MAISHA NDANI YA JIJI LA DAR ES SALAAM
Ilikua ni usiku wa manane merry aliniacha maeneo yale ambayo yalikua ni maeneo ya karibu na ile bar ya SUGAR REY. Nilijisogeza karibu na jamaa mmoja aliekua umbali wa kama mita 100 hivi kutoka ilipo ile bar yeye alikua anafanya biashara ndogo ndogo. Alikua anauza vinywaji especially pombe kali, sigara na vingine vidogo dogo.
Baada ya kukaa na yule jamaa niligundua anauza vitu vingi sana ukiacha vile nilivyoviona. Mfano wateja wengi walikua ni wateja wa condoms na bangi kwa usiku ule. Kwa kua na mimi nilikua mvutaji mzoefu nilinunua ( sigara kubwa) na kuinyonga kwa ustadi wa hali ya juu kitu ambacho kilimvutia sana muuzaji yule (pusher).
Kwa rafudhi yangu ilikua rahisi kugundua kama nilikua mgeni na natokea kaskazini upande wa Arusha. Jamaa aliniomba nisiivutie pale nitafute sehemu nyingine mbali na pale maana police wanapita mara nyingi maeneo hayo.
Wakati nanyanyuka kuelekea eneo la giza ilikuja gari aina ya alteza nyeusi na kupark pembeni ya ile meza ya jamaa anaeuza pombe kali. Waliongea Kama baada ya dakika moja gari iliondoka na yule muuzaji aliniita. Kisha akaniambia nisubiri kuna watu wanakuja kuna deal la masaa kadhaa naweza pata hela ya kula.
"Dogo unaonekana kuwa mzoefu kwenye matumizi ya weed, kuna jamaa watakuja mtaenda kufunga mzigo maeneo ya mbagala" yalikua maneno ya yule jamaa muuzaji. Na mimi sikua na kipingamizi sababu sikua na sehem ya kwenda kwa muda huo.
Walikuja jamaa wawili kwenye pikipiki aina ya sun LG na wakapewa maelezo ya kuondoka na mimi.
"Ras kasema mzigo umefika, mchukueni na huyo janja anaweza kazi. mudi amelewa sana ataharibu kazi" yalikua ni maelekezo waliyopatiwa wale jamaa waliokuja na pikipiki.
Na hapo tukaanza safari ya kuelekea mbagala ilikua mishale ya saa 9 kasoro usiku.
Ilituchukua muda wa dakika 20 kufika maeneo ya sabasaba kwa mpili kisha tulikunja kushoto kuitafuta njia ya kwenda kijichi. Umbali wa mita 150 tulikunja tena kulia na kusimama nje ya nyumba moja kuukuu sana.
Palionekana kua uswahilini sana maeneo yale, nilifanikiwa kuligundua hilo japo ilikua ni usiku sana.
Baada ya sekunde kadhaa niliiona tena ile alteza nyeusi na wakati huu alishuka mwanaume wa makamo mrefu mweusi na mwenye Rasta ndefu zilizoonekana kuwa matunzo ya hali ya juu. Rasta alikua na Heineken mkononi, na alielekea mlangoni na kufungua mlango bila kumsemesha yeyote kati yetu.
RASTA: oyaaa!! Huyu dogo mmemtoa wapi??
Jamaa walijibu kwa uoga sana "boni kasema tuje nae anaweza kazi"
RASTA: ingieni ndani anzeni kazi huyu dogo niacheni nae apa.
Rasta alinipa maelekezo ya kutoa kila nilichokua nacho mfukoni huku akiniangalia kwa makini sana. Sikua na vitu vingi zaidi ya simu niliyopewa na merry, kibiriti pamoja na scientific calculator.
RASTA: dogo unasoma? Nimeona scientific calculator umenikumbusha mbali sana.
MIMI: ndio bro!! Ila nimeacha.
RASTA: kwanini umeacha??
MIMI: ni story ndefu bro!! Tunaweza kuendelea na mambo mengine kwani siwezi rudi tena huko.
RASTA: ok! Hua sipendi kufanya kazi na watu nisiowajua, ila kwakua watu wa chuga hawaja wahi kuniangusha zama ndichi ila simu nitabaki nayo Mimi.
Ndani ya kile chumba kulikua na viroba kadhaa vya bangi na shughuli kubwa ilikua na kuiandaa na kufanya packing. Kwa haraka nilitambua kama mzigo huo ulikua unasafirishwa nje ya jiji. Ila sikutaka kuhoji sana zaidi ya kufanya kazi hiyo kama nilivyoelekezwa na wenyeji wangu.
Tulimaliza kazi ile saa tatu asubuhi huku nikiwa hoi kwa usingizi wa zaidi ya siku mbili. Nilipitiwa na usingizi kwenye kigodoro kidogo cha futi tatu kilichokua kimechoka mno. niliamshwa na mtu nisie mjua mida ya saa 9 mchana, jamaa yule alinipa maelekezo nimfuate anapoenda.
Tulitumia muda mchache kufika sehemu moja inaitwa kijichi, tuliingia ndani ya bar ambayo ilikua opposite na barabara. Tulikaa meza ambayo tayari ilikua na watu wawili ila niliweza kumtambua rasta peke ake.
RASTA: dogo inaonekana umechoka sana pole.
MIMI: Asante bro.
Alinipa simu yangu na shilingi elfu kumi kama malipo ya kazi ya jana usiku kisha akaniambia tunakazi nyingine usiku huo. Hivyo kama nitahitaji kupumzika baada ya kula nipumzike tu kwani usiku huo tutakua na safari. Baada ya kuingalia simu upande ule wa call log nilikuta missed calls nyingi za namba mpya niliamini hizo zote zilikua ni juhudi za merry akitaka kujua nipo wapi.
Zilishushwa buckets za Heineken pamoja na kilo kadhaa za mdudu (pork) kiukweli niliya furahia sana yale maisha huku nikijaribu kuwaza ni kwa namna gani naweza tengeneza pesa mingi ka hizo.
Nilishtushwa na mlio wa simu na baada ya kupokea alikua na merry.
MERRY: massawe upo wapi mpenzi wangu?
"Samahan kaka Ras apa ni wapi" nilianza kuulizia jina la mahali nilipo kabla ya kujibu.
MIMI: nipo kijichi Merry.
Kwa maelezo ya merry alidai yupo temeke na jioni ataenda kuanza kazi sehemu moja ipo kurasini inaitwa PUB ONE hivyo kama nitahitaji kuonana naye niende hapo. Nililudi tena sabasaba kuendelea na usingizi wangu na ilipofika mida ya saa 3 usiku niliamshwa na Ras. Tulipakia mzigo na safari ilianzia, kwakua nilikua mgeni sikujua kabisa tunaelekea wapi na hata hivyo sikutaka kuuliza kila kitu niliamua kua mpole.
Baada ya masaa kama matatu hivi tulikua pembezoni mwa fukwe eneo ambalo baadae nilikuja kulijua kwa jina la mbweni.( Niliona mengi maeneo yale lakini kubwa zaidi ilikua ni bandari bubu inayoingiza na kutoa mizigo bara na visiwani).
Baada ya kumaliza kilichotupeleka eneo lile tulianza safari ya kuludi, na safari hii tulikua wawili tu na hatukua na mzigo wowote ata hivyo Ras alionekana kua mchangamfu kwani alianza kunipigisha stories pia.
Wakati tunapiga stories niligundua Ras amependa kunitumia kwenye safari yake kwa sababu kuu kama mbili hivi.
Kwanza; nilikua Smart kimuonekano ukilinganisha na washirika wake wengine ambao ungewaona tu ungejua ni wala ganja walio kubuu.
Pili; confidence na umakini kwenye kuongea, kwani sikua naonyesha dalili ya kumuogopa kwenye maongezi yetu.
Tukiwa njiani tunaludi simu iliita mfululizo na nilipoishika ilikua ni namba aliyoitumia merry kunipigia mchana.
MERRY: massawe upo wapi?
MIMI: nipo njiani naelekea mbagala
MERRY: naomba upitie nilipo kwambia nipo.
Kwakua nilishamueleza Ras black & white mpaka siku ile ameniona, ilikua rahisi kumwambia tupitie PUB ONE usiku huo kwani sikujua merry amepatwa na changamoto gani. Tulifika maeneo ya chuo cha T.I.A ambapo kulikua na bar kama mbili hivi japo sikumbuki vizuri lakin zilikua zimechangamka sana. Nilipiga ile namba na ikapokelewa na merry ambae alikuja upande wa pili wa barabara baada ya maelekezo yangu.
Merry alikuja akiwa analia huku akiniomba nisimuache eneo hilo peke ake, nilimuangalia Ras ambae nae alijua kabisa kama nahitaji msaada wake na Aliishia kusema tuingie kwenye gari. Sikumuuliza chochote merry zaidi ya kumuomba aache kulia kwani bado tunasafari ndefu.
Wakati huu sasa Ras aliamua kutupeleka mpaka nyumbani kwake maeneo ya kijichi. Tulipofika alinionyesha chumba cha kupumzika lakini akimtaka merry apumzike kisha mimi na yeye tutakua na maongezi mafupi.
Lilikua ni jumba kubwa lililopo ndani ya fensi lakini pia kilichonishangaza ni ukimya wa jumba hilo kwani hukukua na mtu yoyote tuliyemkuta ndani apo.
RASTA: dogo nimeamua kuwapa msaada wa siku moja kwa sababu yule binti umri wake na kile alichokua anakifanya pale haviendani. Msaada wangu wa mwisho, kesho tunaenda Moro kuchukua mzigo yeye tutamuacha msamvu asubuhi apande gari za mwanza aludi shule. Wewe kwakua umechagua upande huu tutaendelea kua pamoja. Nenda kupumzike.!!!
Kwa maelezo ya Ras inaonekana hakutaka dialogue ni kama alikua ana nipa taarifa.
Nilipoingia ndani merry alikua amelala usingizi mzito na sikuona haja ya kumuasha na mimi pia niliamua kupumzika.
Majira ya saa 9 kasoro usiku ndio tulianza safari na gari nyingine aina ya Rav 4. Mda ote huo sikua nimepata nafasi ya kuongea na Merry kuhusu jambo lolote kwani tuliamshwa usingizini na kujiandaa na safari kwa muda mchache.
Tulitumia almost 2:50 hours kuzimaliza 195.97 km kwani speed ya gari ilikua ikipungua sana basi ni 70km/hr.
Saa 12 asubuhi tunaingia moro huku Merry akipewa laki moja ambayo tuliamini itamfikisha bila changamoto za aina yoyote.
Niliagana na merry katika namna ambayo iliniumiza sana kwani hatukupata nafasi ya kuongea jambo lolote. Na kwa mara ya kwanza machozi yalinitoka baada ya kuona Merry akiwa akinipungia mkono maeneo ya stand ya msamvu. Alipanda gari ya kampuni ya Ally's Na huo ndio ulikua mwisho wa kuonana na Merry kwenye maisha yangu.
Nikiwa ndani ya hostels za wanafunzi wa SUA ambapo niliachwa na Ras huku yeye akitokomea porini. Majira ya saa 3 asubuhi ilitufikia taarifa ya ajali mbaya iliyohusisha magari matatu eneo la mkundi kwa makunganya. magari hayo ni ya kampuni ya sumry, shabiby na Ally's.
Kwa wenye kumbukumbu mnaweza kuikumbuka ajali hii na hapo ndipo nilipompoteza Merry ( alifia hospital akipelekwa kama majeruhi).