Utajiri wa Magofu ya Rapta

Dah stori nzuri sana nimehuzunika kwa kifo cha huyo binti sijui hata wazazi wake kama walitambua kuhusu kifo cha binti yao au mazishi yalifanywa na serekali, maana wazazi hawakua na taarifa ya safari zake walijua Yuko shule
 
SEHEMU YA 03

Ras alitumia siku nzima akiwa mashambani na baadae alitumwa kijana mmoja ambae bila kukosea nadhani alikua mwanafunzi wa S.U.A. ambae alinichukua mpaka eneo moja ambalo kwa haraka sikuweza kulitambua. Lakini lilikua ni ghetto la vijana ambao na wenyewe pia niliamini ni wanafunzi. Hapo sikumkuta Ras, zaidi ya kupokea simu iliyonipa maelekezo ya kukagua mzigo uliokua umefungwa kwenye magunia makubwa matano.

Miaka 7 niliyoishi ENGARONI (ARUMERU) ilinifanya kua bora sana linapokuja swala la utambuzi wa ipi ni pure and energetic weed (sativa) na ipi schwag or dirt weed. Na hii ndio sababu iliyofanya Ras azidi kuniamini na kunitumia kwenye deals zake.
Baada ya kukagua mzigo na kujiridhisha nilitoa taarifa na kuludi tena eneo nililokua mwanzo ambako nilimkuta Ras akinisubiri.

RAS: dogo pole na msiba, ingia kwenye gari tunalud dar mda huu.

MIMI: dah!!!!!! sasa broh kama Merry amefariki tunafanyaje maiti yake?
RAS: unataka ukamzike?

Kwa swali lile nilijua kabisa hataki tena tuhusike na mwili wa Merry hivyo nilikaa kimya.
MIMI: broh!! Mbona mzigo tumeuacha?

RAS: mzigo utaukuta dar, unafika saa kumi alfajiri. Kuna gari imebeba mchele inatokea mang'ula ndio itabeba na mzigo wetu calm down janja. Yule jamaa uliemkuta SUGAR REY ndio anaupokea kabla gari haijaingia temeke stereo kushusha mchele.

Tukiwa njiani tuliongea mengi sana na Ras na hapo nilipata
kumjua vizuri na yeye pia alitumia nafasi hiyo kunijua vizuri.
Alinieleza ni kwa namna gani biashara hiyo ilimpa faida kiasi kwamba alisahau kama aliwahi kuwa fired kwenye moja ya kampuni kubwa nchini.

Kwa maelezo ya Ras ni kwamba hapo awali alikua ni operator wa machine inaitwa RTG na SSG (sidhani kama niko sahihi haya majina ya hizi mashine) kwenye bandari ya dar es salaam. Alifukuzwa baada ya onyo nyingi zilizosababishwa na ajali za mara kwa mara zilizotokana na ulevi. Kazi hiyo ilimpa connection kubwa za maderava wa transit ambao walikua wakifata mizigo bandara ya dar es salaam.

Kwa upande mwingine kazi hiyo ilimpa connection ya mabaharia waliokua wanatumia mihadarati. Yaan meli ikifika dar wakati inapakua na kupakia yeye alikua anawajua mabaharia wanatumia either cocaine au bangi hivyo alikua anawaletea ndani humo au anatoka nao na kuwa nunulia dawa hizo nje.

Na hapa ndio ulikua mwanzo wa kuingia kwenye biashara hii.

Kwa maelezo yake mabaharia hao wapo waliokua wanataka wanawake hivyo alijikita pia kwenye kuwa tafutia wanawake mabaharia hao. Japo wanawake hao mara nyingi walilalamika kwamba mabaharia ni watu wa kusodomise, yan ukila dola 200 ya baharia lazima akupeleke kwa mpalange hivyo wapo wadada waliokua wanachukizwa na michezo hiyo japo walikua wakijiuza
.
Tuliongea mengi lakini kubwa aliloonesha kusikitika sana ni kwamba week moja kabla ya kufukuzwa kazi, aliwahi kutoa rushwa ya pesa ambayo hajawahi kuipata hadi leo pesa hiyo. Na hapo ndipo alipoingia rasmi kwenye black market, anasema ilikua ni geti linaitwa 7/8 (saba,nane)..................

Anyway tuliache hili tusiingie sana kwenye taasis za watu.

Tuliingia dar usiku mida ya saa tano na hapo akasema tupumzike sasa kwani tumekua busy siku nzima. Nililala chumba kilekile ambacho nilikua na Merry last night, mbaya zaidi nilikuta hereni zake ambazo inaonekana alizisahau.

TUENDELEE BAADAE WAKUU.
 
Saa ngapi unaendelea
 
SEHEMU YA 03

Nyumba ya Ras ilikua kubwa kiasi kwamba inaweza accommodate zaidi ya familia tano kwa wakati mmoja lakini nilishangaa kwanini anaishi peke ake. Ukaribu wa fukwe pia uliifanya mandhari ya nyumba hiyo kuzidi kua ya kupendeza na kumfurahisha yoyote ambae angeishi ndani ya nyumba hiyo. Ilikua ni mara yangu ya kwanza kulala sehemu nzuri kama ile, lakini pia niliamini kuna shughuli nyingine Ras anafanya inamwingizia kipato kikubwa zaidi ya kile kama sihivyo basi atakua na ushirika na mtu mwingine.

Baada ya mapumziko mafupi aliniamsha na kuniambia tutoke kuna wageni anatakiwa kuwafata na hawezi niacha ndani humo peke angu.

Safari hii tulitoka na gari nyingine aina ya alphard na uelekeo ulikua ni kariakoo tuliingia mtaa mmoja ambao aliniambia unaitwa aggrey. Pale nilinunuliwa simu aina ya iphone 6's na ile simu ndogo niliyokadhiwa na Merry aliichukua yeye, kuna namna Ras hakua ameniamini sana ndio maana hajawahi kuniacha peke angu na alionekana kusimamia mawasiliano yangu yote.

Baada ya hapo tulifanya shopping ndogo ya nguo na kisha tukaanza safari ambayo tulikua tunaelekea kigamboni kupokea wageni. Tulivuka ferry na baada ya kufika upande wa pili tuliendelea barabara iliyonyoosha moja kwa moja, kutokana na ugeni wangu sikujua tunapoelekea lakini nakumbuka tulitumia zaidi ya saa nzima tukiwa barabara ya vumbi.

Baadae tulipita sehemu moja inaitwa kichangani. Baada tena ya mwendo nilishangaa kuona kama uwanja mdogo wa ndege ila haikua tabia yangu kuuliza uliza maswali. Lakini hadi leo najiulizaga sana maswali kuhusu uwepo wa uwanja ule wa ndege mdogo kigamboni.

Ras anaijua dar es salaam kila Kona, kuwa nae kwa zile siku kadhaa nilijikuta nafahamu mengi sana. Likiwemo hili la kukuta kiwanja cha ndege kwenye kapori huko kigamboni maana kwa kipindi kile kigamboni ilikua bado sana sijui kwa sasa ipoje. Na nina uhakika kile kilikua ni kiwanja cha ndege japo sina uzoefu na usafiri huo wa ndege.

Tulitembea kwa kitambo kidogo tukatokea kwenye fukwe nzuri iliyokua imetulia sana huku gari tukiwa tumeiacha umbali wa kama mita 200. Ras hakua mtu wa story sana muda mwingi alikua na sigara ya embassy mdomoni.

Tukiwa fukwe ilikuja boat ndogo na kushusha majitu manne makubwa ya kizungu ambayo yalikua na miili iliyojengeka kwa mazoezi. Miili hiyo ilikua imefunikwa na tattoo mpaka maeneo ya shingo, njemba hizi za kizungu zilikua zimevalia overoll kubwa za rangi ya carrot zikiwa na maandishi mgongoni yameandikwa MAERSK

Hizi njemba zilikua zinapiga kile kingereza cha kimarekani huku Ras alikua ana kizungu chake cha kawaida sana. Nilitumia fursa hiyo kuonyesha kingereza changu cha PCM, lakini kilikua bora kuliko kile cha Ras na Ras alionekana kulifahamu hilo sema kilichompa Ras confidence ni ile kuonana nao mara kwa mara watu wa aina hii.

Ilikua ni mara yangu ya kwanza kukutana na mzungu ambae hajui kiswahili kabisa hivyo siku ilikua ndefu mno. Niligundua jambo moja kwenye uzungumzaji wa kingereza, yaan kama sio mzoefu wa lugha ile basi ukizungumza mda mrefu namaanisha ukitumia saa nzima, kuna njaa ya ajabu na uchovu vita kupata.

Tulisogea mpaka maeneo tuliyokua tume park usafiri na kuanza safari ya kuelekea kijichi. Ndani ya gari kulikua na boxes za Heineken za kutosha jamaa wale walionekana ni watumiaji wazuri wa Heineken hizo. Nikishangaa kuona mmoja wao alikua na radiocall kwenye mfuko wa over roll lake, hiki kitu kiliniacha na maswali mengi sana japo nilishindwa kumuuliza bro Ras.

Baada ya kufika home kijichi jamaa walishuka na kwenda kupata maji kwanza ili miili ikae sawa, na muda huu Ras aliniambia hao ni moja ya washkaji zake ambao alijuana nao kwenye kazi yake ya hapo awali. Hivyo wale jamaa walikua ni mabaharia, asee!!!!! Watoto wa dar wanaojiita mabaharia ni kwamba hawawafahamu tu hao mabaharia wanafananaje!.

Laiti wangewafahamu wangeacha mara moja, kwa haraka niligundua hao jamaa walionekana kutokua hata na hofu ya mungu. Kwa maelezo ya Ras alisema mabaharia ya Maersk na MSC na wale wa meli za kirusi (Russia) wengi ni ma giant ukilinganisha na wale mabaharia ya kifilipino.
Lakini pia kuna meli ndogo za mombasa na Zanzibar zenyewe mabaharia wake ni wabantu wakawaida kama sisi.

Ras aliniuliza kama nipo vizuri kwenye driving, kiukweli nilikua dereva lakini sio kwenye jiji lenye magari mengi kama dar. Udereva wangu ulikua ni kwenye migomba huko moshi kwa kutumia land Rover 110 la Mzee massawe. Nilitamani kuendesha gari dar lakini iwe usiku swala hili lilimchekesha sana Ras.
Ras aliishia kunipa funguo za alphard na kunipa namba ya simu ya mtu ambaye natakiwa kumfuata maeneo ya sinza.

Nilifika sinza kwa mbinde sana ambapo nilikuta timu ya mabinti wazuri nane hivi, nilimkabidhi gari mmoja wapo ambae alikua ni dereva pia ili atuludishe tena kijichi upande wangu niliona changamoto nyingi sana akati nakuja apo sinza.

Baada ya kufika ndani na wale mabinti, nyumba ili badilika kabisa na kua kama casino pombe na unga vilivutwa kwa kwa wingi huku ngono za threesome waziwazi. Nilienda kukaa nje nikipoteza muda kwa kuvuta weed niliyokua nayo mfukoni sikuwa mpenzi wa pombe kwa wakati huo.

Nikiwa nje baharia mmoja alikuja kukaa nami na alijitambulisha kwa jina la McKenzie, swali lake la kwanza ni kwanini nilikua nje kwa wakati huo kwani ndani kulikua na simple Houseparty.
Aliuza je mimi ni Christian ambae sifurahishwi na kalamu za kishetani?


Nilimjibu kama naweza kushiriki lakini wanawake waliokuwepo hawakunivutia kabisa kwani nilihitaji wadada slim na sio BBW kama waliofika hapo. McKenzie alicheka sana kwa upande wake alisema mashine imegoma kabisa kusimama hivyo anahitaji more of cocaine na hewa safi ndipo ataludi ndani.

Tuliongea mengi lakini aliuliza ukaribu wangu na Ras, nilimjibu Ras ni brother wangu baada ya muda Ras alifika na misosi ambayo bila shaka ilikua ni pork. Hawa jamaa wanapenda nguruwe sana na wakija bongo wanapendelea nguruwe wa kienyeji hivyo Ras anamachimbo yake ambapo anachukulia nyama hiyo akijua kama ana ugeni wa namna hiyo.

McKenzie alimfata Ras wakateta kwa muda wa dakika kama 10 kisha McKenzie akaludi ndani kuendelea na ufuska wao.
Walitumia siku nzima kunywa kuvuta na ngono ya hovyohovyo kama mbuzi vile na mimi nilipewa binti mmoja wakunisindikizia siku. Mabinti wa sinza washenzi sana, nilikuja kustuka chuma iko rough road inakata tope la kutosha.

All in all siku iliisha vizuri japo sikumbuki nililala saa ngapi, ila wakati naamka sikukuta mtu ndani na ilikua jioni ya siku ya pili.
Jioni hiyo Ras alilud na kuanza kunipa stories za Peru kwenye mashamba ya koka, akidai McKenzie aliona nafaa sana kwenda huko kama nitakua tayari amjulishe yeye ata ratibu kila kitu kuhusu safari yangu.

HUU NDIO ULIKUA MWANZO WA SAFARI YA SOUTH AMERICA tukutane baadae ilikujua niliishi vipi uko.
 
Kuna sehemu natumia vifupi Mfano neno BBW (big body whores)
MAERSK na MSC hizi ni shipping line
RTG na SSG ni mashine za kisasa za bandari kwa waliowahi kufika bandari kitengo cha kontena ni ile mikonga iliyoingia baharini. Kuhusu virefu vyake sivijui lakini hizo ndio mashine zenyewe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…