Utajiri wa Magofu ya Rapta

Kwaiyo ticts na Hutchinson port nani aliyeanza? Na wakati unajibu hili Kumbuka mkataba wa ticts ni tangu mwaka 2002 kama sikosei.

Sent from my ZTE T1002 using JamiiForums mobile app
 
Au kwa maana rahisi naomba unipangie hizi kampuni kulingana na muda wake,
THA, TICTS na HUTCHINSON PORT tuanzie hapa kwanza

Sent from my ZTE T1002 using JamiiForums mobile app
 
Wazanzibari wameshatuingiza chaka tupeleke kwa Fatemeh tuondoe stress
 
Hutchison port ndo ilianza TICS ikwafuta
Ni hivi chief,

TICTS ilisaini mkataba na TPA mwaka 2000, na mkataba huo umemalizika mwaka huu 2023 na kabla ya mkataba huu hakukuwahi kuwepo na kampuni nyingine hapo awali.

Swali ni je!! Hawa Hutchinson port walioperate kitengo cha kontena kuanzia mwaka gani wakati kwenye mkataba wanasomeka TICTS ina maana hizi kampuni mbili zili operate simultaneously?

NB: Hutchinson port hakuwahi kuwa na mkataba nyuma ya mwak 2000, yaani kuanzia miaka ya 1990's.

Sent from my ZTE T1002 using JamiiForums mobile app
 
Turudi kwenye simulizi yetu wakuu hili la bandari tuliache kwani ujanja wa musa ndio ushamba wa falao.

Sent from my ZTE T1002 using JamiiForums mobile app
jamani kwa hiyo wajinga ndo waliwao , ila usiandike sana hayo mambo ya bandari maana kuna mijitu kazi yao ni kucopy humu na kwenda kujibebea sifa huko twitter wakijifanya ma genius. Andaa article yako ifungulie uzi wake kila mtu asome
 
Mashirika haya ya ujasusi Hufanya hivyo endapo wakiona wanahitaji kukutumia kwenye misheni zao, sababu ya kuchimba sana information za mtu huyo ni kuepuka kushirikisha mtu ambae hawamjui kabisa au mtu ambaye sio sahihi.

Hivyo maswali yangu yalijibiwa kwa staili hiyo japo mara nyingi fatemeh alitumia majibu ya mkato mambo mengine mengi nilijiongeza mimi mwenyewe.

Kuhusu swala la wao kupata passport yangu nalo lilijibiwa vilevile ilikua ni kazi ya MOIS, sasa hapo likaja swali hawa MOIS wanashida gani na Javier kwanini wametumia nguvu kubwa sana kupata wanachokitaka kwa Javier.

Kulingana na fatemeh mi kwamba MOIS wanaepusha mgongano wowote baina yao na CIA kwani baadhi au miongoni mwa wale wanaotaka taarifa zao wapo wenye uraia pacha kati ya marekani (USA) na ujerumani.

Hivyo basi ikumbukwe kuliwahi kutokea mambo kadhaa yaliyohusisha CIA na taifa la Iran miaka ya nyuma kwa maslahi ya marekani.

CIA walilazimika kuingilia mambo ya ndani ya nchi ya Iran na kushinikiza kutolewa madarakani kwa aliyekua shah wa kipindi hicho.

Kwa namna ya kutaka kuepusha migogoro baina ya idara hizo mbili basi MOIS wanafanya kazi zao kwa weredi mkubwa mno huku wakichunguza kila wanaemshirikisha kwenye misheni zao ili kuepuka kuchuja kwa taarifa zao.

Kwa mujibu wa MOIS ni kwamba wamiliki wa mashamba yale wengi hutokea North America na ata CIA wanawatambua vizuri sana.


Lakini pia kuna muingiliano mkubwa kati ya idara hiyo na jamaa ambao ni wamiliki wa mashamba hayo. Jambo hili Ndio linawafanya idara ya MOIS kufanya kazi kwa umakini mkubwa sana.

Hivyo basi fatemeh alipewa taarifa zangu zote kabla ya kunishirikisha kwenye misheni na bila mimi kujua kama nashirikishwa. Walijua weakness zangu walijua strength walijua pia kwanini na kwa namna gani nilifika hapo.

Mwanzoni walijua naweza kuwa nimetokea marekani lakini baada ya kupata zile preliminary information walijiridhisha kama ni m'bongo na hapo wakaenda uchagani kuchimba zaidi ili kunijua.

Mpaka muda huo fatemeh hakutaka maswali tena zaidi alisema mpaka hapo amejitahidi sana kwa kile kikubwa alichoniambia.

Aliniambia alishaandaa chumba ambacho nitalala siku hiyo kabla ya safari,

Aliongea huku tukiwa tunaelekea kupanda rift ya hotel hiyo ambayo juu kwenye flow ya mwisho kulikua na swimming pool nzuri kwa ajili ya kuogelea.

FATEMEH: i have already prepared a room for you
( Tayari nimekuandalia chumba utacholala leo)

Nilishangaa sana........

MIMI:I knew we were sleeping together
( Mi nilijua leo tunalala wote)

Fatemeh alijibu akiwa serious sana,

FATEMEH: not that much easy
( Sio rahisi kiivyo)

Alinifikisha kwenye chumba ambacho nitalala siku hiyo, apa roho iliniuma sana yaani sikuamini kama naondoka narudi bongo bila kumuonyesha ufundi wangu mrembo fatemeh.

Tulipoingia ndani alinipa karatasi na peni ili niandike destination au airport ya mwisho ambayo nitaelekea kutokea pale ili kufika nyumbani. Kwa kinyonge sana niliandika dar es salaam na kumkabidhi karatasi yake.


Fatemeh alijua kama nimekua mpole ghafla na alijua sababu ni nini,

Hapa aliniambia kitu kimoja tu, kwamba hakua tayari kumpa mwanaume yoyote mwili wake kabla hajatimiza ahadi aliyo waahidi wazazi wake lakini pia usiku wa ndoa yake ndio usiku utaoenda kutoa zawadi hiyo kwa yoyote atakae kuwa amemuoa tayari.

Hivyo alisisitiza niache upumbavu nijiandae na safari ya kurud kwa baba yangu Moshi.

Alimalizia kwa kusema ata ile blowjob ya siku ile alijikaza sana kwani hakuwahi kufanya kitu kama hicho kwenye maisha yake. Hivyo jambo lile lilikua katika namna ya kuhakikisha ana niteka, lakini pia anasema alijuta sana kwani alitumia nguvu kubwa kumbe kazi ilikua ndogo sana.

Baada ya maneno yale nilikua mdogo kama punje ya haradani.



Sent from my ZTE T1002 using JamiiForums mobile app
 
Room ile ndani ya hotel hiyo ya Costa del Sol Wyndham ilikua ni Grand residence, kulikua na huduma nyingi sana ndani ya chumba hicho ukilinganisha na room nilizowahi kukaa kwenye hotels nyingine hapo kabla.

Tukiwa ndani kabla fatemeh hajaondoka kuelekea kwenye room yake, nilimuomba fatemeh jambo moja kama ataweza kunisaidia.

MIMI: can you please do me one big favor
( Kama hutojali naomba unisaidie jambo moja )

FATEMEH: what is that thing?
( Ni jambo gani hilo)

MIMI: i need to meet someone at Tehran (Shahzad)
( Nahitaji kukutana na mtu mmoja huko Tehran anaitwa Shahzad)

Fatemeh aliuliza Shahzad ni nani?? Alionekana kutokumjua kabisa wala kusikia taarifa zake mtu huyo.

Nilijaribu kumueleza kwa ufupi sana kama ni mtu ambaye yeye na ukoo wake wanaijua vizuri historia ya mji wa zamani uliopatikana huko pwani ya Africa mashariki.

Mji huo ulizama baharini na hazina kubwa sana ya mali hususani dhahabu. Habari hizo kwa mara ya kwanza niliziskia kwa bwana Javier ambae naye habari hizo alizipata huko Düsseldorf kwa aliyekua veteran wa ki-NAZI bwana Schulz.

Nilimueleza fatemeh nia ya kukutana na jamaa huyo aliyejulikana kwa jina la Shahzad, nia yangu ilikua kuonana nae kama tunaweza kushirikiana turudi tena bongo kupambana na kuona tunaipataje mali hiyo iliyo ndani ya mji huo.

Fatemeh aliuliza kwanini nisirudi tu bongo alafu hilo zoezi nilifanye mi mwenyewe kwani tayari nimeshajua mji huo ulipo kupitia taarifa ya Javier.

Hapa nilimjibu kuwa taarifa za Javier hazijitoshelezi bado kuna uhitaji wa kuwa na ile original document iliyoandikwa na muasisi mwenyewe ambae ni Claudio Ptolemy.

Lakini ukiacha documents hizo, uwepo wa watu wa familia hiyo ni muhimu kwani wao wana taarifa nyingi za ziada zilizohusu mji huo.

Nilimsisitiza kuwa ndani ya nchi yetu sijawahi kabisa kusikia watu wakiongelea mji huo apa maana yake wengi bado hawajui lolote kuhusu mji huo.

Apa nilimsisitiza kuwa ata mimi mwenyewe nilimaliza shule level ya sekondari bila kusikia taarifa zozote kuhusu mji huo.
Fatemeh aliuliza swali lingine ambalo lilikua ni la msingi sana hapa alitaka kujua kama anatakiwa sasa kubadili destination sio tena dar es salaam hivyo nitafatana nae Tehran.

Kwa kujiamini sana nilijibu hivyo kwamba bado nahitaji kufuatana nae ili nikakutane na mtu huyo aliyejulikana kwa jina la Shahzad.

Kuna muda fatemeh alisita lakini nikaona kabisa amekubaliana na mimi kuhusu kughaili safari ya bongo na kuelekea Iran.

Hapa sasa nilipewa masharti machache sana kuhusu Iran na ni kwa jinsi gani nitakaa huko kabla ya kurudi tena dar es salaam.

Fatemeh alisema nikiwa huko sitafanya chochote wala sita kwenda popote wala sitakutana na yoyote pasipo idhini yake.
Kwangu lile lilikua jambo jepesi sana kwani sikua mwenyeji huko hivyo nisinge kua na mishemishe zozote ndani ya mji huo.

Aliendelea kunisisitiza kuwa tulikua na vita mpya tumeianzisha na Javier, hapa aliendelea kusisitiza kama Javier sio mtu wa kawaida alikua na mtandao mkubwa hivyo amani yetu itatengemaa pale ambapo Javier atakua ametiwa nguvuni.

Shida kubwa iliyokua inawapa hofu idara ya MOIS na wale agents wake wengine akiwemo fatemeh, ni kwamba kikundi kile ambacho alikua anatokea Javier kilikua kinapata support kubwa kutoka kwa USA yani (taifa la marekani) lakini pia Israel intelligence service hawakua nyuma kwenye kuwasapot kikundi hiki cha TONDAR pia.



Fatemeh alisema toka kuanzishwa kwake kikundi hicho miaka ya 1999 chini ya bwana mmoja aliyeitwa Fathollah Manouchehri au maarufu kama Farvand Fooladvand.

Kumekuwepo na shaka kubwa baina ya serikali ya Iran kwamba kikundi hicho kilipata support kubwa kutoka kwa washirika wake hao ambao ni marekani na Israel.

Hivyo basi serikali ya Iran inachukulia jambo hili kwa umakini mkubwa kwani linahusisha mataifa makubwa yenye taaluma kubwa ya kiinteligensia.

Na ushahidi waliokua wakiutafuta utaenda pia kuwathibitishia uwepo au ushirika wa marekani kwenye kikundi hicho ambacho serikali ya Iran ilikiita kikundi cha kigaidi.


Hivyo basi fatemeh aliendelea kunisisitiza kuwa tunatakiwa kuwa makini sana ata mimi mwenyewe mpaka muda huo natakiwa kuwa under intensive care mpaka pale jambo lao litakapo kuwa limefikia muafaka.

Fatemeh aliniomba nipumzike, lakini mpaka wakati huo kuna ka uoga kalikua tayari kameniingia baada ya kujua nipo kwenye hatari kubwa muda wowote.

Lakini fatemeh alinitoa hofu hiyo kisha akaniambia kwa uwepo wake eneo hilo hakuna kitu kitaharibika kwani ata room ambayo naenda kulala ipo safe zaidi ndio maana yeye alitangulia hivyo hakuna baya lolote litanipata.

Sura yangu ya uoga na hofu haikujificha kabisa kwa yoyote ambaye angeniona kwani jasho lilinitoka usoni especially baada ya kusikia kuna mkono ata wa Israel kwenye jambo lile dogo sana.

Kwa story nilizowahi kusikia kuhusu Israel niliamini wanaweza ata kuingia ndani ya room ile bila yoyote kujua na kisha wakaondoka na mimi.

Nilitamani kumuambia fatemeh tukalale wote ila nilijua hatowaza kwamba naogopa ila atawaza ni miongoni mwa mbinu zangu za kutaka kuchakata mbususu.

Hivyo niliamua kujikaza kiume tu kwani mpaka wakati huo nimeshapitia magumu mengi nimesha lala kwenye deck ya meli ( hatch cover) usiku kucha tena ndani ya bahari ya pacific.

Sasa napataje uoga kulala kwenye grand residences room nzuri kama hiyo huo utakua ujinga wa kiwango cha rami.



Fatemeh aliondoka na kuniacha room, kwa staili aliyoondoka fatemeh au manuela ni kama mama anaemlaza mtoto na kisha kufunga mlango na yeye kuelekea chumbani kwake.

Kwani baada ya kuondoka fatemeh ( Manuela) nilijifunika blanket bila kuchelewa kwa namna kama najificha.

Sababu ya kufanya hivyo nilikua nahofia mengi sana wakiwemo CIA na hao wazee wa kazi wana wa israel. Kuna muda niliwaza mawazo ya kitoto sana eti ikitokea wamekuja wazee wa kazi wa Israel ( MOSSAD) nitawaambia kuwa mi ni mchaga.

Wote si mnajua zile story zinasema wachaga asili yetu ni Israel, naogopa kusema nitawapa hii story wakati mwingine maana nimeahidi mambo mengi lakini unachotakiwa kujua ni hivyo sisi wachaga huku bongo tulipotea njia kabisa kwetu ni mashariki ya kati.

Kifupi tu wachaga asili yetu ni kaskazini mwa Ethiopia na maeneo ya Eritrea ambapo kuna kabila dogo lenye asili ya huko Israel kabila hilo lilikua kwenye miliki ya watu wa aksumite na liliitwa Beta.

NONDO ZINAENDELEA KUSHUKA WHATSAPP 0623329512

Sent from my ZTE T1002 using JamiiForums mobile app
 
Duuuuuh!!! Ntakesha hapa milele mangi
Tunapoelekea ndio balaa meku, huko juu hii simulizi imeanza kawaida sana ndio maana wengi wakisoma lines mbili tatu wana comments shit wanaondoka ila wangejua kinachofuata.

Anyway tuendelee kula mtori nyama zipo chini.

Sent from my ZTE T1002 using JamiiForums mobile app
 
Mkuu Mugabonihela nafuatilia kwa umakini sana simulizi hii. Iwe ni kweli au ya kutunga, salute mno kwa simulizi nzito. Kama alivyosema member mmoja Msanii kuwa kuna suala ya kisarufi kufanyia kazi. Pia suala la kingereza kwa kiasi kidogo tu. Mfano katika episode hii mwenyeji wako kakutukana hairless chimpanzee. Umeandika hearless chimpanzee na kutafsiri masokwe wagumu kuelewa. Ukweli ni kuwa alimaanisha sokwe wasio na nywele. Tuendelee mkuu. Tuko pamoja ✌️
 
Mi nipo Sana mkuu, tuombe uzima, miongoni mwa nyuzi Kali Sana kuwahi kutokea hapa jf. Ilikuaje Hadi mwamba Javier akakamatwa na kuhukumiwa kifungo Cha maisha mwaka 2020?? Natamani kujua
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…