TUNAENDELEA WAKUU.
Story na wale jamaa zilinifanya nizidi kuwa huru zaidi ya ilivyokua hapo kabla, na mpaka wakati huo nilijua kuwa Rehman ndio aliyeniwekea ile memo siku ile nikiwa msikitini.
Na wenyewe pia walikubali kuwa Tala ni fatemeh, na jina hilo alipewa wakati akiwa bado mdogo sana na mlezi wake wa hapo mwanzo ambaye aliitwa Zahra.
Kiukweli niliyajua mengi sana kwa siku hiyo na ni moja kati ya siku niliyowahi kuvuta sigara kubwa ambayo mpaka leo sijawahi kuipata tena.
Kwa mujibu wa mohamed ni kwamba ganja ile waliyokuwa wanatumia ilitokea au ilikua inazalishwa huko kaskazini mwa India. Na kwa jina maarufu iliitwa Idukki gold, ni moto wa kuotea mbali na kama una kichwa ya kuku hii kitu pita nayo mbali sana bwashee hahah hahaha.
Nimetumia neno hilo kichwa ya kuku kwasababu wote tunajua kichwa cha kuku hakiwezi kuvishwa kilemba eenhe.
Sifa moja ya Idukki gold ambayo inalimwa huko Kerala ni kwamba hii bwana ni miongoni mwa zile ganja ambazo ukivuta tarajia njaa moja ya hatari sana.
Na kumbe washkaji zangu wale wa kina Rehman na Mohamed ambao nilikua navuta nao wenyewe wanalijua hilo hivyo kabla ya kuivuta hujiandaa kabisa au huandaa kabisa mazingira ya misosi.
Hivyo basi kabla sijaanza kulalamika kuhusu kuhitaji msosi jamaa walinichukua mpaka kwenye apartments ambazo walikua wakiishi wao na zilikua kwenye floor moja juu chini ya apartment ile ya fatemeh.
Kwenye floor ile jamaa walikua wakikaa rooms tofauti tofauti lakini wote watatu walionekana kuwa wanashare mambo mengi sana hususani upande wa misosi.
Niligundua hilo kwani wote watatu walikua wakitumia jiko moja, napo sema wote watatu usipagawe sana kwani mpaka sahivi nimemtaja Mohamed na Rehman pekee.
Tukumbuke hawa ndio madereva wanaokuwa wakipeana shift kumzungusha fatemeh kwenye mizunguko yake. Na sababu ya wao kuwa madereva ni kwamba walitaka wajue ratiba na kila sehemu anayokwenda fatemeh.
Basi kwa mantiki hiyo, ina maana fatemeh siku hiyo alitoka na mtu mwingine mbali na Rehman na Mohamed ambao ata mimi niliwahi kukutana nao hapo kabla ila sikujua kama ni sehemu ya walinzi wa fatemeh.
Aliyetoka na fatemeh siku hiyo kama dereva alikua ni jamaa mmoja kibonge sana niliwahi kukutana nae ile siku niliyokua namtafuta Mohamed kwenye basement.
Na huyo jamaa ndiye alinielekeza sehemu ambayo naweza kuonana na mohamed ambayo ilikua ni floor ya mwisho juu kabisa nilipokaa nao siku hiyo.
Je! Hili jengo linashughuli gani nyingine? Au ni makazi pekee ya watu hawa. Kwani toka nimefika hapo sijawahi kuonana na watu wengine mbali na hao wachache na kuna siku nyingine niliwahi kukutana kwenye lifti na mashekhe au watu waliovalia kanzu.
Sasa sijui kama watu hao ndio wale wale wakina Rehman ila tu nilishindwa kuwatambua sababu ya ugeni wa mazingira hayo.
Kwa mujibu wa bwana Mohamed ni kwamba sehemu kubwa ya jengo lile lilitumika kama makazi ya vijana wa MOIS wanaofanya kazi nje na Ndani ya nchi. Hivyo basi wengi miongoni mwa majasusi walio nje kwenye misheni mbalimbali wanaporudi nchini kwao hufikia kwenye jengo hilo.
Lakini pia mbali na hapo jengo hilo hilo pia kuna floors zipo zikitumika kwa ajili ya vikao na mikutano ya siri ya idara yao.
Apa alidai kuna vikao vinaendelea Ndani ya idara ambavyo kiuhalisia hata serikali yenyewe kuna mambo haipaswi kuyajua kuhusu idara hiyo.
Changamoto kubwa ya idara yao ni hofu ya uwepo wa mapandikizi ya Mossad aidha Ndani ya serikali au ndani ya idara, hivyo basi kwa kuhofia hilo kuna vikao na mipango hufanywa na watu wachache sana Ndani ya idara kwa kuhofia kuvuja kwa taarifa zao kwa upande wa pili.
Kitu kikubwa nilichokipenda kuhusu hawa jamaa ni kwamba kwao pesa sio issue kabisa kwenye maisha na operation zao.
Yaani ukiwa agent hususani wale walioitwa field agent kwako pesa inakua sio issue kabisa yaani kila sehemu umezungukwa na pesa. Lakini nilichogundua ni kwamba hawa jamaa licha ya kuzungukwa na pesa nyingi hawana muda wa matumizi kabisa.
Lakini pia niligundua sababu ya kuwafanya au kuwapa jamaa access ya mpunga mwingi kiasi kile ilikua ni kuwaweka kisaikolojia wa amini pesa kwao sio tatizo la kuwafanya mpaka wao kutoa taarifa za siri kwa adui.
Nadhani hii kitu ata bongo itakua inatumika tu, kwani ukiwa agent wa haya Mashirika ya kijasusi alafu kwenye maisha yako unaandamwa na madeni kuanzia bank, vicoba, madukani mpaka bar unafikiria ukipata upenyo wa kuiba au kuuza taarifa utashindwa kweli kufanya hivyo. Huwezi kushindwa kufanya hivyo ata kama utakua ni mzalendo wa viwango vya juu kiasi gani.
Na sababu kubwa ya kushindwa kufanya hivyo ni moja tu,
The highest goal of life is happiness,
hivyo basi watu wanaitafuta furaha kwa namna yoyote ile. Huwezi kukosa amani kwa madeni wakati unajua kuna kitu ninacho na kinaweza kunisaidia kulipa madeni hayo.
Kwa mantiki hiyo basi hawa ma agents hupewa kila kitu cha msingi anachokihitaji binadamu ili ajione yupo kwenye ulimwengu ule mkamilifu.
Yaan apa namaanisha agent ataishi sehemu nzuri, atakula anachotaka na usafiri wa kwenda popote bila kuhofia vitu vidogo vidogo kama wese na entry permit za maeneo sensitive.
Kiufupi jamaa wanatengenezewaga mazingira ya kuifurahia nchi yao ( enjoying the land to the fullest ) na hii huwapelekea kuwa wazalendo kiasi kwamba ile spirit ya kuilinda nchi na viongozi wake kuwa kubwa sana.
Na tukumbuke hawa jamaa kawaida wapo kwa ajili ya kulinda maslahi ya nchi, amani pamoja na mfumo ila sio maslahi ya mtu au kiongozi kama ilivyo kwa Baadhi ya mataifa ya Africa.
Kwa mataifa mengi ya kiafrika unakuta Rais anapewa title au anaitwa sponsor wa idara ya inteligensia ya nchi husika.
Kwa mujibu wa hawa jamaa hili ni kosa, Kwani kwa kufanya hivyo ni wazi kunauwezekano wa kutengeneza mianya ya idara hizo kuanza kupambania maslahi ya sponsor baada ya kusimama kwenye lengo kuu ambalo ni usalama na maslahi ya nchi.
Yote haya niliyapata nikiwa na Mohamed pamoja na Rehman wakati wa kuandaa msosi mezani, lakini pia niligundua hawa jamaa wa Asia wanatudharau sana waafrika kuliko ata wazungu.
Yaani jamaa kila nilichokua najaribu kukitetea kwamba sisi tumejitahidi jamaa walikua wananipinga.
Japo kuna muda jamaa walikua wananipinga kwa facts ila nilikua najaribu tu kubisha sikutaka kuendelea kukubali kila walichokua wananiambia.
Kwa jinsi nilivyo enjoy siku hiyo kwa kupiga stories lakini pia kwa kuvuta kitu cha Idukki ambacho laiti kama yule muheshimiwa aliyekisifia cha Arusha hivi juzijuzi angeonja hii kitu ya Idukki basi nadhani angetengua kauli.
Tunatakiwa kujua kuwa kuishi kwingi ni kuona mengi, lakini tuwaaminishe watu kuwa kutembea kwingi ni kujua na kuona mengi zaidi.
Apa namaanisha unaweza kuwa mzee wa miaka 90 au ata 100 lakini kama maisha yako yote umeyatumia au umezeekea kwenu huko mbekenyela.
Huwezi kujua mengi kujilinganisha na kijana wa miaka 30 aliyewahi kuishi au aliyetembea kwenye nchi kubwa zaidi ya 7 duniani.
Lakini pia kama nusu ya ujana wako uliutumia kwenye kilimo na mifugo, basi huwezi kujilinganisha na mtu ambaye nusu ya ujana wake aliutumia kwenye shughuli kama za usafirishaji, biashara na nyingine za kufanana na hizi.
Watu hawa mara nyingi wakaua wame interact na watu wengi na wanakua wanajua mengi zaidi kuliko mtu aliyekaa sehemu moja.
Hivyo naomba nisisitize tu tutembee sana angali tukiwa bado vijana na tuna nguvu, kwa kutembea tutajua mengi na tutajifunza mengi tukiwa bado kwenye umri mdogo.
Mtu anaetembea sana hana tofauti na risk taker na tukumbuke kuwa mara nyingi risk takers ndio wanatoboa japo wakiangukia pua wanafulia vibaya sana hahahaha hahahah.
Risking ni sawa na sacrifice, sasa basi unapo sacrifice kikubwa ni wazi utatarajia kikubwa na unapo sacrifice kidogo basi ni wazi utatarajia kidogo zaidi.
Sacrifice kubwa Duniani inaaminika kuwa ni damu lakini sio kweli tunasahau kuwa kuna kitu kinaitwa MUDA. Uki sacrifice muda kwenye maisha yako basi ume sacrifice kitu kikubwa zaidi na hili nitakuja kulielezea vizuri wakati ujao.
Sacrifice ya Damu inagusa physical world kwa uchache sana na spiritual world kwa uchache pia. lakini wakati huohuo muda unagusa kuanzia physical mpaka spiritual world kwa sehemu kubwa zaidi ( ulimwengu wa kiroho ).
Siri zote kuu za ulimwengu wa kiroho na kimwili pamoja na maisha kwa ujumla zipo ndani ya muda na ndio maana siku muda ukisimama basi kila kitu kitasimama.
Niliwahi kusema hapo nyuma kuwa kuna maeneo huko baharini na angani yana sifa za kutokufungamana sheria za ki fizikia.
Moja ya sifa hizo nilisema ni kusimama kwa muda Ndani ya eneo hilo, apa nilimaanisha kama umeingia hapo ukiwa miaka kumi (10) basi ata ikipita miaka elfu moja 1000, utaendelea kuwa na miaka kumi hiyohiyo.
Hahahahaha hahahaha apa kama hujashiba yaani una njaa au unatumia akili kwenye kuvukia barabara tu huwezi kunielewa ata kidogo.
Anyway! Point kubwa nilitaka kuelezea logic ya kusimama kwa muda na nini kitatokea endapo muda utasimama lakini pia kwanini sacrifice kubwa tunaamini ni muda kuliko damu.
Naona kabisa naelekea kutoka nje ya simulizi lakini mtanisamehe kuna muda kichwa kina vitu vingi ambavyo natamani nivitoe tu.
Turudi kwenye simulizi yetu sasa,
Mazingira yale ambayo walikua wanaishi wale jamaa lakini pia nikiangalia na mazingira yale aliyokua anaishi fatemeh ni wazi jamaa walikua wanakila kitu lakini pia pesa haikua tatizo kabisa.
Tulipiga misosi ya kutosha, tena tulikula kweli sio masiala ogopa sana msosi unaopikwa wakati wa njaa tena mbaya zaidi njaa iliyosababishwa na majani ya Kerala.
Msosi mzito uliwekwa mezani huku kila mtu akiuparamia kwa style yake, mimi nilianza kwa push-up mbili tatu japo walinicheka sana kwamba pushups zangu za kitoto simfikii fatemeh ata kidogo.
Rehman ye alivua nguo zote na kubakia na boxa tu ndipo akaja mezani, kiuhalisia kilichokua kina endelea pale sio chochote bali ilikua ni trick ya wale jamaa kunifanya niwe huru zaidi kua nao lakini pia kunifanya mshkaji wao.
Walikua wanaandaa mazingira ya mimi kuwaamini na kuwazoea zaidi lakini pia na kuwa huru zaidi ninapokua nao.
Kwakua nilitarajia kufuatana nao kuja nao bongo basi niliamini hiyo ilikua ni miongoni mwa mipango yao ili tu tunapofika huku wao wasiwe wageni kwangu na mimi nisiwe mgeni kwao.
Tukiwa tunaendelea na stories na msosi pia jamaa waliahidi kwamba kuna siku kabla ya kuondoka Tehran watanipeleka eneo moja hivi nikafurahie watoto wa Tehran.
Na walisema hayo Kwani waliamini mpaka muda huo sijagusa mbususu kwa miezi kadhaa,
kuna muda Rehman alisema yeye ndiye alikuja bongo mara ya mwisho baada ya kupewa taarifa zangu ambazo waliziomba kutoka kwa agent wao aliyepo East Africa.
Kwanini Rehman alisema hayo! Apa alidai kuwa kwa nchi ya Iran swala la wasichana kuuza miili yao halipo kabisa. Ila tu wapo wasichana wachache kutoka mataifa jilani ambao wanaingia huko kimagendo kwa ajili ya biashara hiyo.
Lakini alidai alishangaa sana alipofika Africa mashariki baada ya kukutana na wadada wanaojiuza kwa bei rahisi kiasi kile. Tena kwa maelezo ya Rehman Alidai nchi jirani ya Kenya ndio balaa kuna biashara hiyo kwenye sehemu nyingi huku Nairobi ikiwa ndio kidedea.
Nchi nyingi za Asia huku Dubai ikiwa ndio kinara, kuna wadada wengi wa ukanda huu wa Africa mashariki hususani kenya wanaenda huko kwa ajili ya kuuza miili.
Story zilikua nyingi lakini nilitoka pale na jambo moja tu kwamba nilihitaji wanitimizie ahadi yao ya kunipeleka kule walipodai tutaenda kabla ya kuanza safari ya kuelekea bongo.
Niliondoka na kuelekea kwenye apartment yetu mimi na fatemeh kwa ajili ya kuendelea na ratiba yangu ile ya kuangalia muvi.
Lakini haikua hivyo kwani nilipofika tu na kutulia kwenye sofa nilipitiwa na usingizi mzito na wa ajabu ambao bila shaka ulisababishwa na Idukki gold pamoja na ile shibe.
Nilikuja kuamshwa na shughuli za fatemeh ambazo alikua akizifanya, ulikua ni usiku umeshaingia na sikumbuki nilala saa ngapi ila nilishangaa kuona usiku tayari umeshaingia.
Fatemeh alichofanya ni kunipa pole ya usingizi mzito alionikuta nao pale, alidai toka amefika pale yalipita takribani masaa matano na hajui mimi nilianza kulala mda gani.
Ata hivyo mi mwenyewe sijawahi kulala usingizi wa namna hiyo toka kuzaliwa kwangu hivyo nilihisi inawezekana kuwa ni ile weed niliyopewa na Mohamed na mwenzie.
Na kama sio weed basi kuna kitu wamenifanyia kwa makusudi kabisa kama walikua na mpango wa kuingia ndani ya apartment yetu kwa ajili ya upekuzi.
Fatemeh alijua usingizi ule haukua wa kawaida hivyo basi baada tu ya kuamka na kuniona nimeanza kukaa vizuri swali la kwanza lilikua ni, nilienda wapi na nilikutana na nani na walinipa kitu gani kwani alidai usingizi huo haukuwa wa kawaida.
Sikumficha Chochote fatemeh, nilimwambia kilakitu kwamba alipotoka yeye tu haukupita mda mrefu Rehman na yeye alifika hapo na kutaka kuongea na mimi.
Lakini nilimueleza kuwa hatukuingia Ndani zaidi ya kwenda floor ya mwisho juu kabisa ambako uko tuliungana pia na Mohamed. Na nilimwambia pia kuwa Rehman na Mohamed wanaonekana kuwa ni watu wa moja.
Baada ya kumpa majibu hayo nilirudisha swali kwa fatemeh mwenyewe, nilimuuliza amefikia wapi kuhusu kile alichokua anakitafuta kwenye details au taarifa zilizomuhusu Rehman.
Majibu ya fatemeh yalikua kama yangu tu, alidai Rehman hakua gerezani kule fashafuyeh lakini ni kweli alikua askari wa kikosi cha wanamaji ambae baadae alihamishiwa kwenye idara hiyo.
Mbali na hapo alikiri pia kuwa uwepo wa watu hao ni sehemu ya ulinzi ambao ulipangwa na wakuu wao ambao waliamini kumuacha fatemeh huru kuna hatari kubwa ya kumpoteza.
Yaani bila ulinzi wa aina yeyote inaweza kuleta madhara na wakamkosa kama ilivyokuwa kwa baadhi ya wataalamu wao waliouawa hapo kabla.
Fatemeh aliongezea kusema yeye alikua akiamini hana maadui mpaka kufikia umri huo lakini sio kweli, ni kwamba ana maadui wa karibia aina tatu wanaomtafuta kwa namna yeyote ile ili wampate.
Adui wa kwanza ni haya Mashirika ya kijasusi ambayo yamekwisha tengeneza audui dhidi ya Iran. Bila shaka watakua ni Mossad na CIA ambao wanamtafuta fatemeh lakini sio kwamba wanamjua la hasha.
Mossad na CIA kwa mara kadhaa misheni zao zimekua zikifaulu kwa upande wa technology au TEHAMA dhidi ya Iran.
Lakini kuanzia mwaka 2012 kumekuwepo mtu ambae ameonekana bora zaidi kwenye kulinda mifumo ya kikompyuta na kinyuklia mpaka kuweza kugundua uwepo wa virus kwenye mifumo hiyo.
Mbali na hapo mtu huyo ameonekana kuboresha ulinzi zaidi kwenye mifumo yao na ni mifumo hiyo sasa imeonekana kuwa imara zaidi ya ilivyokua awali.
Sasa basi CIA na Mossad wanachopambana kujua ni nani huyo aliyeingia kwenye kitengo hicho na kuimarisha sekta hiyo.
Lakini sio tu kumjua pia ana ujuzi gani na aliutolea wapi mpaka kufikia hatua ya kuwaumiza kichwa watu ambao wanaamini wao ndio wana akili duniani.
Hivyo basi ili tu wasiweze kumpoteza fatemeh kama ilivyokua kwa maprofesa kadhaa wa hapo nyuma wamelazimika kumuwekea fatemeh ulinzi wa namna hiyo.
Lakini watu wengine ambao ni maadui wakubwa wanaomtafuta fatemeh ni wale wanaoaminika kuwa ndio ndugu wa mwanamama aliyejulikana kama zahra. Sasa ndugu wa zahra wanatafuta vitu vikubwa viwili, cha kwanza wanataka kujua kama fatemeh yupo hai au amekufa na kama amekufa basi ndicho wanachotaka ila kama yupo hai basi kwa gharama yeyote anatakiwa kufa.