabisa wapo hivyo. Walioweka picha za wanyama, relatively wana maamuzi na matendo kama ya wanyama. Na wale wasioweka picha means they don't care, na kweli wenyewe wako laissez-faire tu.

Huu utafiti unatoa mwangaza mpya wa aina ya wana JF unaopanga ima kukutana nao au unapochat nao kuwajua japo kwa uchache tabia na mwonekano wao (imaginary). Awamu ya pili ya utafiti huu inaendelea...

NB: sitaanika members niliokutana nao wala "derived instruments & indicators" for privacy.
Sasa mkuu sisi ambao hatujaweka ovatar unatuweka kenye kundi lipi
 
Jambo moja kuhusu mimi....napenda sana watoto.

I have a soft spot for them.

So hapo umekosea. But no big deal.

Ngabu loves the kids[emoji133]
Hahaaa, kwa hiyo analysis nimekosea lakini naona utafiti kwa ujumla wake naona bado unakubaliana na dhana ya avatar.

I like it!
 
Hahaaa, kwa hiyo analysis nimekosea lakini naona utafiti kwa ujumla wake naona bado unakubaliana na dhana ya avatar.

I like it!
Nah..nakubaliana nayo kwa kiasi kidogo sana aisee.

Si zaidi hata ya asilimia 10.

Na hiyo ni kwa sababu kila mtu anaweka picha kwa sababu zake anazozijua mwenyewe.

Sasa unless labda mwenyewe akwambie kuwa hiyo avatar alonayo inamaanisha au inawakilisha nini, wewe huwezi kujua.

Na kwa vile huwezi kujua basi utaishia kukisia na kusadiki tu.

Sababu za mimi kuiweka hiyo avatar hujagusia hata moja kwenye hiyo analysis yako.

Kwa hiyo mkataa [verdict] hapo ni kwamba, si lazima avatar awekayo mtu iwe inamuakisi huyo mtu.

Mtu anaweza tu kuweka avatar kwa sababu labda inampendeza tu machoni mwake, basi.
 
Nakubaliana na utafiti wako kwa 75%
Na nyongeza ID anayotumia mtu inaendana kwa kiasi kikubwa na maisha yake halisi au vile alivyo.
Nadhani hili suala la ID na Avatar lipo kisaikolojia zaidi.
We fanya kwanza utafiti halafu ndiyo uje na conclussion hapo nahisi unekubaliana naye may b labda nawe kakugusa
 
Back
Top Bottom