Utafutaji wa kiwanja umenifanya nielewe mwanadamu ni hatari sana

Eli Cohen

JF-Expert Member
Joined
Jun 19, 2023
Posts
4,460
Reaction score
13,715
Pesa, Ardhi na Mapenzi.

Hivi ni vitu vilivyo mwaga damu sana, vilivyo karibisha ushetani, vilvyo vunja utu na vilivyo tengeneza uhasama mkubwa sana.

Lakini bado ni vitu vyenye thamani kuliko vitu vyote.

Unapotafuta kiwanja, inabidi uwekeze zaidi katika umakini na upelelezi.

Kuna sehemu nilipata kiwanja, jamaa akawa tayari kuniuzia, lakini kumbe nyuma ya pazia kile kiwanja ni urithi wa watoto wa kaka yake yani baada ya kaka yao kufariki na barua zipo. Yeye akawa amepewa cha nyuma yake ila yeye anang'ang'ania pote.

Kuna sehemu nilipata kiwanja, jamaa akawa ananihakikishia kabisa kuwa hakuna tabu na hadi majirani zake (kabila moja) pale wakawa wanachochea. Lakini kwa bahati nzuri kuna afisa ardhi anaishi pembeni na anamjua mshikaji wangu niliekuwa nae, akatuita pembeni na kuniambia kuwa hapo pana mgogoro jamaa anaekuuzia alinunua kiwanja cha mtu mwingine kwa hio ni kama anataka arushie mtu janga asepe.

Kuna sehemu tena, jamaa ana burgain bei na mimi bei kumbe kiwanja sio chake, ni cha mdogo wake, baadae baada ya kumchimba eti ndio ananiambia sio chake. Kwa hio ina maana bei aliotaka kupatana na mimi ilikuwa kaeka commission yake juu.

KUWENI MAKINI.
 
Viwanja vingi ni bei rahisi na vipo ila mikono mingi na matapeli ndo ujinga wa watu wengi.

Mi mambo ya viwanja niliachana nayo mpaka nipata muhusika maana nilitaka kununua kimoja ,nikatonywa na jamaa hiko kiwanja kina migogoro watu satatu wamauziwa tena kila mtu kapigwa bei tofauti.
 
Kabla hujanunua sehemu tafuta guest uweke kambi kwanza upata taarifa halisi kuhusi ile eneo kwenye madalali kwenye vijue vya kahawa majilani nk taarifa kwa mda mfupi huwezi kupata ukweli watu wanapangwa hata mabalozi wana kua kwenye hiyo dili take your time kutoa pesa......utapeli wa viwanja ni ajira kwa watu siku hizi kuna mtandao.
 
Kuna hivi vinavyotangazwa kila kukicha kwenye maredio vinapatikana mlandizi, bagamoyo, sijui kigamboni na inasemwa ni bei ya chini sana, je uhalali wake upo vipi???

Mwenye taarifa au uzoefu na hili atujuze.
 
Kabisa ni bora ugharamike katika uchunguzi
 
Me Pana mpumbavu aliniuzia kiwanja ubavu wa nyumba yake baada ya kuondoka kurudi nakuta kamuuzia mtu mwingine na keshajenga kabisa na frem,yaani namuangalia huyu Mzee simmalizi sijui nimpe adhabu gani.
Hata pesa za kurejesha Huwa hawana Mimi nataka niuze nyumbani yake.
Hawa wazee wa kiswahili sijui wanaivunia Nini
 
Utapeli wa damuni huo daaaaah
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…