Utajiri uliojificha kwenye viatu vya mtumba

Utajiri uliojificha kwenye viatu vya mtumba

Hello

Natumaini ni wazima wa afya mwaka jana mwezi kama huu niliandika uzi kwenye jukwaa ili kuhusu biashara ya viatu


Kwa kweli nawashukuru sana mlipokea ile biashara kwa mikono miwili na watu walinipongeza sana wengine kupitia ule uzi waliijua biashara ya viatu na kufungua maduka magoli nadhani paka sasa maisha yao yamebadilika.

Kwa upande wangu nikiri nimepokea simu nyingi sana na kuonana na watu wengi sana waliokuwa wanataka kuifanya biashara ya viatu .

Kwa kweli kila aliyekuja kwangu nilimpa ushirikiano mzuri na kumsaidia kwa ushauri na kuwatia moyo

Kwenye ule uzi mimi nilikuwa naelezea biashara ya viatu vya special tu

Ila katika watu kutoa maoni kuna mdau mmoja Kyawanjubu alitoa maoni yake kuhusu biashara ya viatu vya mtumba nadhani ile comment yake ni best kabisa kwenye ule uzi .

Kupitia ile comment nilipata wazo la kufungua biashara ya viatu vya mtumba

Kwa kweli niseme wazi biashara ya viatu vya mtumba ukiwa seriously kabisa inabadili maisha yako

Baada ya kusoma yale maoni niliamua nitumie hiyo fursa kufungua biashara ya viatu vya mtumba mara moja

Nilifikiri ni wapi eneo zuri la kufungua hiyo biashara ndio nikakumbuka nje ya mjini kidogo nina eneo langu niliweka hapo kakibanda nauza juis maji nk

Niliona ni sehemu nzuri itayonifaa ikabidi niachane na biashara ya kuuza vinywaji nifunguwe viatu vya mtumba

Kwa haraka sana nikatafuta kijana nikamlipa anirekebishie ilo eneo akapanga vizuri mfuko nikapata level nzuri

Nikamuita fundi akaja kunitengenezea banda

Baada ya matengenezo kukamilika nilichukuwa laki moja nikaenda mlango mmoja kuperemba viatu vya hiyo bei

Kwasababu nilikuwa na mtaji mdogo nilikuwa natafuta viatu vya elfu 6000 elfu 8000 nilipata peaa zangu kadhaa nikaenda nyumbani nikavisafisha vizuri kisha nikaenda golini kwangu kutega nashukuru Mungu siku ya kwanza tu niliuza pea mbili moja niliuza 22000 hiki kiatu nilichukuwa kwa 8000 na kingine 15000 nilikinunua 6000

Kesho yake tena mapema nilienda lango kutafuta viatu vingine kuendelea na biashara ikawa nauza pea moja mbili kwa siku ata tano

Hii biashara ni nzuri sana ina faida kubwa sana kwasababu kwa mwezi lazima niwe na faida 200000 au laki na nusu .

Ndani ya huu mwaka nimeongeza goli lingine la viatu na mambo yangu yapo vizuri kabisa .

nimshukuru Kyawanjubu kwa maoni yake mazuri niwashukuru wote walioshiriki kwenye ule uzi wangu wa kwanza Mungu awabariki sana
Mwisho

Nakaribisha maoni maswali na ushauri

Asante Sana

View attachment 1944305View attachment 1944306View attachment 1944336View attachment 1944337View attachment 1944338View attachment 1944339View attachment 1944340View attachment 1944341View attachment 1944342View attachment 1944345View attachment 1944346View attachment 1944347View attachment 1944348View attachment 1944349View attachment 1944350View attachment 1944351View attachment 1944352View attachment 1944353
hongera sana brother kwa ku-share pamoja nasi sas Mzigo mzur nawza pata sehem gani kwa mwanza?
 
Back
Top Bottom