Utajiri wa Magofu ya Rapta

Utajiri wa Magofu ya Rapta

Baada ya Shahzad kumaliza maelezo yale yaliyohusu namna gani ya kufika kwenye mji huo kupitia ramani ile. Alianza kutupa story za mzee Schulz na harakati zake za kuitafuta rapta akiwa Tanganyika ya enzi hizo.

Mzee shahzad akiwa Tanganyika hakuwa amekaa hivi hivi uku akiseti mipango yake ya kuzamia mji wa rapta. La hasha!!! Akiwa Tanganyika mzee shahzad na mke wake walikua ni miongoni mwa wafanya biashara wakubwa Ndani ya jiji la mzizima.

Ukiacha wahindi kadhaa waliomiliki maduka makubwa na mfumo mzima wa biashara nchini Tanganyika. Basi waliofuata hakuna namna utawaacha washiraz wa bara na visiwani ambao nao pia kwa sehemu kubwa walimiliki mifumo mingi ya biashara.

Shahzad alikua ni miongoni mwa washiraz wachache waliomiliki biashara kubwa nchini kwa enzi hizo kabla ya uhuru.

Akiwa kwenye biashara zake za siku zote siku moja shahzad alikutana na bwana mmoja mjerumani aliyejitambulisha kwa jina moja tu la seabot, seabot alikua ni mjerumani aliyekua anaishi Tanganyika kwa miaka mingi hapo kabla na muda wote alijichimbia mkoa wa lindi wilaya ya nachingwea.

Seabot alikua anafika Dar es salaam mara chache sana kwa ajili ya kufanya shopping ya vitu ambavyo kwa maeneo ya lindi mjini ilikua ngumu kuvipata.

Shahzad hakuwahi kujua kwanini seabot alijichimbia maporini huko miaka yote hiyo. Lakini baada ya kufahamiana na kutambulishana seabot alimueleza Shahzad kuhusu uwepo wa Schulz mkoa huko.

Kwa maelezo ya seabot ni kwamba Schulz aliishi kwa rafiki ake seabot uku akiwa anaendelea na uchunguzi wake wa kuutafuta mji wa rapta.

Swali la kwanza la Shahzad kwa seabot lilikua ni kwanini huyo Schulz asikae dar es salaam au ata maeneo mengine ya karibu mfano kilwa na sio kwenda kuishi mbali hivyo ( nachingwea).

Kwa mujibu wa seabot ni kwamba Schulz alienda kukaa kwa seabot mara kadhaa ambazo alikua anahitaji kupumzika lakini mara nyingi anakua sehemu moja maarufu kama muhoro huko lufiji na wakati mwingine anakua kilwa.

Sasa basi baada ya seabot kukutana na shahzad aliomba awakutanishe wawili hawa ili wasaidiane kwenye kile kinachotafutwa kwani seabot aliona kabisa matumaini ya kuupata mji huo kwa Schulz peke yake asinge weza.
Mpaka Wakati huo Seabot hakuweza kufahamu kwamba wawili hao walishawahi kukutana hapo kabla. Na ilibidi Shahzad amueleze ukweli bwana seabot kuwa alishawahi kukutana na Schulz wakiwa huko Tehran miaka kadhaa nyuma.

Pia alimueleza kuwa yeye ndiye aliyempa Schulz habari hizo zilizohusu mji huo.

Kuanzia hapo seabot alimuomba sasa awakutanishe ili wasaidiane, lakini kwa mujibu wa shahzad hakua tayari kushirikiana na Schulz kwa madai ya kwamba alishamjua ni mtu wa aina gani.

na in case wakapata chochote basi Schulz asinge shindwa kumtoa mwenzie roho ili tu mali zile azimiliki yeye mwenyewe.

Alichokifanya Shahzad kwa Wakati huo ni kumpa bwana seabot maelezo ya namna gani ataweza kufika hapo kwa kua yeye mpaka wakati huo alishakua ameenda tayari awamu ya kwanza na kufanya survey.

Alichokua anasubiri ni kwenda safari nyingine ambayo ndio ilikua ya kwenda kuchukua au kufungasha mizigo au mali zilizokua huko bila ya kujua kuna changamoto kadhaa.

Kwanini Shahzad alitoa maelekezo kirahisi hivyo kwa seabot ili yakamfikie Schulz na Schulz afike huko kwa wepesi, kilichotokea ni kwamba Shahzad alikua anaamini kwa jinsi kule Ndani kulivyo Schulz asingeweza kufanya chochote au kutoka na chochote.

Wajermani walikua na utaalamu kwenye mali kale zilizoachwa na ndugu zao pekee enzi za German East Africa. Lakini kwenye mali zilizoachwa na wengine au ata kutelekezwa na wengine basi wajermani hawakua na ujanja.
Na shahzad alishalijua hilo mapema sana ndio maana alitoa maelekezo ya kufika huko kirahisi sana kwa bwana seabot.

Shahzad hakua tayari kukutana na Schulz au kushirikiana na Schulz kwani tayari alishamjua ni mtu wa aina gani.

Lakini pia mbali na hayo tayari alisha ahidiana na yule bwana wa ushelisheli kuhusu kushirikiana kwenda huko hivyo hakua tayari kumuhusisha na Schulz.

Kwa mujibu wa seabot Schulz alifanikiwa kufika rapta, lakini baada ya kuzamia na kufika huko alichokuta ni vitu viwili tu.

Kwanza Schulz alifanikiwa kuona kuta nene zilizo mong'onyoka na kudondoka kutokana na maji yaliyokua yamezunguka kuta hizo.
Na Schulz ni miongoni mwa watu waliokubali kuwa mji huo ni mji wa kale kutokana na kile alichokiona huko au kutokana na jinsi mawe ya ukuta ule yalivyoonyesha kuwa ni yamebebana kwa karne na Karne.

Hilo lilikua ni jambo la kwanza kuliona Schulz akiwa uko underground chini kabisa ya bahari iliyozunguka maeneo ya Mafia. Na kwa bahati mbaya Schulz hakuona chochote kile kilichoonekana kufanana na mali au artifacts kale.

Jambo la pili kuliona Schulz hakuna aliyelijua kwani ata seabot mwenyewe hakuambiwa na mwenzie. Kilichofanyika ni kwamba Schulz alimwambia tu seabot kwamba pale rapta hakuna chochote na kama kitakuwepo basi kuna nguvu na roho za ziada zinahitajika kupata ilichopo pale.


Schulz aliona nini? Lilikua ni swali langu kwenda kwa shahzad,

Lakini Shahzad alisema tuendelee, na kuhusu alichokiona Schulz atakiona yeyote ambae ataenda pale kwa nia ovu ya kuiba urithi ule uliokuwepo pale.

Kwanini Shahzad anatumia neno kuiba, mwenye mali ile ni nani hasa?

Kwa mujibu wa shahzad ni kwamba wenye mali ile ya rapta ni wafalme wa bahari wenyewe na ndio waliouficha mji huo kutoka kwenye macho ya kawaida ya binadamu na pia kutoka kwenye uso wa dunia.

Kuna muda kumuelewa Shahzad ilikua ngumu sana kwani alikua anazunguka zunguka sana bila kunyoosha mambo.

Mpaka hapo alikua ameanza kunivuruga, sasa kama Schulz alikua anaiba na mimi si nitakua naiba pia na kuna tofauti gani kati yangu na Schulz.

Kwa alichokisema shahzad ni kwamba tofauti yangu mimi na Schulz ni kwamba mi nitaenda pete ambayo itanipa utambulisho.

Na apo shahzad aliongeza kitu kuwa kuna mambo mawili, jambo la kwanza kutambulika na jambo la pili uwezo wa kuondoka na kile kilichopo japo alisema zile million tonnes za gold kule chini hakuna wa kumaliza.

Kwa mujibu wa shahzad pia alisema history ya afrika kwa sehemu kubwa ipo chini ya ardhi, hizi historical sites chache tunazoziona afrika hususani Tanganyika ni sehemu ndogo sana ya history nzima ya Tanganyika au afrika kwa ujumla.

Rehman yeye mda wote alikua ni msikilizaji mkubwa hakupenda kuongea chochote na kikubwa alichokuwa anasubiri yeye ni safari tu na sio vitisho vya Shahzad.

MIMI: lakini mzee wangu wewe ulienda na pete kwanini hukutoka na chochote.

SHAHZAD: hahah ahaha hahaha aaaa siri ya jandoni inabaki jandoni, we pambania malengo yako kwanza una uhakika gani kama sikutoka na chochote.

Hapo nikaikumbuka kauli yake ya kwamba kuna millions of tonnes ambazo si rahisi kuzimaliza kwa namna yeyote ile.

Nikajiongeza tu kuwa kuna uwezekano alitoka na chochote lakini pia bado kuna mzigo wa kufa mtu umebaki huko chini.

Shahzad alidai kwamba toka kuzama kwa mji huo hakuna mtu mweusi yoyote aliyejaribu kufika huko chini kwa nia ya kutaka kubeba mali ile. Hivyo alikua ana sapoti kwa asilimia kubwa sana safari yangu akiamini naweza rudi na matokea mapya.

Apa Alidai kwakua mji ule uliozama wenyeji wa kwanza kabisa walikua ni watu weusi basi kuna uwezekano warithi wa mali ile wanaotambulika wanatakiwa kuwa watu wenye kutokea nasaba za weusi pia.

MIMI: hivi mzee kilichopo kwenye mji ule ni dhahabu pekee, na imetunza kwenye mazingira gani miaka yote hiyo na hii pete itanipa ishara gani kuhusu iliko mali?

Nilipenda kutumia kiswahili kuuliza maswali kwakua ndani ya maswali yale nilihusisha pete ambayo shahzad hakutaka Rehman aifahamu.
SHAHZAD: ukiwa na hiyo pete mara tu atakapokaribia eneo lile au ufalme ule utahisi kitu cha tofauti sana kwenye mwili wako. Mji ule umezungushiwa ukuta kwenye mipaka yake na ukiwa na pete hiyo ukikaribia mipaka basi utaweza kuona njia zote na kila kitu.

MIMI: je!! Pete hii inafanya kazi baharini peke

SHAHZAD: hahahaha ahahaha nilisahau kitu cha msingi sana tena kwa jinsi wewe ulivyo na roho ndogo na nyepesi hii pete vaa ukiwa unaanza uzamiaji tu.

Muda wote huo mi naongea na shahzad Rehman alikua bize kuisoma upya ramani ile na kuna muda alimuuliza kitu shahzad kutoka kwenye Raman ile. Na shahzad aliendelea kumpa maelekezo kwa sehemu zote ambazo aliona zinampa changamoto Rehman.
Mwisho kabia mzee alisema nahitaji kupumzika sasa na tunaweza kuondoka, binafsi nilichokifanya ni kuchuka address ya Rehman na kumwambia tutawasiliana baadae.

Shahzad nilimwambia kabla ya kuondoka nitarudi tena kumuaga hivyo hizo siku kabla ya kuja kumuaga nitakua najiandaa na safari. Kuhusu Rehman nilimuomba tukutane ili tupange bajeti na mikakati mingine mingi.

Japo Rehman Alidai ya kwamba ili kufanya bajeti sahihi tulitakiwa kufika kwenye field kwanza na kuona ni miundo mbinu ipi itatumika tukiwa apo.

Tulikubaliana hivyo na mimi nikawa wa kwanza kuondoka eneo hilo nikimuacha shahzad na Rehman wakiendelea na maongezi yao.


Fatemeh kama kawaida mda wote alikua ananisubiri ili tuweze kuondoka wote kurudi nyumbani. Nilimueleza kuhusu Rehman na nikamwambia nimechukua address yake hivyo kabla ya safari itabidi tuonane.

Kwa mujibu wa fatemeh alidai mpaka alipofikia wakati huo Rehman hakua mtu m'baya katika misingi inayoijua yeye.

Labda aendelee na uchunguzi wake mwingine na amuangalie kwa upande mwingine, kwani alidai jina lake pia lipo kwenye list ya wafungwa waliwahi kufungwa kwenye gereza kubwa kwenye nchi hiyo.

Muda wote huo nilikua naisubiri report ya fatemeh kutokana na kile alichoniambia asubuhi ya siku hiyo kwamba alikua anaenda kukutana na director ili amjibu baadhi ya maswali yake.

Fatemeh alisema tufike nyumbani kwanza, lakini kwa taarifa fupi mpaka muda huo alishajua ni namna gani kifo cha Gatkuoth kilitokea na ni kweli Javier hajahusika kabisa wahusika wakuu walikua ni MOIS.


KWANINI MOIS WALIMUUA GATKUOTH?

Nusu ya maajabu ya pete ya shahzad yanapatikana pia kwenye ngozi na mifupa ya mnyama anayeitwa NGEKEWA,

Watu wa mali kale na madini nadhani mnanielewa, kwa upande wetu huu wa East Africa maeneo tunayompata NGEKEWA ni kwenye misitu ya kongo pekee. Huku ndipo kuna wataalamu wa kumtega ili kumpata mzima mzima, sitangazi biashara ila kwa anaejua matumizi ya ngozi na mifupa ya mdudu huyu atajua nachomaanisha.

Njoo kule Whatsapp kama unamjua huyu mdudu na unataka kumtumia.
Hii stori Ina mvuto was aina yake, Chamecha mbe..
 
TUNAENDELEA WAKUU

Kwa mujibu wa fatemeh ni kwamba taarifa iliyomuhusu Rehman ilimchanganya sehemu moja tu, Kwanza Rehman alionekana ni askari wa kikosi cha wanamaji nchini Iran yaani NEDAJA kama nilivyotangulia kusema hapo awali.

NEDAJA ni jina la Jeshi la Wanamaji la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran au wengine huita ISLAMIC REPUBLIC OF IRAN NAVY.

Jambo jingine lililomchanganya fatemeh ni kwamba Rehman huyohuyo kwa kipindi hicho hicho alionekana kutumiakia kifungo kwenye gereza moja maarufu na kubwa nchini humo.

Tehran central prison au fashafuyeh ndilo gereza alilosemekana kuwepo bwana Rehman wakati huo huo kuna taarifa zilikua zinadai jamaa alikua ni mwanamaji wa Iran.
Taarifa hizi alizipata fatemeh baada ya uchunguzi wake wa masaa machache kabla sijakutana na Rehman, je alijuaje kama kuna mtu naenda kukutana nae anaitwa Rehman kwa kweli sikujua mpaka muda huo.

Na ata ujio wake fatemeh kuja pale kwa shahzad ni baada ya kukadilia au kujua muda ambao Rehman ata kuja pale kuonana na sisi. Ila kilichonifurahisha ni kimoja tu baada ya kudai Rehman hakua mtu m'baya kabisa labda akiendelea na uchunguzi kama atagundua madudu mengine yanayomuhusu Rehman.

Kitengo na taaluma ya fatemeh ni vitu vilivyomfanya aweze ku access taarifa nyingi zilizohusu nchi na wananchi kwa ujumla. Huku akizipata taarifa za aina zote yaani zile taarifa za siri na zisizo na siri na wakati mwingine za halali na zisizo halali.


Fatemeh alisema niendelee kumpa muda atakuja na file lote la bwana Rehman kuhusu alipoanzia yaani kuzaliwa mpaka kufika pale alipo.

Alidai ni lazima afanye hivyo kwani kama safari ya kuelekea bongo na yeye atahusika hawezi kufuatana na mtu asiye mjua ukizingatia yeye ni mtu nyeti sana kwa idara yake.

Mpaka hapo nilishaanza kuona dalili zote za kurejea bongo nikiwa na mrembo fatemeh kwani ni kama alikua akifanya maandalizi hayo japo hakuniweka wazi moja kwa moja.

Sikujua unyeti wa fatemeh upo wapi kwenye idara yake lakini nilichokiona ni kama fatemeh alikua mtu mmoja untouchable sana kwenye idara hiyo. Na hilo niligundua baada ya kujua kama kwenye jengo lile 90% walikua ni watumishi wa idara hiyo na ni kama walikua wana keep distance na fatemeh kiasi kwamba hawakuweza kumzoea kabisa.

Tulipofika home akili yangu ilikua inawaza mambo mawili tu yaani habari za fatemeh Kuhusu kile alichoenda kuongea na director wake na aligundua nini kwenye kifo cha Gatkuoth.

Bila kusahau nilihitaji pia kumsisitiza afuatilie taarifa za Rehman ili tuwe na uhakika kuhusu mtu tunae enda kushirikiana nae huko rapta.

Tulipokaa tu baada ya kufika Ndani swali langu la kwanza lilikua ni kutaka kujua kilichojili baada ya kuonana na director.

Mara nyingi fatemeh hakupendelea kuzungumza mengi yaliyohusu idara yake nadhani ilikua ni desturi ya watumishi wengi wa hizi idara za inteligensia.

Hivyo namna ambayo fatemeh aliitumia kujibu maswali yangu haikua namna ya moja kwa moja, yaani fatemeh alitumia njia za mkato mno kujibu maswali yangu kiasi kwamba binafsi nilitakiwa kujiongeza ili kupata majibu ya maswali hayo.

Nilipo muuliza kuhusu kile alichokiongea na director Kuna mfano mmoja fatemeh aliutumia ambao wenyewe haukuhitaji akili kubwa ili kuelewa alikua akimaanisha nini,

Fatemeh alisema nchi kwa kawaida inafananishwa na nyumba yenye familia kubwa Ndani yake, kwenye nyumba hiyo lazima kutakua na mkuu wa mji au baba kwa jina lingine.

Sasa basi baba ndio kwa kawaida anahusika na mambo yote ya msingi kwenye jumba huku jukumu la ulinzi likiwa ndio jukumu kubwa na la msingi kwa familia yake.

Eeh ndio hivyo mzee, ata mwanamke anapoolewa kikubwa cha kwanza anachojihakikishia kwa mwanaume wake ni ulinzi na usalama wake.

Hivyo basi kama baba wa familia jukumu kubwa na la msingi ni kwamba unatakiwa kuhakikisha familia inakua secured by any means.

Sasa baba wa familia analinda vipi mji wake dhidi ya kila aina ya adui anayetazamiwa kuleta hofu kwenye familia yake.

Apa bwana kwenye ulinzi huo ni kwamba kuna aina kuu mbili za ulinzi dhidi ya mji au familia kulingana na maelezo ya fatemeh,

Aina ya kwanza kabisa Kuna ulinzi usiooonekana kwa macho ya kawaida yani kwa jina jingine huitwa INVISIBLE SECURITY

Aina ya pili ni ulinzi unaojulikana kama VISIBLE SECURITY huu wenyewe ni ulinzi wa kawaida kabisa unaonekana kwa kila anaesogelea familia au mji husika

Tusijasahau sana apa ni wakati fatemeh anajaribu kunielezea ulinzi wa nchi lakini alitumia mfano wa nyumba au mji huku akisema baba wa familia ndio anajukumu hilo la kuhakikisha familia inakua secured muda wote.

Sasa binafsi ndio nilitafsiri kua hiyo familia ni kama nchi na baba ndio kiongozi mkuu ambae anahusika na kuhakikisha familia inakua secured muda wote.

Sasa tuanze na visible security, huu ni ulinzi wa kawaida kabisa mfano nyumbani kwenu au kwako kama baba unaweza kuweka mbwa, mgambo ukampa na kilungu au ata CCTV camera pia.

Kikubwa apa kwenye visible security ni kwamba yeyote atakae fika nyumbani apo atajua au ataona ulinzi huo na ni rahisi kwa muhalifu kupambana na visible security kuliko invisible security.

Kwa maana hiyo visible security haijawahi kuwa bora kuliko invisible security mahala popote pale, tukija kwenye mfano wetu wa nchi ambapo mimi ndio niliojiongeza.

Kwenye nchi hakuna tofauti na familia ukizungumzia nchi basi visible security ni majeshi yote ya ulinzi na usalama. Kama kutakua na radars na vingine kama hivyo basi vyote kwa pamoja vinaunda kile kinachoitwa visible security.

Aya sasa tuangalie invisible security,

Invisible security ni ulinzi ambao hatuwezi kuuona kwa macho nikimaanisha ata adui anapo panga kuvamia mji au familia hawezi kujua au kuona ni namna gani mji huo unalindwa. Na hili jambo ndilo linafanya invisible security kuwa bora zaidi kuliko visible security wakati wote.

Ubora unatokea wapi? Ni kwamba adui anayetazamiwa kuleta hofu au madhara hushindwa kuujua ubora wa ulinzi wa ngome husika. Na sio ubora tu, pia hushindwa kumjua au kujua ni namna gani ata attack mlinzi ambae hamjui wala hajawahi kumuona.

Kwenye ngazi za familia au mji ulinzi ambao ni invisible security mara nyingi huwa ni siri kati ya baba na mama au wakuu wa familia wenyewe kwa wenyewe.

Wanafamilia wengine kawaida hawahusishwi kabisa kujua nini kinaendelea kwenye invisible security au ata hao wanafamilia wanaweza wasijue kama wanalinda kwa ulinzi huo.
Huwezi kuwaambia wana familia Kuhusu invisible security Kwan kuna muda maadui hutumia weakness za baadhi ya wanafamilia ili tu kugundua au kupata info zinazohusu hiyo invisible security.

Tusijasahau sana haya ni maelezo ya fatemeh,

Anaendelea, invisible security ni very controversial na pia inatumia intelligence ya hali ya juu sana kwakua moja ya malengo ya invisible security ni kumtambua adui na kumthibiti kabla hajaleta madhara kwa familia au mji.

Hivyo basi kuendesha invisible security ni gharama kubwa na akili kubwa pamoja na usiri vinahitajika, tukirudi kwenye uhalisia hii ndio sababu inafanya watu kama ***ISS wawadharau sana wana jeshi kwani wanaamini wao ndio wa kwanza kudumisha amani.


Wanaamini hivyo kwakua tu watu wa visible security hufanya kazi mara nyingi penye machafuko au ambapo amani imepotea tayari.

Hivyo ukiona sehemu kuna machafuko maana yake invisible walishashindwa kazi ndio sababu machafuko yametokea na hapo ndipo tutawaona visible kazini.

Hivyo basi invisible security ipo kazini muda wote kuhakikisha familia inakua secured muda wote lakini visible huingia kazini rasmi mara tu amani inapokua imepotea.

Kwanini invisible security ni inahusisha usiri wa hali juu, hii ni kwasababu sio tu miiko yake bali ata technique zinazohusishwa mara nyingi hazihitaji kumshirikisha kila mtu.


Mfano tu, baba anaamua kuulinda mji dhidi ya wezi na vigagula kwa kutumia njia za kiutamaduni yaani kwenda kwa waganga wa kienyeji.

Unafikiri yale masharti ata mwambia kila mtu kwenye familia au kama kapewa kadawa ka kuweka mlango atawaambia kama kaweka kadawa. Ukiona umeambiwa basi jua na wewe ni sehemu ya mpango au ni sehemu ya wakuu wa familia.

Huu nao ni mfano tu wa invisible security kwenye jamii zetu au kwenye majumba yetu.

Haya maelezo yaliyohusu invisible security na visible security aliyatoa fatemeh baada ya kumuuliza kuhusu nini kiliendelea baada ya kukutana na director. Ila ndani yake kuna mbwembwe nyingi nimeziongeza mimi mwenyewe lakini kikubwa upate concept kuhusu nini maana ya visible security na invisible security.

Turudi kwenye invisible security na sifa zake, agents wa invisible security kuna uwezekano mkubwa sana wasijuane japo wao pia hufanya shughuli moja au shughuli yao ikawa na lengo moja.

Kwa sababu zile zile kama usiri au kucheza na psychology za adui au hata kuzuia utengenezwaji wa mamluki ndio maana kuna muda hawa agent hawajuani.

Kwa mfano baba anaweza kumuweka mtu mtaani awe anaangalia muenendo wa nyumbani kwake hususani watoto wake au atawizi wa mali zake. Lakini asimuweke mtu mmoja pekee yaani akaweka ata watu watatu na wote wasijuane lakini misheni yao ni moja.

Na bado akaendelea kupokea taarifa za usalama wa mji wake kwa watu wote watatu kwa muda tofauti tofauti.
Kwanini hufanya hivi ni kwasababu agent akiwa mmoja kuna uwezekano mkubwa akatumiwa na maadui au ata yeye mwenyewe akageuka adui hivyo basi kwa kuzuia hali kama hiyo kuna ulazima wa uwepo wa multiple agents into a single mission.

Kwanini hawa ma agents hua ni siri na kuna madhara gani endapo watajulikana,

Nchi ya Iran mara kadhaa imepitia scenario zilizohusu mauaji ya watu wake muhimu kwenye idara yake baada tu ya kuwa watu hao wamejulikana.

Na ubora wa fatemeh ulionekana kuanzia miaka ya 2012 kushuka chini ambapo mara kadhaa alifanikiwa kugundua uwepo wa virus kwenye mifumo ya nyuklia na mifumo mingine ya ulinzi ya nchi.


Kwanini fatemeh amekua mtu wa kufichwa sana na muda wote yupo under intensive care na MOIS walitumia kigezo gani kuanza kumtumia fatemeh.

ukweli ni kwamba nchi ya Iran imekua ikipoteza watu muhimu kwenye mashambulizi ya hapa na pale yanayosababishwa wa maadui zake ambao ni waisrael na wamarekani.

Nitaweka list ya ma agents waliouawa na wengine kupotea kwa sababu tu walitambulika kama ni wahudumu wa MOIS.

Mfano 2011 July electrical engineer aliyekua akifanya kazi national security research facility aliuawa kwa kupigwa risasi na watu wawili wasiojulikana lakini wahahofiwa kuwa ni watu wa kutoka shirika la Mossad.


Baadae nakuja na list ya ma profesa na ma engineer walio uawa pamoja na udukuzi uliofanywa na Mossad juu ya mitambo ya nuclear ya Iran.

Hii yote ni series ya masimulizi aliyoyaanzisha fatemeh kabla hajanipa kile alichokipata kutoka kwa director.

TUKUMBUKE DIRECTOR NDIE SPY MASTER WA TAASISI YEYOTE YA INTELLIGENCIA.

0623329512 kwa wanaotaka muendelezo Whatsapp tunachangia buku 3 tu,

Mambo mazuri yanakuja mbele, leo tulikua mkoa wa kaskazini pemba huko micheweni kwenye bandari bubu moja hivi.
Napenda sana uandishi wako bro, yani natamani uendelee kuandika
 
"Mkataba wangu na ule wa amobi na Obi ulikua na tofauti kubwa kwani wao walijaza mikataba kama mercenaries yaani wanajeshi wakulipwa. Kwa Colombia waliita PRIVATE MILITARY CONTRACTOR (PMC) na hapa CV yao hawa jamaa ndio iliwabeba.

Hapo baadae tutaelezana ni kwa namna gani hawa jamaa wa PMC wanaendaga kushiriki vita za huko mashariki ya kati na malipo yao kiujumla."

Kuna vipolo kama hivi ambavyo hua naacha kwa kuahidi nitavitolea maelezo baadae, navikumbuka sana nasubiri tufike sehemu flan flan hivi ndio nianze ku clear vitu kama hivi.
 
"Mkataba wangu na ule wa amobi na Obi ulikua na tofauti kubwa kwani wao walijaza mikataba kama mercenaries yaani wanajeshi wakulipwa. Kwa Colombia waliita PRIVATE MILITARY CONTRACTOR (PMC) na hapa CV yao hawa jamaa ndio iliwabeba.

Hapo baadae tutaelezana ni kwa namna gani hawa jamaa wa PMC wanaendaga kushiriki vita za huko mashariki ya kati na malipo yao kiujumla."

Kuna vipolo kama hivi ambavyo hua naacha kwa kuahidi nitavitolea maelezo baadae, navikumbuka sana nasubiri tufike sehemu flan flan hivi ndio nianze ku clear vitu kama hivi.
Tupo pamoja
 
Mzeevip
"Mkataba wangu na ule wa amobi na Obi ulikua na tofauti kubwa kwani wao walijaza mikataba kama mercenaries yaani wanajeshi wakulipwa. Kwa Colombia waliita PRIVATE MILITARY CONTRACTOR (PMC) na hapa CV yao hawa jamaa ndio iliwabeba.

Hapo baadae tutaelezana ni kwa namna gani hawa jamaa wa PMC wanaendaga kushiriki vita za huko mashariki ya kati na malipo yao kiujumla."

Kuna vipolo kama hivi ambavyo hua naacha kwa kuahidi nitavitolea maelezo baadae, navikumbuka sana nasubiri tufike sehemu flan flan hivi ndio nianze ku clear vitu kama hivi.
 
Unaweza kuwa sahih kuataja majina na maeneo ila kukaa na IRGs agent tena mwanamke hilo nakataa iran kuna sheria kali sana mzee
 
Back
Top Bottom