Utajiri wa Magofu ya Rapta

Duh binafsi leo sijakuelewa kabisa nmefatilia hii stry mwnzo mwisho lakn leo naona ni stry nyingine tofaut
 
Moja kati ya vitu walivyofanikiwa kuvipata Persian kutoka roma ilikua ni sanduku la hazina. Wakati sanduku hilo likiwa limewekwa Ndani ya TRIREMES (meli ya kivita) walijaribu kulivunja lakini walichokuta wasasania ilikua ni mafurushi ya makaratasi.

Kitendo kile cha kukuta makaratasi yale kwenye sanduku wanajeshi waliolichukua sanduku hilo walijiona wote ni wajinga. Kwani hawakuona cha thamani zaidi ya mafurushi ya makaratasi yalipangiliwa utadhani ni kitu cha maana.

Babu yake na Shahzad ndiye aliyekua nahodha wa chombo hicho na ndiye wa mwisho kuondoka na sanduku hilo la hazina. Sanduku lile liliendelea kumilikiwa na ukoo wa Shahzad mpaka ilipofikia miaka ya 350's kuelekea 400AD.

Baadae bwana mmoja kutoka kwenye bloodline ileile ya Shahzad ambaye nae alitumia jina hilo hilo yaani kwa maneno mepesi ni kwamba nae aliitwa Shahzad.

Shahzad huyu wa pili yeye alikua ni mfanya biashara au mchuuzi aliyekua ana langua pembe za ndovu na ngozi za wanyama kutoka pwani ya Africa mashariki na kuzipeleka Syria, Egypt na nchi nyinginezo kama Greece ( ugiriki ya kale).

Wakati huo kulikua na ushindani na wimbi kubwa la wafanya biashara kutoka bara Arab, India, ugiriki na wengine ureno.

Baadhi ya wafanya biashara hususani wareno walitumia neno Azania kumaanisha ni pwani ya Africa mashariki. Huku warabu walitumia neno zenj kumaanisha ni ardhi au nchi inayokaliwa na weusi.

Mara nyingi Shahzad wa pili alikua akifikia miji kama Mogadishu, kilwa, malindi na sofara kwa wakati huo waajemi na waarabu wengi walitumia majahazi kwenye safari zao.

Wakiwa kwenye majahazi yao walitumia pia upepo kuweza kufika Azania au pwani ya Africa mashariki.

Ambapo sasa wafanya biashara kutoka uajemi ya kale, bara Arab na India waliweza kufika Azania kwa kutumia North East monsoons winds.

Waliweza kutumia muda wa mpaka miezi 3 na 4 kulangua bidhaa zao za biashara na kisha wakarudi kwa kutumia aina nyingine ya upepo ulioitwa South West monsoons winds.

Kipindi hicho cha karne ya tatu (3) kuelekea ya nne bwana Shahzad wa pili alifanikiwa kuijua vizuri miji hii ya Azania. Lakini pia aliwajua vizuri wenyeji wake pamoja na mahasimu wake wa biashara ambao kwa sehemu kubwa walikua ni wareno.


Hakika wareno na watu kutoka ghuba ya uajemi na watu kutoka bara Arab hawakua na mahusiano mazuri kwa Wakati huo. Japo walikutana africa kwa shughuli za utafutaji na wote walikua ni wageni wanyonyaji.

Kama ulikua hujui wageni wa mwanzo mwanzo waliokuja Africa hawakuletwa na serikali zao za kikoloni laa hasha, wageni wengi walikua na wajasiria mali.


Naweza sema ni wajasiria mali ambao waliwahi kuona fursa za afrika zikiwemo upatikanaji wa mali ghafi kama pembe za ndovu na dhahabu hivyo wengi walijitosa makundi kwa makundi kama watafutaji wengine tu.

Nadhani baada ya serikali zao kugundua hilo ndipo nazo zikaanza kuingilia resource hizo na hatimae tukafika huku tulipo sasa.

Kilichotokea hapa ni mfano wa wale jamaa wachimbaji madini wanaitana wakipata taarifa kama kuna sehemu kuna mali.

Wana maneno ya utasikia kuna MUITO CHUNYA hapa wanamaanisha huko chunya mali imeanza kutoka haijalishi ni mali gani.

Sasa hiki ndicho kilitokea kwa nchi za kigeni kwa wakati huo yani ma hustler na watu wengine wapambanaji walipeana taarifa kuhusu Africa na baadae uongozi wa nchi zao uliingilia kati.
( Kuna mengi ya kuelezea kuhusu hili ila muda hauruhusu tuendelee na mengine)

Sasa kulingana na uzoefu alioupata Shahzad wa pili kutoka kwenye aina na biashara alizokua akifanya lakini pia watu wa mataifa mengine aliwahi kukutana nao.

Siku moja aliwahi kuamua kuwa serious na lile furushi la makaratasi yale yaliyopatikana wakati wa vita ya roman-persian ndipo aligundua kitu kwenye michoro ya makaratasi yale.

Furushi lile lilijaa machapisho, na machapisho mengi yalikua wanawahusu baadhi ya watu maarufu wa Roman na ugiriki ya kale. Lilitumika neno Greco-Roman kwenye machapisho yale.


Watu wale walikua ni Marcus Aurelius, Seneca, na Cicero. Lakini kwa kiasi kikubwa alionekana bwana mmoja maarufu kama Claudio Ptolemy ambae kwa wakati huo ndio alikua mwana geografia na mwana hisabati mkubwa kwa ukanda ule.


Mbali na hayo pia alikua ni mwana astronamia mkubwa kwa maeneo yale yote kuanzia misri ya kale mpaka ugiriki na kisha Roman.

Yaliandikwa mengi kwenye machapisho yale lakini kubwa lililomvutia Shahzad wa pili lilikua ni chapisho lililohusu mji ulioitwa rhapta.

Kwani taarifa za mji huo kwake hazikua ngeni kabisa mara kadhaa amekua akikutana na taarifa za mji huo alipokua kwenye safari zake kuelekea Azania. Mji huu uliokwisha kuzama baharini ulisifika kwa kuwa na shehena za akiba ya dhahabu kitu kilichowatamanisha wengi kutamani kufika hapo.

Hapo awali alipata taarifa za rhapta kama mji mkongwe na tajiri barani Africa hivyo basi Shahzad alitamani kufika hapo na kuuona ni namna gani mji huo umebarikiwa utajiri huo.

Kulingana na chapisho la Claudio Ptolemy alionyesha kwenye chapisho hilo ni sehemu gani ndani ya eneo hilo la Azania unaweza kuipata au kufika mji huo wa rhapta.



Ramani hii inaonyesha eneo Ndani ya Azania linalo aminika ndipo mji wa rhapta ulipo.
Picha PDF
 
Tusichanganyikiwe saaana, hayo maelezo ya juu nilikua najaribu kurahisha kile alichokua akikisema Shahzad kwa bwana Schulz kuhusu mji wa rhapta.

Mpaka hapa tumejua kumbe ukoo wa Shahzad ndio ulikuwa na taarifa za rhapta lakini pia mtu wa kwanza kujaribu kufika au kuitafuta rapta alikua ni Shahzad wa pili.

Huyu Shahzad aliyekutana na Schulz yeye ni miongoni mwa vitukuu vya Shahzad wa kwanza aliyejaribu kuitafuta rapta.

Sasa basi huyu jasusi m-Nazi bwana Schulz na Shahzad walifikia wapi harakati zao za kufika rhapta.



Tusijisahau sana haya maelezo yote yametoka kwa Javier, akijaribu kunipa picture juu ya mzungu aliyemuita babu yake kwa mara ya kwanza lakini haikua hivyo.

Babu huyo aliishi mkoa wa Lindi hivyo apa tunaenda kuelewa babu huyo alifikaje lindi kutokea ujerumani.

Babu huyo hakua mwingine ni Schulz ambaye kwa mara ya kwanza alipewa taarifa za rhapta na bwana Shahzad ambaye alikua ni rafiki ake kipindi chote akiwa Iran.

0623329512 Whatsapp

Nimeahidi simulizi nitaiweka mpaka itakapofika mwisho, wanaomtafuta huyo jamaa wa Whatsapp ni wale wenye kuhitaji kusoma kwa haraka na kila siku. Bila shaka wao wameshafika mbali,
 
TUNAENDELEA


Uhalisia wa mambo ulivyo na kulingana na machapisho yale ya Claudio Ptolemy, ni kwamba Ptolemy yeye alionyesha tu ni wapi ulipo mji wa rapta.

Ila Kuhusu ni namna gani rapta ilikua na mali, nguvu pamoja na ushawishi wake kwenye eneo lote kuzunguka azania kiukweli Claudio Ptolemy hakuandika chochote kwenye machapisho yale.

Sasa Shahzad wa pili yeye alipata kusikia habari za mji huu wakati Akiwa kwenye biashara zake huko azania (ukanda wa Africa mashariki).

Mara nyingi wafanya biashara hawa wa bara Arab walipokutana waliongea kuhusu mali iliyopo ndani ya mji huo uliozama baharini kwenye bahari ya Indi.


Baada ya kupita miaka 170's tangu kuzama kwa mji wa rapta, taarifa nyingi zilizohusu rapta zilibaki kwa wageni kwakua wenyeji walionekana kuwa na madhaifu makubwa kwenye utunzaji wa taarifa

Mara nyingi wenyeji wa pwani ya Africa mashariki walitegemea kurithishana taarifa kwa njia ya masimulizi huku wenzao wageni walitunza taarifa kwenye maandishi.

Wale wataalamu wa history wanaweza kusema kwamba waafrika tulitgemea (masimulizi) oral traditional wakati wenzetu walikua wakihifadhi taarifa kwenye maandishi.

Hivyo kwa kutegemea masimulizi ilikua ni rahisi sana kupoteza history ya sehemu yoyote kwani tulitgemea uwepo wa anaejua history husika. Mara tu msimuliaji anapokufa na historia imekufa.

Kuna wenyeji wachache sana mpaka kufikia karne ya tano ndio walijua kuandika na kusoma, lugha waliyojua kuindika na kuisoma Ilikua ni kiarabu hii ilitokana na wageni wao wa mwanzo mwanzo kua ni watu wa bara Arab.

Hivyo tunaweza kusema wenyeji hawakua na taarifa za uhakika zinazohusu rapta isipokua zile za kusadikika. Hii ilitokana na hao wenyeji kukosa utaratibu mzuri wa kutunza au kuandika historia yao.

Ni jambo la kusikitisha sana kuona waafrika tunaisoma historia yetu ya ndani kupitia machapisho ya wageni yaani wazungu na waarabu.

Shahzad wa pili sasa aliamua rasmi kuweka makazi yake ukanda huu wa pwani ya Africa ambao ulifahamika kama Azania.


Sababu ya Shahzad wa pili kuweka makazi yake huku Quiloa (kilwa) maeneo ya kuzunguka Azania ilikua ni kuhakikisha anaipata milki au mji ule wa rapta ambao ulizama baharini.

Kulingana na maelezo ya Shahzad ni kwamba sababu za kuzama kwa mji wa rapta bado ni controversial sana.

Kwani kuna nadharia tofauti tofauti zinazokinzana zikielezea sababu hizo, sababu hizi zipo zinazo shikiliwa na wenyeji lakini pia zipo zinazo shikiliwa na wageni.

Hapo baadae tutazielezea nadharia hizo kwa undani katika namna ambayo wageni na wenyeji wa pwani ya azania wanakinzana.



Sasa basi tukumbuke Wakati huu wa huyu Shahzad wa pili, mji wa kilwa au (Quiloa) kama ulivyotamkwa na wareno wa mwanzo. ulikua bado mchanga sana na haujafikia ule umaarufu uliokua nao ambao tulipata kuusikia.

Shahzad alikuja ku settle kilwa (Quiloa) mnamo karne ya tano kuelekea ya sita ili kuhakikisha anaupata mji huu,
na hizi ndio sababu zilizompelekea ku settle kilwa.

Sababu ya kwanza; mnamo karne ya tano na ya sita kilwa ulikua mji mchanga sana ukiwa na idadi ndogo sana ya wageni.

Hivyo kukosekana kwa wageni hususani wale wageni wa kireno na kiingereza kungempa Shahzad uhuru mkubwa wa shughuli yake hiyo.


Hapa tunaweza kuona kwamba mji wa kilwa ulikua kwa kasi kuanzia miaka ya 950's AD au tunaweza kusema karne ya kumi. Lakini mji huu ulianguka ghafla mnamo karne ya kumi na tano yaani mwaka 1505 AD na hii ili sababishwa na ujio wa wareno na waingereza.


Sababu ya pili; Shahzad alikuja ku settle kilwa (Quiloa) kwa sababu tu kulingana na machapisho yale ya Claudio Ptolemy ni kwamba mji wa rapta ulipatikana kaskazini mwa Quiloa ( kilwa). Hivyo kwa kutumia direction hiyo Shahzad aliamini akija ku settle kilwa kazi haitokua ngumu kabisa.

Sababu ya tatu; miongoni mwa machapisho yale aliyokua akiyaangalia Shahzad. Lipo lililohusu au lililomuhusu nahodha wa kigiriki (Greek captain) aliyejulikana kwa jina la Theophilos.

Kulingana na Theophilos yeye alikua anatumia muda wa mpaka siku 21 hadi 22 kutokea horn of Africa hadi kufikia rapta.

Sasa ni hivi kwa Wakati huo ambao technology ya usafiri wa bahari ilikua bado haijakua ni kweli wafanya biashara wengi walitoka Horn of Africa mpaka Quiloa ( kilwa) kwa idadi ya siku hizo hizo.

Hivyo basi chapisho hilo la Theophilos lilimuaminisha kwamba rapta haitakua mbali na kisiwa hicho cha Quiloa.

Tunaposema horn of Africa inajumuisha nchi kama nne hivi ambazo ni Djibouti Eritrea, Ethiopia, Somalia. Hizi ni zile nchi zinazopatikana kwenye lile pembe la Africa.


NB: taarifa hizi za rapta zinatoka kwa Shahzad, sio zile nilizozipata mimi mwenyewe kutoka Tehran. Episode za mbele tutaona taarifa nilizozipata mimi mwenyewe kutoka Tehran nikiwa fatemeh (Manuela).
 
Well
 
😴😴😴😴😴😴😴😴😴😴😴😴😴😴😴😴😴😴😴😴😴😴😴😴😴😴😴😴😴😴😴😴😴😴
 
Daaah!!!


Sijui lin titarud kwa Manuela
 
Niligundua jambo moja kwenye uzungumzaji wa kingereza, yaan kama sio mzoefu wa lugha ile basi ukizungumza mda mrefu namaanisha ukitumia saa nzima, kuna njaa ya ajabu na uchovu vita kupata.
🀣🀣🀣
Aisee.. quite amusing!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…