Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Yakobo aliupataje utajiri mkubwa zaidi kumzidi Mjomba wake Laban?Hakuna siri ya utajiri au kuwa Msiri ndio utajiri . utajiri wa siri unatoka kwa shetani. Neno la Mungu linasema Mungu ndie akupae utajiri . soma kumbukumbu 8:18 Mungu ndiye atupae nguvu ya kupata utajiri Mungu akikupa hakuna cha siri . Matajiri wenye siri utajiri wengi wameupata kwa njia zisizo halali, wizi , dhuruma, kupora , kuua watu, ruswa na ufisadi. ndio maana utajiri wao ni siri. ila tajiri alie pewa na Mungu hakuna usiri soma kina Ibrahimu na selemani, na Ayubu ktk vitabu vya Mungu hakuna siri ktk utajiri wao.
Kwann Mungu aliamua Kumuotesha Ndoto Farao halafu Tafsiri akaamua kuiweka kwa Yusuph na asingempa Farao mwenyewe?Neno la Mungu linasema Mungu ndie akupae utajiri soma kumbukumbu 8:18 Bibilia. Neno alijasema Mungu anatupa kwa siri. utajiri wa siri ni washetani pia kumbuka si kila tajiri ni mkono wa Mungu wengine wameua . wachawi, wanaishi na manyoka ndani wameua watoto na wazazi wao hizo ndizo siri za utajiri sio kila tajiri ni Mungu. utajiri wa Mungu kwake hakuna siri. bali ni baraka.
Soma habari ya Samsoni, kilichomkuta aliambiwa asije akatoa SIRI ya NGUVU ZAKE, akajichanganya akamuambia mke wake..Hizo nguvu alipewa na Shetani au Bwana wa Majeshi?fedha na dhahabu ni Mali ya Bwana Mungu umpa ampendae . sio siri. utajiri wa siri ni washetani hata shetani ni tajiri sana . je? wewe unaongelea utajiri gani? kweli utajiri wa shetani ni siri kubwa uwa mama au mtoto au watoto , kuvunja na kupora na kuua. wizi wa mali mbali mbali na ujambazi kisha ukawa tajiri ndio Maana matajiri wengi na utajiri ni siri kubwa wakikueleza unaweza kuzimia au kufa kabisa.
Kwann Mungu alikuwa anaongea na Musa, peke yake na kumpa maagizo akiwa peke yake? Na kwann wana wa Israel walipotaka Kuongea na Mungu kama ilivyokuwa kwa Musa, ilishindikana?wewe umefikiria siri za kupata utajiri ni siri . ila hujafikiria njia wanazopita Matajiri zikoje na kwanini ? ni siri kubwa nadhani mtoa Mada ni kijana bado mimi ni mzee miaka 64 sasa nyani mzee amekwepa Mishale Mingi. Pia nina Maisha Mazuri sana ila si tajiri . achana na siri ya Mtu tajiri . kwa Mungu hakuna siri . Mungu anampa ampendae utajiri sio kwa siri . hata wewe unae soma ujumbe huu Mungu akupe utajiri kwa Mapenzi yake . siri kwa siri Anae toa kwa siri ni shetani kwa sababu njia zake si halali
SIRI NI YA UFUNGUO WA MAFANIKIO,kuna watu hawana siri ni wawazi na wakweli na uwazi wao uliwapatia utajiri Mkubwa . kuna vitu vitatu ukitaka kufanikiwa maishani Uwe Mwaminifu sana, uwe kweli, uwe Msikivu na Mnyenyekevu. uwe na bidii na juhudi na Maarifa. Mtangulize Mungu kwa kila kitu .
Ni kweli kabisa mkuu.Hanna watu wabaya Kama ndugu, HATA kufungiana rizki na kurogana.
Utakuta miongoni mwa ndugu yako ndo anakulostisha.
[emoji28][emoji28][emoji28]Ndio haya maswali ya masikini yanavyokuwaga,
Wewe hata nikiwa tajiri unafikiri itakusaidia?
Nashukuru mfano bora umejitokeza, na wewe utakuwa Case Study humu Jamvini
Siri ya utajiri ni kujua fursa iko wapi, kazi kwa bidii na adabu
Hii hata mimi imewahi nikuta, nimewahi kuwa nafanya kazi na kampuni fulani, ila kipato changu na aina ya maisha yangu hayaendani kabisa.....sasa kuna mfanyakazi mwenzetu mtu mzima kiasi alinifata na kuniomba sana nimsaidie kumkwamua maana alipo Ana majukumu makubwa isitoshe kipato chake ni kidogo sana.....nikamuonea huruma kwa kumuonesha kamfereji kadogo sana kakupata mshiko.....Aisee sikuamini macho yangu yeye ndio alienda kuwa mwiba katika kazi yangu kama nisingekuwa na misuli mikubwa hata kazi ningeipoteza....sasa hivi kale kamfereji kamezibwa yeye naendelea kuteseka mimi naendelea ku make money....sasa hivi zaidi ya majuto hakuna kingine kinacho mtesa, hawezi hata kuniangalia usoni. SIRI SIRI SIRI.....BINADAMU SIO KABISANtachangia kwa mfano hai,
Kuna jamaa angu, Tunafanya biashara eneo moja.
alnifata kuniomba nimsaidie chimbo la bidhaa flani maana kwa bei anayonunua (sh.850) na Bei ya kuuzia sokoni (sh1000) hamlipi kabisa.
Nkamuonea huruma nkampa chimbo la kununua sh. Sh.220 ili akauze ile ile sh.1000
Baada ya wiki
Mteja anauliza Bei gan hii, unamwambia Elfu moja.
Anakujibu, Mbona flani pale anauza jero jero.
Mfanyabiashara mwenzang mwingine akaja ananiuliza,
Aisee Jamaa anapata wapi mzigo, Pale kwake anauza jero jero rejareja.
Dah!
Nkajua tayar picha ishaungua.
Baada ya hapo,
Ile FAIDA kubwa nliokua naipata kwenye ile bidhaa ikapotea ivyo kabisa na mauzo yakashuka.
NLIJUTA SANA!
Nowdays,
NIMEKUA BANDIDU KABISA,
Kuna baadhi ya machimbo ya hela Hadi mke wangu wa ndoa au Ndugu wa damu sitaki ajue kabisa.
NAUNGA MKONO HOJA, uko sahii Sana mtoa mada
Binadamu pumbavu sanaKisa kingine,
Miaka ya nyuma, nlipata mchongo na wazungu flani.
Ilkua biashara ya kununua magogo Aina flani ya miti kutoka kusini
yanakusanywa, kontena likijaa nawataarifu
Wanakuja na mashine yao, wanayasaga saga mogogo yote yakua unga.
Kisha wanapaki kwenye viroba na KISHA WANANILIPA CHANGU kwa Kila kilo ya unga iliyopatikana Na kuyasafirisha kwenye ndege.
Nikaja nikamdokeza iyo fursa Binamu yangu mmoja Alkua anaishi maisha ya tabu sana.
Lengo lilikua tuunganishe Nguvu, niweze kukusanya mzigo wa kutosha FAIDA iwe kubwa.
Na nkajitolea siku moja naenda kuchukua mzigo nkaenda nae kabisa,
Siku nakabidhiwa malipo yangu, mchakato mzima anauonana KABISA.
Alichokifanya,
Akaanza kuhangaika kuomba omba mitaji kwa ndugu na watu wengine.
Nkashangaa kwny grup la familia,
Katibu wetu kaanzisha Uzi na anaomba wanafamilia wote wamchangie ndugu yetu afanikishe iyo project yake.
Siku sio nyingi nkaanza kuona watu wananifatilia,
Mara niamshwe usiku usiku, polisi wamekuja kunikagua nyumbani.
Nkiendesha usiku, Mara polisi wenye pikipiki wanisimamishe kunikagua.
Mara niitwe na
Nikakamatwa nikihisiwa kufanya biashara ya madawa ya kulevya.
Polisi, ananihoji eti Kuna miti huwa nasaga nasafirisha unga unga.
Nimweleze uwo unga unakazi gani.
Nikakana Kila kitu,
Walinishikilia siku 3.
Yaani ilkua Ni usumbuf JUU usumbufu.
Baadae,
Kule nlikokua nanunua mzigo, wakaanza kunitilia mashaka Kila nkija kununua mzigo.
Mara waanze kunihoji hoji maswali hayana kichwa Wala miguu.
Siku sio nyingi,
Wale wazungu wakaja kuchukua mzigo Kama kawaida,
Baadae nkaja kuskia wamedakwa na polisi usiku airport wakipakia mzigo kwny ndege.
Taarifa zikaenea kua ule unga ulkua inachanganywa na vitu vingine kutengeneza Aina flani ya dawa za kulevya.
Nkaona isiwe tabu,
Nkahama ule mkoa haraka sana na NAMBA ya SIMU nkabadilisha kabisa.
Nkafunga mawasiliano na ndugu na wanafamilia wote.
Almost 2yrs,
Ule upepo ulipopoa ndo nkarejea kwny maisha ya kawaida.
NAJUTA KABISA.
Avatar yako inatisha mkuuu 😁Binadamu pumbavu sana
Ndio siri zenyewe hizo mkuu[emoji16][emoji16][emoji16]Avatar yako inatisha mkuuu [emoji16]
Hahahha!
Ikiwa kijana akipata tuu milioni 10
anaona amepata pesa anaanza kudharau waru, kulewa hovyo, kunya na kukojoa hovyoo, kunyamba na kutema mate hovyo, unafikiri hiyo milioni 10 zitakubali hayo?
😁😁😁😁😁 Duuh 😆Ndio siri zenyewe hizo mkuu[emoji16][emoji16][emoji16]
Mshahara huo wa mtu kwa mweziHivi 10M ni pesa ndefu??
Hivi 10M ni pesa ndefu??
Mshahara huo wa mtu kwa mwezi
Inshort sio hela ya kujivunia kabisa mkuu