wao ni wao
JF-Expert Member
- Dec 23, 2022
- 1,179
- 2,807
Ndimu mkata shombo? [emoji3][emoji3]Buyoye akiiona hii ataenda kuwauzia wajinga telegram[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ndimu mkata shombo? [emoji3][emoji3]Buyoye akiiona hii ataenda kuwauzia wajinga telegram[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Kumekucha...Tuliingia Dubai international airport (DXB) mapema sana tofauti na mawazo yangu ambayo yalinituma kwamba ingetuchukua zaidi ya siku nzima. Airport yao ina passenger terminals kama tatu (3) hivi zikiwa na airlines tofauti tofauti. Kuna free shuttle buses zinazokuwezesha kutoka terminal 1 mpaka terminal 2 na terminal 3 kwa urahisi sana.
Sikuwahi kua mtumiaji wa usafiri wa anga apo awali lakini kwa haraka niligundua airport hiyo inaweza kua miongoni mwa airports kubwa kwenye nchi zile za falme za kiarabu au ata duniani kabisa.
Eneo lote la airport lilikua bize sana huku number ya abiria wanaoingia na kutoka ikiongezeka kila sekunde. Kiasi kwamba kama huna confidence na ni mgeni unaweza kushindwa kujua unatakiwa kuanzia wapi.
Nikiwa eneo la arrivals alikuja bwana mmoja alievalia kanzu na kilemba chekundu chenye drafts nyeupe na akijitmbulisha kwa jina la Mahmoud Huku akitumia kingereza Safi sana.
Mahmoud alisema yupo pale kwa ajili ya mapokezi yangu na kuhakikisha anakamilisha ratiba zangu zote. Alichukua begi langu lililokua dogo na vitu vichache ndani yake kisha tukaingia ndani ya gari na kuanza safari ya kuelekea hotel ambayo niliandaliwa.
Ilituchukua Kama dakika 7 (saba)au 5 (tano) tu kutoka (DXB) mpaka kufika hotel iliyojulikana kwa jina la JUMEIRAH CREEKSIDE HOTEL (Rebat street).
Kwa upande wangu ilikua ni sehemu ambayo sikuitarajia kama nitawahi kufika na nilijiuliza nina kitu gani special mpaka nimepewa mapokezi ya aina ile.
Mandhari ya hotel, wahudumu pamoja na furniture ilionekana sio sehemu ya kawaida kwa mtanzania mchovu kama mimi ku afford mazingira yale. Hili jambo liliniongezea maswali mengi mpaka muda ambao Mahmoud aliponiambia naweza pata chakula kisha nipumzike kwa masaa kadhaa kisha tuendelee na utaratibu mwingine.
Nilifungua begi langu na kutoa baadhi ya vitu na wakati huu niliziona zile hereni za Merry alizoziacha room siku anasafiri na nilijikuta mawazo yameenda mbali hatimae nilipotelea usingizini.
Niliamshwa na simu ya hotel ambayo ilikua inatoka kwa Mahmoud akinielekeza niende nionane nae kwa ajili ya michakato inayofuata kwa siku hiyo kwani muda ulikua mchache sana uliobaki.
Kwa kutumia gari ileile tuliyofika nayo pale Jumeirah hotel tulitoka na kuelekea sehemu moja niliyoitambua kwa jina la Al Raas Private Medical Clinic, Kama ilivyoonekana kwenye documents baada ya check-up ya mwili mzima.
Nilijiuliza maswali mengi lakini hatimae nilikumbuka kuwa kwenye mikataba mingi ya kazi huwa lazima kuwe na medical forms zinazoelezea hari ya kiafya ya muhusika. Kwani hata mashuleni wakati wa ku report hua tunakadhiwa forms ya aina hiyo ili kujua hari ya afya ya mwanafunzi hivyo nilijitoa hofu kwa namna hiyo.
Nikiwa Al Raas medical clinic kwa sehemu kubwa niliona wagonjwa ambao ni wakina mama na baadhi wenye dental appointments. Alikuja bwana mmoja kama singasinga mwenye ndevu nyingi kisha Mahmoud akinielekeza kwamba naweza kumfuata mtaalam huyo.
Tulitembea kitambo kidogo kiasi kwamba nilihisi tumehama kabisa flow ya clinic ile. Kisha tuliingia room moja hivi ambayo haikua na mambo mengi zaidi ya mashine ambazo sikuweza kuzitambua.
Baada ya check-up walikuja jamaa weusi wawili ambao kwa kiingereza chao nilihisi wanaweza kuwa watu wa west Africa especially Nigeria. Walikua ma Giant na wapo serious kiasi kwamba walishindwa kunipa ata Salam, asee! Unapokua nje ya Africa ukimuona mtu yoyote mweusi unahisi anaweza kuwa ndugu yako. Basi mangi nikavunja ukimya bwana!!!
MIMI: hi brothers
NIGERIAN: hi broh, how is everything?
Kabla hatujaendelea na mambo mengine yule singasinga mwenye ndevu nyingi aliwaita jamaa wale ambao nilitamani kuwauliza Mambo mengi. Inaonekana Kama wote tupo safari moja, lakini wao wanaonekana kujua mengi kuhusu safari hiyo pia wanaonekana wanajua mengi kuliko Mimi.
Ndani ya muda mfupi alikuja Mahmoud na kunichukua kisha tukaludi tena kule hotel nilipofikia. Kwa maelezo ya Mahmoud, muda huo alikua anafanya mpango wa safari nyingine ya Colombia ambako ndio kituo changu cha kazi. Alichukua documents zangu Kama passport na vingine kisha akasema tutakutana baada ya masaa matano kuanzia muda huo.
Muda wote huo nilikua na fahamika kwa jina la mustapha, sikuhitaji kuendelea kukaa ndani tena hivyo nilienda eneo moja nje ya hotel kuangalia mazingira. Ila wakati natoka niligundua jambo moja, niligundua wapo wengi wanao ufahamu ujio wangu na wananifuatilia ukiachana na Mahmoud ambae ndio aliyejitambulisha rasmi kwangu.
Nilihisi jambo hilo baada ya kuona baadhi ya watu wakipashana habari kwa namna kama wanaulizana naelekea wapi. Zilipita dakika chache nikamuona Mahmoud ambae alisema atalud baada ya masaa matano ukiwa eneo.
Mahmoud aliuliza kama natafuta sehemu yoyote kwa ajili ya refreshments huku akisisitiza na kuamini kama waafrika wengi ni waraibu wa pombe na wanawake. Kwakua nilikua na uchovu mwingi nilikubali kama ni kweli natafuta sehemu ya kupumzisha akili, Mahmoud alicheka sana kisha akanichukua tena na tukasafiri kwa umbali wa takribani kilimeta 20.
Tulifika kwenye jengo moja ambalo kwa nje unaweza ukahisi ni makazi ya watu lakini ukweli ni kwamba hayakua makazi ya watu. Nilichokikuta ndani mule ilikua ni balaa, nikipata wasaa wa kutosha hapo baadae nitawaeleza mambo baadhi tusiyo yajua kuhusu Dubai.
Nyuma ya pazia Dubai kuna Mambo ya ajabu mengi na starehe nyingi sana japo taifa hili linatumia mwavuli wa dini kuficha baadhi ya vitu. Ila hakuna starehe ambayo utaweza kuikosa Dubai kikubwa uwe na connection na uishi na watu vizuri.
Nilimaliza nusu siku nikiwa pale na baadae mwenyeji wangu Mahmoud aliniamuru tutoke tukajiandae na safari.
Tulitumia zaidi ya masaa 20 kutoka DXB Dubai international airport mpaka (Aeropuerto Internacional Almirante Padilla ) huko Riohacha-colombia kwa kutumia Qatar airways.
Na muda huu niliwaona kwa ukaribu sana wale jamaa zangu niliohisi ni wa Nigeria shida ni kwamba tulikaa siti za mbalimbali sana.
Baada ya kutua Riohacha-colombia wote watatu tulipokelewa na mtu mmoja ambae alijitambulisha kwa jina la Miguel na akatupeleka nje kabisa ya mji huo.
Jamaa zangu wa west Africa mmoja alikua anaitwa Amobi na mwingine obi.........
KWA AMBAO WATATAKA KUISOMA KWA HARAKA ZAIDI WA MUONE HUYU 0623329512 Whatsapp
Kama huna haraka mi nitaipost humu mpaka mwisho wake.
Hahahaha mi nakula za luponda-nachingweaLeta story Mzee sasa hv nasubiria mwendelezo nimekaa kwenye sofa najinywea pepsi baridi na korosho za Newala
Story kali ila leo fupi, hongera kiongoziAmobi na Obi mkataba wao, kazi pamoja na training zilitakiwa kufanyika hapohapo nchini Colombia lakini kwa upande wangu nilitakiwa kwenda Peru.
Mzee wake na Miguel alinitambua kwa jina la mustapha na akitaja taaluma yangu eti nilikua ni chemical processing engineer na alikua na kitambulisho changu cha mzanzibari mkazi. Kwa kua nilishakubali jina hilo hakukua na namna ya kukataa kama sikua mimi kwa hata zile hati za kusafiria ziliandikwa MUSTAPHA ABDUL-QADR MAKUNGU.
Kitambulisho hicho cha mzanzibari mkazi sikuwahi kukiona na sikujua kilifikaje hapo.
Aliendelea kwa kusema mpaka chuo nilichopitia kinaitwa Eduardo Mondlane University, Maputo-Mozambique.
Niliendelea kumsikiliza mzee huyo ambae alikua anaongea kwa uhakika na kile alichokua anakisema huku akiamini ana nijua in and out.
Alitumia kingereza cha ajabu sana kilichochanganyika na kihispania Huku ka rafudhi ka ki Mexican kwa mbali.
Nikiwa naendelea na baba ake na Miguel alikuja mzungu mmoja mrefu mwenye nywele nyingi za blonde. Na kisha kumchukua Amobi na Obi ambao walijaribu kuulizia nyaraka zao hususani passport lakini bila mafanikio waliondoka huku mzungu yule akisisitiza wanachelewa wapo nje ya muda.
Kiukweli tokea tumefika Cabo de la vela niliona treatment yetu imebadilika kwa kiasi kikubwa sana.
Kulikua hakuna tena kubembelezana zaidi ya amri tu, ata swala la chakula kuanzia tuna fika Cabo de la vela ilikua sio option tena bali utakula kile kinachopatikana.
Kwa maelezo mafupi sana bila kurudiarudia, mzee wake na Miguel alisema usiku wa siku hiyo mimi na baadhi ya wenzangu tunaoelekea mashambani tunatakiwa kusafiri na meli ya panama.
Tukiwa ndani ya bus tunaelekea sehemu ambayo sikuweza kuitambua lakini ilikua pembezoni mwa pwani ya Cabo de la vela. Nilizishuhudia sura ngumu zilizokata tamaa ya kuendelea kuishi wengi walikua kama mateja wengine kama vichaa kabisa.
Niliumia baada ya kujua kama wale ndio co-workers (wafanyakazi wenzangu) kwani walinikatisha tamaa ata ya kufikiri kama tuendako kuna uhai kabisa. Ndani ya bus lile kulikua na askari waliovaa kiraia ila ungetambua kama ni askari Kwa kuona mitutu iliyofichwa kwenye koti yao.
Wale wenzangu waliniangalia kwa kunitamani sana huku nyuma ya siti yangu kulikua na mzee wa karibia miaka 60 kwa kumuangalia. Mzee yule alitumia jina la kunta kinte, niliamini ametumia jina lile kwakua nilikua mweusi peke yangu ndani ya basi lile.