Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 28,297
- 68,017
UTAJIRI NI SIRI, NA SIRI NDIO UTAJIRI WENYEWE
Kwa Mkono wa, Robert Heriel
Kabla hujaanza kutafuta utajiri, basi kwanza kabisa jifunze kuwa na Siri. Huwezi kutafuta utajiri kama huna siri, na kamwe huwezi pata utajiri kama wewe sio mtu wa Siri.
Huwezi pewa nafasi nyeti, nafasi kubwa kama wewe sio mtu wa siri, Siri ndio utajiri wenyewe, siri ndio nguvu, uwezo, na kila kitu katika dunia ya mafanikio.
Huwezi kuwa nabii mkubwa, mchawi nguli, mganga aliyeshindikana, kama huna siri. Ili uwe katika Rank za juu kabisa zaa utajiri ni lazima uwe na siri kubwa, hata ukamatwe uchapwe, uminywe kende, uchomwe na kuchinjwa, bado usiwe mwepesi kuongea mambo yasiyostahili kusemwa.
Amin amin nakumbia, katika hii dunia kuna watu wanajua mpaka siku yako ya kufa lakini kamwe hawawezi kukuambia, kuna watu wanajua kabisa kesho utapata ajali ya Bodaboda lakini hawawezi kukuambia, amini kuna watu wanajua kabisa kesho unaenda kutusua mapesa wakati wewe hujui, lakini hawezi kukuambia.
Watu waliofanikiwa wote duniani kwa ngazi za juu ni watu wa siri, Manabii wote unaowajua na usiowajua wote walikuwa watu wa siri. Wachawi nguli, waganga wa level za juu kabisa ni watu wa siri, kamwe hawawezi kukwambia kitu.
Watu husema dunia haina siri, lakini nakuambia Dunia ina siri nyingi mno,, na siri hizo zinashikiliwa na watu wenye siri.
Utajiri ni Siri kwa sababu yeye aliyetajiri namba moja ambaye ni Mungu mwenyewe, Yeye ni SIRI, hakuna anayemjua na hataki ajulikane. Ila wenye siri amejifunua kwao.
Mungu hapendi mtu kiropo ropo, mtu asiye na Siri kamwe hawezi kuwa karibu na Mungu, kamwe hawezi kuwa Tajiri. Hii inatumika hata kwa Shetani, mtu asiye na siri kamwe hawezi kuwa karibu na Shetani, na huwezi kuwa karibu na hao alafu usiwe tajiri.
Mipango ya utajiri haisemwi na watu wenye siri, wao hutekeleza na inakuwa, lakini mipango inayosemwa kabla haijatekelezwa hiyo kwa asilimia kubwa zaidi ya 95% haiwezi kutekelezeka.
Utajiri ni siri, Utajiri umejificha, Utajiri hupenda watu wenye tabia ya kujifichaa, kutokujionyesha kutokupenda sifa za kijinga jinga.
Ukiona mtu anasema ni tajiri basi jua huyo sio Tajiri, utajiri hauna mdomo bali unavitendo.
Ukiona mtu anakuahidi sana jua hapo utekelezaji ni sifuri, utajiri hauna maneno bali mdomo.
Utajiri ummejificha
Madini na vito vya thamani vimejificha, huwezi ikuta imezagaa zagaa mtaani.
Hata kwenye serikali za dunia, kuna vitengo ndani ya nchi hutakiwa kupewa watu wenye siri sana.
Huwezi pewa wewe mwenzangu na miye kiropo ropo, kila kitu unataka watu wajue, kabla hujafanya unatangaza, ukifeli kukifanya unasingizia umelogwa wakati wewe ndio umejiloga.
Utajiri hauna mdomo, utajiri una vitendo tuu.
Utajiri sio imani, utajiri ni hulka, asili ya mtu, silika ya mtu. Huwezi ukawa tajiri kama huna hulka, asili na silika ya utajiri.
Utajiri sio bahati, utajiri ni jambo la lazima kwa watu wenye asili ya utajiri.
Kama ilivyo kwa umasikini
Umasikini hauji kwa bahati, umasikini ni jambo la lazima kwa watu wenye hulka na asili ya umasikini.
Utajiri unahitaji Usiri
Umasikini unahitaji uwazi
Utajiri unahitaji sheria nyingi
Umasikini unahitaji maisha ya hivi hivi, bila sheria
Utajiri unahitaji Mipango, na kujali kizazi kijacho
Umasikini hauhitaji mipango, haujali kizazi kijacho.
Utajiri una aibu ya kushindwa
Umasikini hauna aibu ya kushindwa
Utajiri hauna visingizio au lawama
Umasikini una Visingizio na lawama.
Utajiri haupendi marafiki wengi
Umasikini unapenda marafiki wengi.
Tajiri hapendi marafiki wengi na ikiwezekana matajiri wengi hawana marafiki bali jamaa tuu.
Lakini Masikini hupenda marafiki wengi, sio rahisi masikini akose rafiki.
Watu hujipendekeza kwa watu matajiri lakini matajiri huwachomolea mbali.
Lakini masikini ndio hujipendekeza kwa watu ili kupata marafiki wengi.
Mtu yeyote mwenye rafiki wengi ni ishara ya unafiki. Watu wenye unafiki ndio huwa na marafiki wengi.
Lakini sio rahisi kwa tajiri kuwa na marafiki wengi, matajiri wengi sio wanafiki, kama hakutaki atakuambia hakutaki, kama hataki kukusaidia atakuambia hataki kukusaidia.
Utajiri ni Siri, na siri ndio utajiri wenyewe.
Tajiri hapendi aonekane anapesa, au anamali hiyo ni moja ya sifa kuu ya tajiri, hata Mungu aliyetajiri namba moja hujifanya hana utajiri na mara nyingi hutenda katika dakika za mwisho.
Masikini hupenda aonekane naye yumo, naye anapesa, anamali, hivyo hujifanya anavaa vizuri ili aheshimike yaani anajidanganya kuwa ana pesa kumbe hana.
Ukiona unatabia ya kutaka kuonekana unapesa, unamali, una nguvu, una uwezo mbele za watu basi jua wewe ni masikini, unahaiba, huika na asili ya masikini.
Ndio maana kuna msemo wa masikini usemao " Mavazi huficha umasikini" Huo ni msemo wa watu masikini, tajiri hashughuliki na mavazi yako, masikini wenzako ndio watashughulika na mavazi yako. Tajiri hafuatilii maisha ya mtu,
Unaweza kukutana na tajiri mkazungumza hata masaa matatu alafu ukaondoka, asijue ulivaa nguo ya rangi gani, ukiona unatabia ya hivi ujue wewe una hulka ya utajiri. Lakini ukiona mtu anaongea na wewe hata dakika tano alafu ukaachana naye, akaja mwingine akakuuliza fulani alikuja hapa ulimuona, wewe ukajibu ndio,; tena nimeongea naye, alikuwa kavaa nguo za rangi hii, na viatu vya namna hii, na pembeni kumechanika, jua wewe upo kundi la masikini.
Masikini huangalia mambo madogo, tajiri hana muda huo;
Unataka kununua kiwanja, unasema, utasubiri sana.
Unataka kuoa au kuolewa unasema, Utasubiri sana
Unataka kuanzisha mradi, unasem, Utasubiri miaka nenda rudi.
Unatafuta kazi au kujiajiri, unasema, utasota mpaka ushangae
Unataka kununua gari, unasema, utatembea soli kama mdudu miaka nenda rudi.
Na kikawaida jamii masikini na watu masikini ndio huwa na tabia ya kusema au kuuliza maswali hayo.
Unakuta mtu hata hamna undugu, anakuuliza;
Vipi unaoa au unaolewa lini?
Utafikiri yeye ni mchungaji ndiye atafungisha.
Utasikia vipi hujapata kazi au ajira?
Utafikiri yeye anayo hiyo ajira, au anataka kukuajiri. Masikini ni wanafiki, wanachotafuta ni habari ya kusema.
Utasikia, vipi mumeo au mkeo hakusumbui?
Mjibu, njoo nikuoe wewe, ili usiwe unaniuliza maswali ya kipumbavu, hata kama ni mtu mzima mjibu hivyo ili akome umbeya.
Utasikia, mpaka sasa huna hata mtoto jamani?
Mjibu, njoo nikuzalishe, kenge wewe.
Sasa unakuta wapenda sifa wakiulizwa maswalli hayo ya kinafiki na watu wasio na msaada wowote kwao, kwa vile wanapenda sifa, nao wanajaa.
Utasikia ooh! Tayari nimeshanunua kiwanja, mwakani namwaga mawe ya msingi, alafu mwezi wa kumi nitaoa au kuolewa. Wewe ni mpumbavu.
Unamjibu yeye, kwani atakusaidia nini, au atachangia nini kama sio unatafuta kukwama.
Mwisho, utajiri wa jambo lolote ile ni siri, na siri ndio utajiri wenyewe.
Ulikuwa nami;
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
0693322300
Kwa sasa Dar es salaam