Utajiri wa Magofu ya Rapta

Utajiri wa Magofu ya Rapta

THE WEALTH OF RAPTA RUINS
(Get Rich or Die Tryin)

Msimuliaji: LUDOVIC MASSAWE

NB: SIMULIZI HII IMEAMBATANISHWA NA BAADHI YA PICHA ZINAZOTUMIKA KUELEZEA MATUKIO, HURUSIWI KUTUMIA PICHA HIZO MAHALI POPOTE.

PROLOGUE/DIBAJI

Mji wa rapta ni mji uliozama baharini kisiwani mafia kwa zaidi ya miaka 2000. Unaweza kua mji mgeni Kwa baadhi ya watu, lakini wengi mnaweza kua mmepata kuusikia uwepo wa mji huu wa kale pembezoni mwa pwani ya Africa mashariki. Wapo wanaodai mji huu unapatikana maeneo ya rufiji kwa sasa na wapo wanaodai mji huu unapatikana pembezoni mwa kisiwa cha mafia. Je! ni nani yupo sahihi?

Mji huu ulipata kuwepo mwanzoni mwa karne ya 1 na imepita zaidi ya miaka 1600 mpaka 2000 tangu kuwepo kwa mji huu. Unaaminika kuwa mji wa kwanza tajiri barani Africa na pia ni miongoni mwa miji kumi na tano inayopatikana chini ya maji. ukiacha miji kama vile Thonis-Heracleion na Alexandria iliyopo Egypt, Yonaguni Jima (Japan), Port Royal (Jamaica) Dwarka (India), Pavlopetri iliyopo south-western Greece, Villa Epecuen (Argentina) nk.

Tofauti na ilivyo kwa watanzania na wakazi wa Africa mashariki wakiwemo wana archeologia. Wengi wamechelewa kuzipata habari za mji huu, mimi nilizipata habari hizi nje kabisa ya ukanda huu. Nilizipata habari hizi nikiwa jiji la Tehran uko inchini Iran (uajemi ya kale) ndani ya maktaba ya taifa (National Library of the Islamic Republic of Iran) iliyoanzishwa mwaka 1937 ikiwa na zaidi ya items milion 15 ndani yake.

Wakati nafika Iran nilikua nikitokea nchini Colombia na Peru kwenye mashamba ya koka (coca plantations). kwa wasiojua koka leaf ndio mmea unaotumika kutengeneza madawa ya kulevya aina ya Cocaine kupitia mchakato mrefu. Na ugumu wa ku control uzalishaji wa cocaine unasababishwa au unatokana na kushindwa kuthibiti chemicals zinazotumitumika kwenye mchakato huo kwani ni chemicals za kawaida zinazotumiwa kila siku kwenye matumizi ya binadamu.

Mfano; ku process coca leaf kuwa coca paste mpaka kupata cocaine base na HCI zinatumika chemicals kama, Sulfuric Acid, Sodium Bicarbonate, Sodium Hydroxide, benzene, Potassium Permanganate, Dichromate, Ammonia Hydroxide, Sodium Hydroxide, Methyl Ethyl Ketone na kerosene. Tutajuzana mengi kuhusu cocaine hapo mbele tukiendelea na simulizi.

Sasa basi Niliwezaje kufika Colombia, Peru kisha Iran na miji mingine mikubwa duniani? Niliwezaje kuzisikia habari za mji wa rapta? nani alinipa habari hizi? na mji huu wa rapta una utajiri kiasi gan ndani yake? Nilifikaje rapta na kwa msaada wa technologia gan nilifanikisha zoezi langu? Kipi kilisababisha mji huu kuzama baharini?

Swali lingine la msingi, wageni wa kwanza wa pwani ya Africa mashariki walikua ni warumi na wachina kabla ya waarabu na waajemi, sasa imekuaje details za rapta zilizoandaliwa na warumi zikafika Iran (Persian gulf) zilifikaje huko?

Najua baada ya kutaja wachina wengi mtajiuliza maswali lakini msijali tutaona ushahidi wa uwepo wa wachina ndani ya mji wa rapta. 90% ya wachunguzi wa mji huu wanatumia taarifa za warumi zilizoandaliwa na Claudius Ptolemaeus (Claudio Ptolemy). Je wana fahamu kua details hizo kabla ya kuwafikia zilishatumiwa na waajemi wa kale Na kuna uwezekano taarifa hizo zilichakachuliwa!?

Je! Mzungu bwana Alan Sutton (mzamiaji) aliyegundua kuta za rapta akiwa kwenye helicopter hivi karibuni, ilikua ni bahati mbaya tu au na yeye ni moja ya wale treasure hunters ila hajaliweka hili wazi?
Ungana nami kwenye simulizi hii ya kuvutia ili kupata majibu ya maswali yote na kwa hakika utajifunza mambo mengi ndani yake.

SEHEMU YA 01

Mgomo sengerema secondary

Wakati unajiuliza Niliwezaje kufika Colombia, Peru na kisha Iran unatakiwa kujua safari yangu ya jasho na damu pamoja na misukosuko mingi ilianzia shule ya sekondari ya sengerema nikiwa kidato cha sita. Kwa waliopata kupita shule hii wanaweza kua mashihidi kwa namna shule hii ilivyokua ya kikomando yaan wenyewe tulikua tunaita late-summer boot camp.

Kwa haraka haraka tu ni shule aliyowahi kufundisha hayati magufuli kabla hajawa waziri na kisha raisi. Nadhani umeanza kupata picha ilikua shule ya aina gani, Ni shule ambayo kila mtu alikua jeuri kuanzia headmaster mpaka mpishi wa jikoni. Wakati nikiwa hapo tuliwahi kushuhudia kesi nyingi ngumu na za ajabu kama wanafunzi kukutwa na kombati za jeshi full set. Kuna mengi kuhusu sengerema ambayo hatuyajui nitawaeleza machache tu na ni kwa namna gani safari yangu ilianzia hapo.

Nilifika hapo kwa mbinde huku o'level nikitokea Ngerengere kizuka sekondari baada ya kufukuzwa MAKOKO SEMINARY, kiukweli nilikua mtoto mtukutu na jeuri ilifika hatua mzee wangu mzee MASSAWE alisema hizi tabia nimeridhi kutoka kwa babu yangu. Ambae alikimbia nchi baada ya kuhusika kwenye matukio mawili, lile la utekaji wa ndege ya ATC mwaka 1982 February kwa makusudi ya kushinikiza mwalimu ajiuzulu na lile jaribio la kuangusha serikali ya mwalimu Nyerere la mwaka 1980's. Babu Yangu alikua ni miongoni mwa wale maafisa wakuu waliosuka ule mpango, Tuachane na babu na tuludi zetu sengerema.

Tukio la mgomo ndio lililoanzisha safari yangu Na lilipangwa usiku baada ya mlo wa jioni, vidume baada ya kushiba dona maharage pamoja na nchima boyo akili zikatutuma tufanye mgomo usiku wa siku hiyo. Sababu za mgomo zilikuwepo japokua hazikua na mashiko sana naweza sema ni ujana tu ndio ulikua unatusumbua ukiongeza na zile bangi zakuvutia maporini (chaka).
Kama kawaida mzee baba siku hiyo ya mgomo niliwekwa kitengo cha TANESCO, yani niliambiwa ikifika saa 2 kamili usiku ni hakikishe shule nzima umeme umezima. Hii ilitokana na ujuzi wangu wa mambo ya electronics na wiring za ujanja ujanja za mabwenini especially bweni la kimweri na sokoine.

Basi ilipotimu saa 2 kamili nilihakikisha Giza limetanda shule nzima kasoro nyumba za walimu tu, na kazi yangu iliishia hapo na Majukumu mengine yaliyobaki yalikua kwa wenzangu wahamisishaji kuhakikisha kila mmoja anashiriki. Lakini pia kuna jamaa mmoja wa mwananyamala yeye alikua na dumu la petrol lita 5 sijui alilitolea wapi usiku ule huyu bwana kazi yake ilikua kuhakikisha moto unawaka maeneo yote yaliyopangwa kuchomwa.

Mpaka kufika saa nne usiku stationary ya mwalimu wetu siwezi kumtaja jina ilikua haitamaniki na baadhi ya walimu walikimbiza familia zao mjini. 90% ya wanafunzi tulikua michepuo ya sayansi yani PCM, PCB na combination nyingine hivyo tulikubaliana kutokugusa maabara wala library wala darasa, wachache sana walikua arts na cha ajabu kwenye hii shule watu wa arts walikua wamestaarabika ukilinganisha na sayansi.

Shule imejengwa mlimani kabisa kiasi kwamba ilipofika saa 4 na nusu usiku defender ilionekana ikipandisha na wote tukapotelea maporini. Jambo la kufurahisha ni kwamba askari hawakufanikiwa kukamata ata mwanafunzi mmoja kati ya wanafunzi 800. Wengi waliishia kulala kwenye miembe na majaruba ya mpunga kwa usiku huo kwani shule ilizungukwa na makachero wakutosha. Lakini massawe nikasema siwezi lala juu ya mti Kama tumbili, usiku ule ule nikaanza safari ya kuelekea mjini mitaa ya soko mjinga.

Pale mjini kuna binti alikua anasoma shule ya jilani inaitwa NTUNDURU alikua amepanga ghetto. Can you imagine!!! Shule ya boarding na bado amepanga mtaani! asee!!... Merry alikua ni hatari sana mnyaturu yule wa singida.

Mishale ya saa tano usiku nilikua mlangoni kwa merry nabisha hodi, baada ya dikaka 3 alifungua mlango nikaingia. Walikua wawili yeye na mwenzie anaitwa jane. Ndani kulikua na chupa za safari na mzinga mkubwa wa konyagi, nilipoingia nilihisi uwepo wa mwanaume mule ndani na baadae niliona funguo za sun LG na vipisi vya sigara. Ila sikujali sana nilijitupa kitandani nikapitiwa na usingizi mzito uliotokana na uchovu wa mgomo na mbio za kuwakimbia field Force.

Nilikuja kustuka saa kumi alfajiri na mlio wa pikipiki uliokua unamrudisha merry ambae alikuja yupo hoi na kwa haraka niligundua jane amebaki na yule kidume wa jana.

Merry akilewa bia hua zinashuka chini, waliosoma cuba wamenielewa hapa. Hivyo baada ya kuingia ndani hakutaka story zaidi ya kutupa nguo kwenye kila kona ya chumba hicho kama mwehu. Na mimi kutokana na nilikua namjua vizuri haikusumbua kujua anataka nini zaidi ya kuanza mtanange wa kukata na shoka uliochukua zaidi dakika 90 kama finally ya Argentina vs France kule Qatar.

Tulikuja kuamshwa na mwanga mkali wa jua la saa 4 asubuh uliokua unapita dirishani Huku merry akiwaza supu. Ilituchukua muda mfupi kujiandaa kwenda maeneo ya stendi kupata supu, nilishangaa baada ya kufika stendi nilikutana na wanafunzi wenzangu wakiwa na mabegi wengine ma tranka. Nilipowauliza walijibu shule imefungwa kwa muda wa week 3 na tutapewa utaratibu wa jinsi ya kurud tukiwa nyumbani. Hapo nilianza kuwaza namna ya kurud nyumbani huku mizigo yangu yote imebaki shule na hakuna mwanafunzi anaeruhusiwa kwenda tena shule kwa muda huo.

Basi bwana tulipata supu na mrembo merry kisha tukarud zetu ghetto kupumzika, nakumbuka ilikua siku ya alhamisi hivyo merry hakuenda shule kutokana na hangover na tulishinda ndani siku nzima mpaka kesho yake asubuhi.

Siku ya pili akili ilivurugika zaidi baada ya kupata habari kwenye vituo vya habari viwili tofauti kuhusu mgomo wa sengerema, kituo cha kwanza ni redio sengerema ilitangaza wanafunzi kumi na tisa (19) wamefukuzwa na wengine kusimamishwa masomo kwa muda usiojulikana. Hivyo hivyo kwa redio free Africa na gazeti la mwananchi, gazeti hili lilitoa majina ya waliofukuzwa na mimi nilikua jina la kwanza kwenye ile list.

Niliwaza namwambia nini mzee massawe ambae alichoshwa na tabia zangu.

Akili ikanituma kuangalia upande wa pili wa maisha na sio kukomaa na shule, niliamini siku Moja nikiludi home na pesa nyingi mzee massawe atanikubali sana jembe lake.

Baada ya kupata wazo la kutoendelea na shule nikaanza kuwaza natakiwa nianzie wapi kutafuta pesa. Apo apo akili ikaniambia dar ndio sehemu pekee naweza tengeneza pesa nyingi, lakin kwa bahati mbaya sikua mzoefu wa mji huo na wala sikutakiwa kufikia kwa ndugu yoyote na bado sina nauli ya kufika huko. Niliamini nikifika Mwanza kwenda dar itakua rahisi hivyo nikaanza mchakato wa kufika mwanza (nyegezi).

Nilimshirikisha merry kwa makusudi ili anisaidie nauli ya kufika nyegezi kwani kutoka sengerema hadi nyegezi ni kiasi cha shilingi 4000 tu. Na kwa maelezo ya merry aliniomba tufike stendi kuna mtu atampatia tukifika hapo.tukiwa stendi Merry alimfuata jamaa mmoja bonge hivi anadeal na tickets pale stendi, Kwa haraka niligundua huyo ndio sponsor waliekua nae jana. Sikujua waliongea nini na merry ila merry aliniambia tusubiri kuna coaster inatokea katolo ndio tutaenda nayo mwanza.

Haikuchukua muda mrefu ile coaster ilifika na walipanda abiria kadhaa kisha bonge akamwambia konda hawa ndio wadogo zangu wanaoenda nyegezi. na sisi tulipanda tukaanza safari, nilishangazwa na uwepo wa Merry kwenye safari sikujua na yeye anaelekea wapi kwani hakua na sababu ya kutoka sengerema siku hiyo kwani masomo kwa upande wake yalikua yanaendelea. Merry alikua mwanafunzi wa kidato cha nne NTUNDURU sekondari na ile siku tumeshinda ote ndani nilitumia fursa kumfundisha almost topics tatu za msingi.

Sasa tukiwa ndani ya coaster kuelekea nyegezi nilimuuliza kwanini na yeye ameamua kusafiri, majibu yake yalikua ni kwamba ana muda mrefu hajafika mjini mwanza hivyo alitaka kwenda kuosha macho kwa muda kisha baadae ataludi sengerema.

Nilipata nafasi ya kupiga stories na konda ndipo niligundua wametokea geita walipeleka msiba na hapo wanarudi dar es salaam. Niliamini safari yangu kufika Dar es Salaam imerahisishwa nachotakiwa ni kuwaza namna gani naweza kushawishi jamaa ili aniruhusu nisafiri nae.

Majadiliano na konda yalikua hivi.

Konda:"dogo! we ni mwanafunzi Nini? Jana tukiwa na msiba tulibeba madogo kama watatu hivi wakiwa na suruali nyeusi na tishet za bluu kama ulivyovaa wewe"

Merry alijibu fasta kama ameulizwa yeye,

Merry: ndio sisi ni wanafunzi, ila tumerudishwa nyumbani ghafla sababu ya mgomo wa juzi usiku.
(konda hakujua kama sengerema ni shule ya wavulana pekee)

Konda: kama wanafunzi wenyewe ndio nyinyi hiyo shule kazi ipo. Kwaiyo nyumbani ni wapi??
Nilitumia swali hilo kama fursa ya kufanikisha misheni yangu.

Mimi: home dar na hatujatumiwa nauli sijui tunafikaje?

Konda: we mtoto wa kiume jitahidi upambane.

Jibu lile lilinikatisha tamaa ya kuendelea na maongezi yale.
Haikuchukua muda tulikua tumefika kivukoni busisi. Abiria wote tulishuka na kupanda kivuko, lakini nilifurahi baada ya kumuona konda anajisogeza kwa merry na kujiongeresha. nilijua kwa ujanja wa merry anaweza kufanikisha safari yangu kirahisi sana.

Baada ya kufika upande wa pili tulirudi ndani ya coaster na kuendelea na safari na wakati huu merry aliniambia ameshampanga konda hivyo tutafika wote dar es salaam.

Merry alikua binti mjanja sana na anamacho Fulani akikuangalia tu unajua atakua fundi, hahahahahaha kwa wale tuliopita sengerema miaka ile najua mtakua mnamkumbuka kwani alikua maarufu sana. Especially tukienda shuleni kwao kwa ajili ya michezo wengi walimtolea macho, nitakuja kueleza nilimpataje hapo baadae.

Baada ya kufika nyegezi tukijiandaa na safari ya kuanza kuitafuta dar es salaam nilishangaa konda aliniita na kunipa buku tano nikatafute msosi. Na kisha konda na merry walipotelea kusiko Julikana, Nilijua merry ameshafanya yake tayar niliishia kuitunza ile buku tano nikiamini itanisaidia mbele ya safari kwani sikua na chochote mfukoni.

Baada ya nusu saa merry na konda walirudi huku nikimuona merry na vifurushi vya kutosha bila shaka ilikua ni misosi na kimoyomoyo nikasema merry hajawahi kuniangusha ata siku moja. Tulikaa kwenye siti na kuendelea na safari Huku tukipiga msosi mzito nakumbuka ilikua ni Sato na chipsi kavu za kutosha.

Mimi: merry ulisema unaishia nyegezi vipi mbona unaendelea na safari???

Merry: sijawahi kufika Dar es Salaam, nadhani hii ni fursa ambayo sitakiwi kuichezea. Najua nipo na wewe hakuna kitachoharibika nitakaa week moja kisha nitarudi shule.

Daaaaah!!!!! Nilihisi mwili unakufa ganzi nilitaman kumwambia Mimi mwenyewe sina pa kufikia ila nikapiga moyo konde. tukaendelea na safari yetu huku stories zikiwa nyingi. Merry pekee ndio alikua na simu Mimi kilichokua mfukoni ni ile buku tano, kibiriti cha gesi na scientific calculator tu.

Baada ya safari ya muda mrefu wote tulipitiwa na usingizi, safari ile ni ya kutwa nzima kwani nakumbuka tuliingia morogoro usiku wa saa tano tena hiyo ilikua ni baada ya abiria kulalamikia speed ya gari ilikua kali mno. Tulipotoka moro baada ya kufika maeneo ya chalinze nilipitiwa tena na usingizi mzito. Nilikuja kushtuliwa na konda akidai alitusahau tumeshaingia mjini mda mrefu.

Konda: nyie mnashukia wapi tumeingia Dar es Salaam tayari.
Lile swali lilikua gumu kwangu kwani sikua ata najua tunapoelekea baada ya kufika dar. Kwa Dar es Salaam nachojua ni ubungo tu hivyo nilimjibu tunashuka ubungo.

Konda: ubungo tumepita tayari sisi tunaelekea mbagara, shukeni hapa mrudi vertinary mkapande gari za ubungo.

Kiukweli sikumuelewa konda ata kidogo kila alichonambia kilikua kipya ila sikutaka kuonyesha kutokujua mbele ya Merry hivyo tulishuka. Tulishushwa eneo moja lina mataa na ilikua saa saba na nusu usiku, nikiwa sijui cha kufanya Merry alianza kulalamika maumivu makali ya tumbo.
Nilijua tu itakua njaa kwani ni muda mrefu hatujapata chakula, baada ya kupepesa macho huku na kule niliona sehemu kwa mbaali kuna watu na mataa mengi yanawakawaka nikajua fika hapo patakua na bar hivyo hatuwez kosa msosi.

"Massawe hapa na kwenu kuna umbali gani?" Lilikua ni swali la Merry na mimi sikuona haja ya kuendelea kumficha ukweli, nilimueleza kila kitu kama nimeenda huko kutafuta maisha na nimeachana rasmi na masomo baada ya kufukuzwa shule na nilimueleza siwezi kurudi moshi kwa mzee massawe hatonielewa kabisa.

Kwa maumivu ya tumbo aliyokua anapitia Merry hakutaka kuendelea na mjadala nilimuona akiongoza kwenye lile eneo tuliloliona likiwa na watu wengi usiku ule.
Baada ya kufika eneo Hilo niliona maandishi makubwa yakiwakawaka yameandikwa SUGAR REY. Ni dhahiri ilikua ni bar, nilishangazwa na mavazi ya wadada wa eneo hilo na sio mimi tu ata merry pia.
"Hhhmmm kweli hii ndio dar es salaam ninayoisikia kila siku" yalikua ni maneno ya Merry. Tukiwa bado tumeduwaa alikuja bodaboda

Bodaboda: vipi mnaenda?

Mimi: hapana tumefika bro.

Bodaboda: punguzeni kushangaa basi.

Tulisogea mpaka eneo lile nikiamini hatuwezi kukosa chakula ukizingatia nilikua bado na lile buku tano la konda.

Tulipofika tu merry alimfuata Binti mmoja aliekua amekaa pembeni akiwa kwenye pozi Kama anamsubiri mtu na waliongea baadae wakafatana sikujua wameenda wapi. Nilijisogeza kwa jamaa wa bodaboda wakiwa na makoti makubwa nikajiunga kupiga nao story huku nikimsubiri Merry.

Mimi: bro samahan hawa wadada mbona wapo wengi na wana mishe gani apa mbona wamevaa kiasala asala?

Bodaboda: hao wanajiuza mjomba. We mgeni nini?

Mimi: ndio mi mgeni.

Bodaboda aliniangalia tu na hakuendelea kuongea chochote Zaidi ya kuwafata abiria wawili waliokua mbele yake.
Baada ya muda kidogo hivi nilimuona merry akiludi eneo nililokuwepo.

Mimi: merry punguza kujifanya unamjua kila mtu apa sio singida hii dar rafiki angu.

Merry: lile tumbo lilikua ni la siku zangu na sio njaa kama ulivyohisi hivyo nilienda kwa yule mdada kuona kama ata nipa msaada wowote si unajua sijatembea na chochote. Lakini pia nimemueleza changamoto niliyonayo kwamba hatuna pa kulala na ndio tumefika mjini.

Mimi: akasemaje?

Merry: kasema atanisaidia kwa leo sehemu ya kulala ila kuanzia kesho nitajua pa kwenda, lakini pia amenieleza kama sina ndugu kabisa atanionyesha kazi ya kufanya na tutakua tunachangia wote kulipa pango la nyumba hivyo mi nimeona niende nae tu.

Kiukweli sikutamani merry aondoke na yule dada lakini sikua na jinsi kwani hata hivyo sikua na sehemu yoyote ya kumpeleka. Merry alinikabidhi simu yake ili iwe rahisi kunipata siku inayofuata kwani alikua anajua sikua na simu. Tuliagana na merry na mimi nikabaki eneo hilo nikiwaza naelekea wapi kwa usiku huo wala sikutaka kujutia maamuzi yangu ata kidogo niliamini nipo sahihi kabisa.

Tunaendelea baadae usikae mbali.View attachment 2583318
Habari ya uongo ya kutunga, sema mji waweza kuwa kweli. Ulipoenda kwa Merry hapo ndiyo umeharibu, yaani uwakute wawili na mizinga ya pombe na vipisi halafu ujitupe kulala na Merry arudi eti asubuhi na pikipiki, idiot hujui kutunga story, rudi shule.
 
MANUELA: calm down Ludovic......i know a lot about you"
(Usijali Ludovic, najua mengi kuhusu wewe)

"ila kwa sasa nina majukumu mengi naomba uende tutaongea baadae. Ishi na Javier kwa tahadhari kubwa sana kwani anachuki isiyoelezeka dhidi ya watu weusi"

mpaka muda huo Manuela alikua ameniweza kwenye kila angle nilibaki na maswali mengi sana kiukweli.

Mbaya zaidi akati anaondoka aliniambia nawapa shida wazee wangu kwani siku ya jana walilazimika kusafiri kwenda ngara kwenye mazishi ya aliyekua mwanafunzi mwenzangu ambaye alifariki kwa kuzama chooni.


Sikujua ni mwanafunzi yupi ila kwa maelezo ya haraka sana Manuela alidai kuna mwanafunzi alizama chooni na kufariki kabisa. Mwanafunzi huyo alikua ni mzawa wa ngara na sababu ya wazee wangu kwenda huko ilikua ni utata wa msiba huo. Kwani wazazi wa kijana aliyemtaja kwa jina la yunus walikataa kuupokea mwili wakidai kijana wao yupo hai.

Sababu iliyopelekea mzee massawe kwenda huko ni kuona mwili huo, lakini hakuambulia chochote kwani haukua mwili wa kijana wao.

By the way Yunus nilikua namjua vizuri kama sikosei alikua ni kiongozi wa ukwata shuleni pale. Hivyo taarifa ya kifo chake ilinihuzunisha sana, kuanzia hapo niliamini Manuela anaweza kua msaada kwangu kwanza kwa kuijua lakini pia kuijua asili yangu.


Sikutaka kujua lolote kuhusu amenijuaje na amewajuaje wazee wangu pamoja na taarifa za zaida kama kufukuzwa shule na nyingine.

Mpaka wakati huo nilijua Manuela sio mtu wa kawaida kuna uwezekano akawa agent wa inteligensia kwa jinsi alivyobadilika usiku huo na ukiangalia uwepo wa wahalifu wengi maeneo hayo.

Baada ya kuyafikiria maswali yake nilihisi kuna uwezekano mkubwa akawa anatafuta taarifa zinazomuhusu Javier na washirika wake.

Tuliachana pale huku yeye akiendelea na mambo yake mengine akinisisitiza niwe makini na Javier lakini nisimuambie kuhusu kukutana nae.

Hapo sasa nilikua dilemma kati ya wawili hao yani kati ya Javier na Manuela nani yupo sahihi. Kura za uaminifu zilienda kwa Manuela Kwani aliongea mengi ya kweli kunihusu. Na kuhusu Javier sikumuamini kwa sababu ya usiri na watu aliokua anakutana nao.

Nilifika ndani mapema kabla ya ujio wa Javier hivyo bwana Javier alinikuta nimeingia ndani kama baada ya dakika 10 kupita. Nilikua bado nimekaa kitandani nikitafakari ile scenario mpya ambayo nimeanza kukutana nayo.

Javier aliingia ndani akiwa amechangamka sana tofauti na siku zote, alirudi na package moja ya chakula ambacho kilikua na taste moja matata sana package ile iliitwa Lomo Saltado kwa mujibu wa bwana Javier.

Mwanzoni nilianza kusitasita lakini mwishoni nikasema ngoja tu nile atakama nilishapewa precautions hapo kabla. Nilitamani kujua ni kwanini javier ameludi akiwa na furaha kiasi hicho.


MIMI: you look happy today!!! what the matter?
(Unafuraha sana Javier kuna nini leo)

JAVIER: I'm happy to meet the same version of hearless chimpanzee
( Bilashaka nina furaha ya kukutana toleo lile lile la wale sokwe wasio sikia la kuambiwa)

Alimalizia kwa kusema hana haja ya kuuliza nilikua wapi na nina fanya nini, kwa sababu sio sehemu ya majukumu yake. Majukumu yake yeye ni kususiwa maiti zetu mule ndani na kuzika kwa kutumia mikono yake.

Ile kauli iliniumiza na kunifikirisha kwa namna moja ama nyingine, niliwaza either amejua nilikua na Manuela na amejua tulichoongea.

Lakin pia niliwaza je ni kweli huyu bwana Javier na Manuela ni mahasim ambao wanawindana lakini yote ambayo yalikua yanakuja na kutoka kichwani kwangu sikukubaliana nayo.

Mwisho nilihitimisha kwa kusema ata iweje nitakua upande wa Manuela kwani Javier alionekana kuwa na element fulani za ukatili na unyanyasaji wa rangi. Hivyo kuanzia pale nilianza kuamini maneno ya Manuela kwamba Javier alikua ni white supremacist na alichukia weusi waziwazi.

JAVIER: so.......!!! Did you have sex
( Vipi..... Ulichakata mbususu)

MIMI: no.........! Only blowjob
( Hapana alininyonya tu)

Hahahahahahaha ahahaha hahahahahaha hahahahahahaha ahahaha nilishuhudia kicheko cha ajabu sana kutoka Javier, kicheko kilichopelekea mpaka akapaliwa na mate na kuanza kukohoa mfululizo.

Baada ya kumaliza kunicheka Javier aliongea kwa hasira na huzuni sana.

" Sijakuona ukitoka wala sikujua kama umetoka, nilichofanya ni kucheza na psychology tu kwani kwa kawaida mida hii unakua umelala au kama hujalala basi unakua umeanza kusinzia.

Lakini leo imekua tofauti sana nimekuta umekaa na macho yamechangamka hii unaonekana hujalala kabisa na ni kama ndio umefika.

Javier aliendelea kusema alishanieleza kilakitu kuhusu background ya Gatkuoth ambaye alikua ni muafrika mwenzangu nini kilimkuta na alikufaje.

Sasa ameshangaa kuona narudia makosa yaleyale, hapa alijiuliza waafrika tuna shida gani kwenye ubongo ( alitoa maneno mengi ya kejeli lakini nilikua bize na msosi)
Mpaka wakati huo nilishukuru Javier hakujua niliulizwa nini na Manuela alichojua yeye ni kwamba nilienda kula tunda tu.

MIMI: javier! You told me very little about Schulz, can you proceed from where we ended.

( Lakini bwana Javier alinisimulia kidogo sana kuhusu Schulz unaweza kuendelea ata kidogo pale tulipoishia)

Niliingiza story hiyo ila kuhakikisha tunayaacha yale mazungumzo ya awali kiukweli sikuyapenda na yalikua na kejeli sana kwetu watu weusi.

Japo kwa namna moja au nyingine alikua akiongea ukweli lakini alikosa njia sahihi ya kuwasilisha ukweli huo. Kwani sikuona mantiki ya kutumia maneno mabaya na makali kama vile kuitana sokwe na majina mengine kama hayo.

Maana alifikia hatua akasema ubongo wa watu weusi umejaa tope na kinyesi cheusi tiiiii kama ngozi yetu.

Javier alinipa condition kadhaa kama nitataka kusikia mambo kadhaa yaliyo muhusu veteran wa ki-NAZI bwana Schulz.

Condition ya kwanza ilikua ni kujibu maswali yote ambayo ataniuliza na ninatakiwa kuyajibu kwa ufasaha na pia natakiwa kuwa na uhakika wa kile ninachokisema.

Swali la kwanza lilikua je! Nakubali kama waafrika ni selfish in nature?

Swali la pili lilikua je! Nakubali kama kuna uchawi miongoni mwa waafrika na kama nakubali, vipi najua Chochote kuhusu huo uchawi
( Apa kwenye uchawi alitumia neno traditional African science)
Mpaka hapo sikuwa nimejua nia ya Javier kwani maswali yale yalikua tofauti na kile ambacho niliuliza wakati huo.

Majibu yalikua hivi; nilikubali waafrika ni selfish tena sana kwa kutumia reference zake yeye mwenyewe alizonipa siku chache hapo nyuma tulipokutana.

Majibu ya swali la pili yalikua hivi; nilikubali kuna uchawi miongoni mwa waafrika kwani hata mazingira niliyokuwepo uchawi tuliusikia sana. Lakini sina ushahidi wa moja kwa moja wa kuthibitisha kwamba uchawi upo, mwisho nilikataa kuhusu kujua Chochote kuhusu uchawi kwani sikuwahi kuushuhudia mahala popote.

Kwa majibu haya Javier alitabasamu na kisha akasema majibu yangu ya swali la pili yamejibu swali la kwanza . Nilijaribu kutumia nguvu kumuelewa lakini niwe muwazi nilishindwa kabisa kumuelewa huyu jamaa.

Kwa mujibu wa bwana Javier ni kwamba kilichomkwamisha Schulz kwenye harakati zake ilikua ni huo uchawi au traditional African science, ambayo ina upofu mkubwa linapokuja swala la methodologies na miiko yake.

Kwa maelezo ya bwana Schulz sayansi ya muafrika imepewa jina baya na image mbaya na waafrika wenyewe.

lakini kiuhalisia ndio sayansi ya kwanza ulimwenguni kwani mwanadamu especially waafrika walitumia walitumia maarifa hayo hayo katika kuyatawala mazingira na kutatua changamoto mbalimbali zilizomkabili.

Inasemekana ile traditional African science inazaidi ya miaka billion 2 ulimwenguni kwani imeizidi ata ile ya ujerumani na uingereza, apa alimaanisha wajermani walikua wakiongoza kwa uchawi kwenye hizi nchi za ulaya.

Huu uchawi au sayansi ya muafrika inaonekana kuwa ni miongoni mwa tamaduni kongwe zaidi ulimwenguni kuzidi zile za uajemi ya kale (waajemi) wayunani (ugiriki ya kale) na mesopotamia/ babiloni ya kale au wasumeri.

Mbaya zaidi taaluma hiyo hufundishwa kwa siri sana na wale wanaoijua na wakati mwingine hutumia mbinu ya kurithisha. Na kwa zaidi ya asilimia 98 imemsaidia sana binadamu especially waafrika katika kupambana na mazingira.


Kwa maelezo ya Schulz wakati anamsimulia bwana Javier ni kwamba Schulz alipata kujua kuwa waafrika waliweza kutengeneza ndege kabla ya mzungu kwa zaidi ya karne kadhaa huko nyuma kabla ya ndege hizi tunazozijua.

Hapa alitoa mfano kwamba eti kwa ukanda wetu huu kulikua kuna ndege za kuweza kubeba abiria mpaka 16 enzi hizo kabla ya hizi Boeing bwana.

Ok!.... Huu uchawi au traditional African science ilimkwamisha vipi bwana Schulz na ni kwanini Javier na yeye alitaka kujua kuhusu huu uchawi.

Bwana Schulz alishiriki vita nyingi mpaka kufikia mwaka 1943 September 9 ambapo Iran na ujerumani walipoingia kwenye mgogoro wa kivita na WA Nazi. Kabla ya mgogoro huu nchi ya Iran iliaminika kuwa neutral kabisa enzi zile za WWII ( vita ya pili).

Hiyo coloured part hapo juu kulikua na typing errors kwenye kipande cha episode 6C kilichopita ndio maana nimekirudia tena.

BWANA SCHULZ WA UJERUMANI NDIO ALIYEKUA NA MCHONGO MZIMA WA RAPTA NA ALIUPATA WAKATI WA HIYO VITA.

sasa tunamalizana na peru mda sio mrefu alafu tunaludi bongo very soon.

0623329512 Whatsapp (kwa mwenye uhitaji wa vipande vya mbele zaidi PDF)
 
Habari ya uongo ya kutunga, sema mji waweza kuwa kweli. Ulipoenda kwa Merry hapo ndiyo umeharibu, yaani uwakute wawili na mizinga ya pombe na vipisi halafu ujitupe kulala na Merry arudi eti asubuhi na pikipiki, idiot hujui kutunga story, rudi shule.
Nadhani aliweka wazi kuna vitu ataruka ili twende kwenye main scenes.....pia hapo hapo alisema walitoka na Merry akarudishwa peke yake.
 
Nadhani aliweka wazi kuna vitu ataruka ili twende kwenye main scenes.....pia hapo hapo alisema walitoka na Merry akarudishwa peke yake.
No kasema alifika akajirusha halafu mambo ya kusema Sengerema pawe na mizinga ya wine sijui pombe kali kwa enzi zile ni uongo. Pia mazingira ya mgomo ni uongo yaani kwa ufupi hii story ya kusadikika
 
No kasema alifika akajirusha halafu mambo ya kusema Sengerema pawe na mizinga ya wine sijui pombe kali kwa enzi zile ni uongo. Pia mazingira ya mgomo ni uongo yaani kwa ufupi hii story ya kusadikika
Punguza ujuaji mkuu! Pia rudia tena kusoma pale kwa marry ndo utaelewa mazingira vizuri,kila kitu kiko wazi! Na pia hata kama ni ya kutunga au la,makasiriko ya nini? Mbona kama unateseka mkuu?.
 
Kumbe africa maendeleo yameanza kitambo sana.sema hawa jamaa walitupiga chenga ya mwili kidogo tu.
Tatizo wahenga hawakuweka vitu kwenye maandishi walipokuja wakoloni kutuvuruga sayansi yetu ikapotea
 
Punguza ujuaji mkuu! Pia rudia tena kusoma pale kwa marry ndo utaelewa mazingira vizuri,kila kitu kiko wazi! Na pia hata kama ni ya kutunga au la,makasiriko ya nini? Mbona kama unateseka mkuu?.
Mkuu nilisoma between lines. Nilichoka sana pale uliposema kuwa eti umemkuta merry na bonge la mzinga wa pombe mara anarudi asubuhi. Anyway, nitarudia tena kusoma
 
Uhondo uko mbele na matukio yasiyotarajiwa,kila siku kijana anakutana na mapya[emoji28][emoji28][emoji28].

Sema ndugu yetu uko slow mno 1 kwa siku haitoshi.
 
Binafsi naona story ikiwa hapa na comments za waja inakaa poa zaidi. Ongeza tu dose, moja kwa siku ni ndogo sana.
 
Duuuh hawa watu ndio ilitakiwa story zao ziwe ktik vitabu maalumu ili kujifunza zaidi bila kujarisha in ya kufikilika au in ya kweli
 
Back
Top Bottom