Utajiri wa Magofu ya Rapta

Utajiri wa Magofu ya Rapta

Huwa nasoma mwanzo mpaka kufikia ilipo.

Huyo Manuela anakupenda ..
 
Alaf kuna akina sie ambao ugonjwa wa 50k tu inabid ukoo mzima ukae kikao ili kujadili namna ya kusaidia


Kiukwel upo sahih hiz id's zingekuwa zinaongea ingekua balaaaa
Ahhahh ukoo unakaa kujadili fifty inapatkanaje apo sim zinalia kila mahali kwa ndugu na jamaa😀😀
 
Ila we mwandishi ni unajua na unajua.
Alafu ni mhuni wa rangi zote!
Wanaobeza mstari au mtiririko wowote wananihakikishia kuwa kweli uchawi ni tabia.
Baada ya kitabu mtafute Director baba yetu wa kambo P mkatengeneze movie lakin si bongo!
 
Ila we mwandishi ni unajua na unajua.
Alafu ni mhuni wa rangi zote!
Wanaobeza mstari au mtiririko wowote wananihakikishia kuwa kweli uchawi ni tabia.
Baada ya kitabu mtafute Director baba yetu wa kambo P mkatengeneze movie lakin si bongo!
Aman sana chief, ngoja tuimalize simulizi kwanza

Sent from my ZTE T1002 using JamiiForums mobile app
 
IMG_20230623_073429.jpg

Shahzad hatunaye tena. Dah!
 
Fatemeh hakuonekana kama ni mgeni kabisa maeneo hayo kwani wakati Tunaingia ndani ya maktaba ile aliongoza moja kwa moja mpaka floor ya pili. Ni wazi alishajua tayari shahzad ni wapi aliko au atampata sehemu gani Ndani ya maktaba hiyo.

Tuliongoza mpaka kwenye chumba ambacho kilipatikana kwenye ile floor ya pili ya jengo hilo, tukiwa mlangoni kabla hata hatujaingia ndani ilisikika Salam nyuma yetu.

"Asalaam aleykum"

Alikua ni mzee wa karibia miaka sabini na mitano au hata kuendelea namaanisha angeweza kufika ata themanini. Ila pamoja na umri wote huo mzee huyo bado alikua anatembea bila hata ya fimbo na alionekana kuwa mwenye afya njema.

Alikua ni mzee wa kishiraz mwenye ndevu nyeupe pee!!! Huku mwili wake ambao haukua mnene kabisa ulionekana kuwa imara zaidi.

Fatemeh ndie alikua wa kwanza kuitikia salam ile, na alimbadilishia lugha mzee yule kwa mantiki ya kutaka na mimi nielewe mazungumzo yaliyokua yanaendelea.

FATEMEH: Waleykum salaam. I hope you are Shahzad
( Natumaini wewe ndio shahzad)

SHAHZAD: of course it's me
( Bilashaka ndio mimi)

Mzee huyu Shahzad alitukaribisha Ndani ya chumba kile ambacho kilikua ile floor ya pili na tulikaa kwenye meza zilizokua ndani ya ofisi ile.
Baada ya kuketi, mzee yule ambae alionekana kuwa mwingi wa busara alijitambulisha tena kwa mara ya pili tena alitumia kingereza kizuri tu tofauti na nilivyomdhania baada tu kumuona.

Alituita wajukuu zake na kiukweli alikua sahihi kulingana na umri wake ukilinganisha na umri wetu mimi na fatemeh. Sisi hatukustahili kuwa watoto zake zaidi ya wajukuu au hata vitukuu kabisa.

Baada ya kujitambulisha mzee huyo ali ruhusu na sisi tuanze kujitambulisha mmoja baada ya mwingine Na aliyefuatia alikua ni fatemeh.

FATEMEH: asalaam aleykum for the second time, I'm going by the name of fatemeh a native and resident of Tehran. Currently I live in Dar es salaam Tanzania working at Embassy of Islamic Republic of Iran.

( Asalaam aleykum kwa mara ya pili, mimi naitwa fatemeh ni mzawa na mkazi wa Tehran ila kwa sasa naishi Dar es salaam Tanzania na nipo nafanya kazi kwenye ofisi za ubalozi wa Iran)

Kwa kweli sijajua fatemeh alikua anawaza nini kwa kujitambulisha kwa namna ile kwani hakuwahi kufika bongo kabisa lakini kwenye maelezo yake alisema anafanya kazi kwenye ubalozi wa Iran apo dar es salaam.

Mzee huyu kikongwe alifurahi sana kusikia fatemeh alikua akiishi Dar es salaam kwa Wakati huo na yeye alimalizia kusema aliishi mji huo kabla ya miaka ya ya 1960's.

Ila alisema hakufurahia kwa namna ambavyo fatemeh amejitambulisha kwani alitumia jina moja tu hivyo asirudie tena wakati mwingine kwani alitakiwa kutaja na ubini wake pia na ndio utaratibu wa kujitambulisha.

(Baada ya fatemeh kuambiwa maneno yale ni kama alikua mpole sana hususani kwenye muonekano wake na mimi nilishajua sababu ya upole ule. Na bila shaka hii ndio miongoni mwa point zinazomuumiza sana fatemeh kwenye maisha yake.)

Mzee huyo kikongwe shahzad alidai ata tuambia kuwa aliwahi au aliishi maeneo gani kwa Wakati huo ila amefurahi kukutana na watu waliotokea Dar es salaam mji ambao aliwahi kuishi enzi za ujana wake.

Apo sasa niliona fatemeh kapatikana kwani kama ataulizwa mitaa ya bongo ni lazima atachemka tu maana kwa haraka nilijua alikaririshwa ulipo ubalozi wa Iran nchini Tanzania.

Ilifuata zamu yangu ya kujitambulisha ila niliwaza nitumie Ludovic massawe au nimwambie mimi ni mustapha. Nikaona tu nitumie jina la kwenye passport kwani Ndio linalotambulika na vibali vyote vilisomeka kama mustapha.

MIMI: asalaam aleykum, my name is mustapha abdul-qadri makungu a citizen from union republic of Tanzania. I am engaged in business in the city of Dar es Salaam and currently I live in the same city.

( Asalaam aleykum, jina langu ni mustapha abdul-qadri makungu ni mtanzania na ninaishi dar es salaam ambako najishughulisha na biashara)

Shahzad ndiye aliyetawala maongezi yetu wakati ule, na alikua makini sana kutusiiliza kuna muda aliweka miwani yake vizuri( iliyokuwa na kamba kwa nyuma) kama ananizoom hivi anione vizuri.

SHAHZAD: bilashaka kwa majina hayo utakua ni mzanzibari wewe tena mpemba.

( Nilishtuka sana kujua kama mzee anaongea kiswahili japo ni kama alianza kukisahau kwani maneno yake hayaku nyooka kama wazoefu)

Mzee aliendelea kusema amefurahi sana kukutana na mswahili hivyo aliniomba tuongee kiswahili kwani ana miaka mingi hajazungumza lugha hiyo.

Nilimwambia kuwa fatemeh alikua hajui kiswahili akasema hakuna shida tutakua tunatafsiri kwa ajili yake lakini hawezi tena kuongea kingereza kwanza hakipendi hivyo tutatumia kiswahili.

Alimgeukia fatemeh,

SHAHZAD: How long do you have since you arrived in Dar es Salaam?
( Una muda gani toka ufike dar es salaam)

FATEMEH: only two years
( Miaka miwili tu)

SHAHZAD: don't stay too long inside, make sure you visit different places like kiriakoo and meets wazaramo.

( Usikae ndani sana hutojua kiswahili kabisa, hakikisha utembea tembea mfano sokoni kiriakoo ukutane na wazaramo)

Baada ya kuitaja kariakoo japo aliitaja kwa kuikosea kimoyomoyo nikasema kazi ipo leo nimekutana na mwarabu wa kariakoo.

Alimuomba Samahani mjuukuu wake fatemeh Kwani atatumia kiswahili muda mwingi hivyo mimi nitakua nikimtasfiria ambacho tutakua tukiongea kwani kutumia lugha ile angekumbuka mambo mengi akiwa Dar es salaam.



Fatemeh hakua na namna zaidi ya kukubaliana na maneno ya mzee yule shahzad ambae alionekana kuwa mwenye furaha mno wakati huo tulipokutana nae.

Kama unavyojua changamoto za wazee bwana akaanza kuleta stories nyingi za dar es salaam bila hata kutuuliza sisi tumefata nini pale. Mbaya zaidi story hizo ziliwahusu marafiki zake ambao karibia wote walikua ni marehemu.

Na kingine Dar es salaam aliyokua anaizungumzia yeye ni Dar es Salaam ya miaka hiyo hamsini kweusi yaani kabla ata ya uhuru.

Kuna muda alisema au aliitaja msasani kama nje ya jiji la Dar es salaam na apa alinishangaza kidogo sema nikabidi niwe mpole niendelee kumsikiliza.


Kuna muda ata fatemeh alichoka kumsikiliza tena ukichanganya na lugha ya kiswahili aliyokua anatumia mzee basi maskini fatemeh alikua bored sana kwa kumtizama tu.

Kwenye story zake nilikariri jambo moja ambalo kama nitakutana na wazee wa Dar es salaam nitawauliza swali hili.

Alidai asili ya neno dar es salaam sio bandari salama kama ambavyo ilikuja kugeuzwa baadae la hasha, Dar es salaam asili yake ni neno la kiarabu eti

Dar al-Islam au Darul Islam apa alisema maana ya neno hilo ni eneo linalokaliwa au kushikiriwa na waislamu. Na alitaja maeneo hayo mengi yalikua ni pale pale City center na kwa logic yake nilielewa kwanini alisema msasani ni nje kidogo ya jiji la Dar es salaam.

Hivyo basi na wewe kama utakua interested jaribu kufuatilia maana ya neno dar es salaam ujue ni kweli lilichakachukiwa au hapana.

Kama lilichakachuliwa ni kwanini walifanya hivyo? Je ilikua ni kuepuka kasumba za udini au vipi. Binafsi kama nilitaka kumuamini mzee huyu alafu kuna muda kama nafsi ilikua inasita kabisa.

Kwanini niitaka kumuamini, kwanza kabisa wale wazee ambao aliokua akiwataja kama ndio wazawa wa dar al-Islam au Darul Islam karibia wote walikua ni waislamu kuanzia majina yao mpaka imani zao za dini.

Lakini pia eneo hilo la dar al-Islam au Darul Islam lilikua na idadi kubwa ya misikiti karibia kila kona, ata wewe unaweza kujaribu kuchunguza mitaa ya city center misikiti ipo kwa idadi kubwa sana.

Any way tuliache hilo na tuangalie jambo lingine, kwenye story zake alimtaja mwalimu Nyerere lakini haikua positively hivyo binafsi siwezi kuelezea alimtaja kivipi kwani naamini na nathamini sana mchango wa mwalimu Nyerere mpaka taifa hili kufikia hapa.

Hivyo basi kwa upande wa shahzad nadhani alikua na chuki zake binafsi dhidi ya mwalimu wetu kipenzi mwalimu Julius kambarage Nyerere.

Na ni kama nilidhihirisha kuwa chuki zake zilikua kidini sana sana kwani alionekana ni wale watu ambao walitarajia serikali ya Tanganyika itakua ni serikali ya kiislamu lakini mambo hayakuwa hivyo.

Kwa maelezo yake ni kwamba wazee wa dar al-Islam au Darul Islam walikosea sana eti kumkaribisha mwalimu na kumpa wazfa kwani yeye ndio alikuja kuupoteza uislam na waislamu wa dar al-Islam kwa miaka ile.
Kumbe washiraz wengi waliukimbia mji baada ya kuona mtawala amekua ni mwalimu lakini pia from the beginning hawa wafanya biashara wa kishiraz ndio walikua wana finance shughuli zote za kudai uhuru au nationalistic struggles.

Na alidai baada ya kuona wazee wa Dar wamempokea mwalimu waliamua kuachana na chama hicho kwenye kuki finance na baadae walihamishia nguvu kwenye chama kingine ambacho nimekisahau jina lakini kilikua na element za kiislamu ndani yake.

Naomba tuziache habari za mwalimu na masuala ya uhuru turudi kwenye simulizi yetu..

Mzee aliongea mengi mengi, yaani mambo mengi sana aliyowahi kuyafanya ndani ya jiji la Dar, lakini ili kumtoa kwenye reli niimuuliza nini kilichompeleka kwenye jiji hilo ambalo aliliita dar al-Islam au Darul Islam.
Hapa alidai kilichompeleka dar al-Islam ilikua ni biashara...

Kabla hajaendelea tulisikia adhana, na alitoa muongozo au alinionyesha njia akimaanisha twende msikitini. Masikini ya mungu hakujua ile kanzu nimeivaa tu na lile jina nimepewa tu....
HAKUJUA KAMA NILIKUA SHEKHE WA MCHONGO,



(0623329512 Whatsapp) aftatu tu kupata muendelezo



Jana kwenye episode za Whatsapp tulikua na kikao cha mwisho na Shahzad,
Na kwenye kikao hicho Shahzad alikua ananipa ABC za vituko vya baharini.
Alidai kuna sehemu baharini hakuna sheria za physics kabisa yaana mambo yanaenda kisengerenyuma kulingana na laws za wafizikia. yaani hakuna cha relativity sijui quantum mechanics wala sijui nini kila kinachosogelea hapo huvutwa na hakiwezi kutoka tena. (Akimaanisha escape velocity ni infinity)

Kiuhalisia ni kwamba hakuna kinachoonekana kwenye eneo hilo ata mwanga wenyewe hauonekani ahahahah hahahha.

Yaani kwa lugha rahisi ata mwanga ukienda hapo haurudi, waliosoma soma physics si mnajua kuwa ili uweze kukiona kitu basi ni lazima mwanga uwe unatoka kwenye hicho kitu.

Sasa basi kwenye maeneo hayo ata mwanga ukienda hautoki, utaona nini eti? Mzee alidai kila kitu husimama kikifika apo mpaka muda husimama eti, yaani kuna uwezekano ukiingia umo usizeeka karne karne.

Bahari inavitukoa sana na baharia shahzad atatueleza mengi kuhusu vituko vya bahari na ndio maana wataalamu wanakubali kutokuijua bahari kabisa. Na kama wanaijua basi ni asilimia zisizozida 7% kwenye 100%,

Tuendelee kusoma kwa kutulia kuna mengi kwenye simulizi







Sent from my ZTE T1002 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom