Utajiri wa kutisha uliopo kwenye biashara ya jezi

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
376,316
Reaction score
871,876
Huu ndio utajiri wa kutisha na wa kweli uliopo kwenye biashara ya jezi za mpira kwa sasa! Tukipiga hesabu za haraka kwa kutumia takwimu rahisi, hizi hapa ndizo namba zinazouma na kufurahisha kwa wakati mmoja:

1. Faida kwa Kila Jezi Moja
  • Bei ya kuuza (Wavaaji): TSh 30,009
  • Bei ya kununua (Jumla): TSh 10,000
  • Faida kwa kila jezi: TSh 20,009

2. Jumla ya Faida kwa Watu Milioni 10
Ukiwa na soko la uhakika la wateja milioni 10 wanaonunua jezi hiyo, hesabu inakuwa hivi:
\(\text{TSh\ }20,009\times 10,000,000\text{\ (Watu)}\)
  • Jumla Kuu ya Faida: TSh 200,090,000,000 (Hizo ni Bilioni mia mbili na milioni tisini za Kitanzania)!
  • Kwanini watu wasitokwe povu😂🙌🏿


 
ok.🐒
 
Ukipata soko zuri na la uhakika hizi bidhaa ndogo ndogo utapata Sana pesa na usipokuwa makini unachanganyikiwa coz ni B's ndo zitasoma...Cha muhimu ni soko la uhakika, hata Kwa Faida ya 5000 Kwa Kila moja bado ni pesa nyingi Sana ukiwa na mamilioni ya wateja, cha muhimu wewe ndio miongoni mwa suppliers wakuu au supplier mkuu wa bidhaa...Bidhaa za Mia Mia, Mia mbili na Mia Tano ndizo zinazowapa Utajiri watu kama kina Bakhresa, MO na Industrialist wengine. Kimsingi Tanzania ukipata Chaka la kupata pesa basi utapata Sana in expense ya wajinga wengi coz peoples hazijali ubora na hawajui na mamlaka hazijali Sana so unafyatua Tu Kwa bei nzuri unakuja kuuza Tambara lako Safi, Ukifanya PR na wadau kadhaa muhimu basi mambo murua.
 
Jezi za club Real Madrid inaongoza wanauza mpaka jezi milioni 3. Jezi za taifa Argentina wanaongoza wanauza jezi karibu 6m. Tz kuuza jezi 10m irakuwa rekodi na huu umaskini hapo bado za kufyatua kibao .
Nimezungumzia kwa mtazamo wa jezi za taifa.. Lakini pia Simba na yanga wanauza almost kwa idadi hiyo
 
Bro jezi zinauzika bongo.. Watu wasingepambana kupata tenda

Mzee baba imagination ya jezi 10mil, ni sawasawa na kwamba watu wote wa Dar es Salaam wakubwa kwa watoto wawe wamenunua jezi, i don't think so...

Bei yenyewe ya jezi tu ni gharama kwa Watanzania wa kawaida...

Na hulka ya watu wengi, huwa wananunua jezi 1, then mtu anaivaa hata miaka 3 kabla hajanunua toleo jingine haswa za Taifa Stars...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…