Utafiti: Wana JF na Avatar zao

Utafiti: Wana JF na Avatar zao

Dah.. Sasa kwa wale wenye id nyingi inakuwaje? Maana kuna watu wana id ya kukopea, kutongozea, kubishania na nyingine za kike mbili ambazo sijui kazi yake[emoji13] [emoji13]
 
Huu utafiti unatoa mwangaza mpya wa aina ya wana JF unaopanga ima kukutana nao au unapochat nao kuwajua japo kwa uchache tabia na mwonekano wao (imaginary). Awamu ya pili ya utafiti huu inaendelea...

imaginary ni kufikirika na sio ukweli na hauwezi kuwa ukweli.
 
Nimekuwa nikifanya utafiti kwa miaka miwili sasa juu ya tabia za wana JF kwa kutumia aina za avatar wanazotumia. Mpaka sasa nimekutana na members zaidi ya 30 humu.

Kiukweli avatar wanazopendelea kuweka zinafana sana na maisha yao halisi au vile walivyo nk. Au kwa lugha nyingine zinatoa preliminary background ya jinsi walivyo. Ukiona member kaweka avatar ya mrembo mkali, asee ni mrembo kweli si mchezo. Ukiona member kaweka picha la jamaa lina hasira, basi ujue yuko hivyo. Ukiona jamaa kaweka picha ya ya kiroho-mbaya ujue anakaribiana na sifa hiyo. Ukiona kaweka avatar ya kituko fulani hivi, naye ni kituko. Kadhalika na wenye avatar za ki hekima hekima, ni kweli kabisa wapo hivyo. Walioweka picha za wanyama, relatively wana maamuzi na matendo kama ya wanyama. Na wale wasioweka picha means they don't care, na kweli wenyewe wako laissez-faire tu.

Huu utafiti unatoa mwangaza mpya wa aina ya wana JF unaopanga ima kukutana nao au unapochat nao kuwajua japo kwa uchache tabia na mwonekano wao (imaginary). Awamu ya pili ya utafiti huu inaendelea...

NB: sitaanika members niliokutana nao wala "derived instruments & indicators" for privacy.
Kuna kaukweli fulani hapa

Mfano Iceman 3D anarandana kabisa na ID yake anaonekana ni mpole sana hata michango yake na ID yake yanadhihirisha hayo


Ila vipi kuhusu wanaobadili avatar mara kwa mara au kuiba avatars za watu?
 
Back
Top Bottom