Basi sikyweki kundi la waandishi, ila kama ulishawahi kuandika hadithi na ikakamilika yote hukupaswa kusema hilo. Waandishi wote huwa hawatamki hayo maana wanajua wanayopitia, siyo mmoja wao ndiyo maana ukasema hayo sikulaumu. Ila napenda nikwambie mimi ni mmoja wa waandishi na hizi zina changamoto kubwa sana kwenye kuziandaa, watu wanapata shida mno mpaka unakiona kisa kikiwa kamili hapo. Kama anataka kutoa kitabu, bado atapitia maudhi ya wahariri ambao anaweza kukurudisha zaidi ya mara tano ukaandike upya hadithi moja hiyohiyo.