Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 5,352
- 15,876
Akifungua Mkutano wa siku moja wa kutoa matokeo ya awali ya utafiti huo uliofanyika Ukumbi wa Kariakoo, Mkoa wa Mjini Magharibi, Mkurugenzi wa Kinga na Elimu ya Afya Zanzibar, Dkt. Salim Slim amesema utafiti huo utawezesha kutimiza malengo ya Serikali ya kuondoa changamoto zinazowakumba mama wakati wa ujauzito na baada ya kujifungua.
Dkt. Slim amesema Zanzibar bado inachangamoto na ipo nyuma katika kudhibiti tatizo la Afya ya Akili kwa mama Wajawazito, hivyo katika kukabiliana na hali hiyo Wizara ya Afya kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wanaosaidia sekta ya afya inaenda kuondoa athari zinazochangia hali hiyo ili kulinda afya ya mama na mtoto na kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi.
Amesema matokeo ya utafiti huo yatasaidia kuonesha njia ya kutengeneza afua za kutibu tatizo hilo na kueleza namna mama wajawazito wanavyoathirika na changamoto za afya ya akili hapa nchini.
Upande wake, Mwakilishi kutoka WHO Tanzania, Dkt. Amanda Kimonge amesema uchunguzi wa afya ya akili kwa mama wajawazito unasaidia kubaini mapema tatizo na kutoa matibabu ya haraka.
Amesema imebainika kuwa chanzo kikubwa cha changamoto hiyo ni msongo wa mawazo unaosababishwa na familia zao na mambo mengine, hivyo ipo haja ya kuandaa mazingira bora ya kugundua matatizo mapema ili kuondokana na matatizo ya Afya ya akili kwa mama mjamzito.
Ameongeza kuwa utafiti huu kwa Zanzibar ulianza Januari na uliwahusisha mama wapatao 418 waliokubali kushiriki ukiwa na nia ya kuimarisha afya ya mama wajawazito na baada ya kujifungua.
Naye Mratibu wa Kitengo cha Afya ya Akili Wizara ya Afya Zanzibar, Hamida Naufal Kassim, amesema katika kukabiliana na Afya ya akili kwa mama wajawazito, ipo haja ya kuendeleza utoaji wa huduma katika vituo mbalimbali na kutoa mafunzo kwa madaktari ili waweze kuwapa elimu mama wajawazito juu ya afya ya akili wanapofika vituoni kupata huduma.
Amefahamisha kuwa hatua hiyo itasaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi pamoja na changamoto nyingine za kiafya wakati wa kipindi cha ujauzito na mara baada ya kujifungua.
Upande wa washiriki wa mafunzo hayo ya uchunguzi wa awali wa afya ya akili kwa mama wajawazito wamesema mafunzo hayo yamewasaida kutambua kwa haraka changamoto zinazowakabili mama wajawazito kipindi ca ujauzito wao na baada ya kujifungua na kueleza kuwa moja ya changamoto kubwa ni ukosefu wa mashirikiano ya karibu kutoka kwa baba pamoja na familia katika kipindi hicho.
Uchunguzi wa Afya ya akili uliofanya Zanzibar Januray,2025 ulifanywa katika vituo vitatu vya Afya , Chukwani, Mtofani na Mpendae. Uliofanywa na Wachunguzi Madaktari na wauguzi waliopatiwa mafunzo ya awali katika uchunguzi huo.