Utajiri wa Magofu ya Rapta

Utajiri wa Magofu ya Rapta

HIKI KIPANDE KIPO SEHEMU YA MWISHO YA SIMULIZI,

NIMEKILETA HAPA ILI TUSAIDIANE BAADHI YA CONCEPTS.

kama haupo interested sio lazima kushiriki au kutoa maneno ya kejeli.

Nilijifunza nini kwenye safari ile ya kwanza kuzamia majini nikiwa na pete ya shahzad?

sehemu kubwa ilikua ni concept ya energy na concept ya matter, ndio nilichokihisi na kukiona kwenye ile trip yangu ya kwanza na baada ya kuvaa pete ile. I hope wote tunajua kuwa energy sio matter.
__________________________
Lakini pia,

Nikiwa na physics yangu uchwara kichwani, niligundua mambo mengi kwenye kile nilichokiona kwenye safari ile.

Kwanza kabisa niligundua sayansi sio kila kitu, yaani kuna mambo yanafanyika nje ya sayansi ( mtanielewa tu ).

Asilimia 90 ya mambo yanayofanyika kwenye ulimwengu wa giza huvunja kanuni za kisayansi hususani physics.

( Nakaribisha mjadala kwa anaebisha kuhusu hili na uwe unazijua kweli kanuni za kisayansi )

Hivyo kwa lugha rahisi ukitaka kuitwa mchawi basi kuwa tu na uwezo wa kufikiri nje ya sayansi au kuwa na uwezo wa kuvunja kanuni za kisayansi.

Mfano, ukiwa na uwezo wa kusafiri kutoka MWAYAYA ( UKANDA WA MANYOVU ) kwenda wilaya ya NKASI MKOA WA RUKWA ndani ya sekunde tatu. Utaitwa mchawi au watasema umeyeyuka ( teleport ) lakini uhalisia ni kwamba umevunja kanuni za physics au kanuni za kisayansi. Bila shaka utakua umevunja kanuni za zilizopo kwenye mahusiano ya muda na mwendo kasi (speed) hahaha hahah haha yaani utakua umesimamisha muda kwa lugha rahisi.

Ebu tuliache hili.

Unajua kwanini ukivunja kanuni za kisayansi utaitwa mchawi?
Hii ni kwasababu sayansi imekua ikichukuliwa kama kipimo cha mwisho cha ukweli au uelewa kwenye dunia hii,

Lakini ukweli ni kwamba sayansi ni sehemu ndogo sana ya maarifa yaliyopo kwenye ulimwengu huu.................!
Kwa kutumia pete ya shahzad niliona mahali sayansi inapoishia huku asili ikienda mbali zaidi kwa kuitumia au kuzitumia energy na matter katika namna tofauti tofauti.

Tutaelewana tu.
Sayansi has many unanswered question.
( Siipingi sayansi Nisieleweke vibaya )

Kwa mfano;
Nadhani wote tunajua kuwa speed ya mwanga inakadiliwa kuwa 300,000km/s, je vipi kuhusu speed ya giza (what about the speed of dark?).[emoji848]

Najua kuna watu watakuja na kusema kwamba giza halitembei bali linatanuka, hayo sio majibu na wala hayatoshi kutetea point husika.

Anyway uwanja ni mdogo sana hili nitalileta kama somo hapo baadae tukisha maliza simulizi yetu, kikubwa tuelewe tu kuwa kile tunachoita uchawi kiko mbele ya sayansi au kimeitangulia sayansi.

Aisee concept ni energy na matter, narudia tena energy sio matter

Hapa kwenye energy na matter hizi concept mbili ndizo zinavunja kanuni za kisayansi hususani physics.

Na hapa ndipo dhana ya nguvu za giza huibuka, kwanini huibuka ni kwasababu sayansi yenyewe au wanasayansi wenyewe hutoka patupu ndio maana hukimbilia kuita nguvu za giza baada ya kuundelea kuumiza vichwa.

Kwenye ulimwengu wa roho na ulimwengu wetu wa nyama tunafahamu ya kwamba kile kinachoitwa spirit au soul kwa kawaida kina energy ndani yake na ndio maana kina uwezo wa kufanya lolote.
( Sio kila sehemu nitakua muwazi utajiongeza mwenyewe )

TUANZIE KWENYE TOFAUTI YA ENERGY YA MATTER.

kuna watu watasema rasta simulizi imemshinda amehamia kwenye physics.
 
Mkuu, bora umerudi tena kutujuza juu ya "Utajiri wa Magofu ya Rapta"! Tulishapata hofu kwamba ulipotelea huko mazima!
 
Amobi na Obi walikua ni wanamgambo wa kikundi cha ISLAMIC STATE- WEST AFRICA PROVINCE chenye makazi yake huko afrika ya magharibi especially nchini Nigeria. Huku wakionekana kuwepo sana upande wa kaskazini-mashariki mwa Nigeria na kwa uchache sehemu za Niger.

Kwa mara ya kwanza walitambulishwa kwenye kikundi hicho na bwana mmoja aliyefahamika kwa jina la Abu Musab al-Barnawi. Walipata mafunzo yote ya msingi chini ya kikundi hicho mpaka kua wanamgambo hodari na wakutegemewa.

Kwa haraka niligundua jamaa hawa ni wale typical Muslims, ambao wanamipango ya kuhakikisha dola ya kiislamu inasimama kutokea west Africa na kisha dunia nzima.

Sababu ya jamaa hawa kutoka kwenye kikundi hicho cha ISWAP ( Islamic State- west Africa province) ilikua ni misunderstanding au mgogoro wa chinichini wa kiitikadi uliokua ukiendelea baina ya kikundi hicho na wanamgambo wengine wa kikundi cha Boko Haram.

Nadhani kuanzia mwaka 2016 kwa wenye kumbukumbu mgogoro huu ulikua wazi na majeshi ya serikali ya Nigeria yalifurahia baada ya kuona vikundi hivi viwili tishio vikianza kupigana wenyewe kwa wenyewe.

Miguel alianza kuwa muwazi kwenye baadhi ya Mambo, Mfano tukiwa safarini alipata kutueleza machache kuhusu safari yetu na nini tunaenda kufanya mwisho wa safari hiyo. Kupitia Miguel ndio nilifahamu wasifu wa amobi na Obi, amobi na Obi walikua ni watafutaji pia baada ya kuona mipango ya ISWAP inaelekea kubaya ndio waliamua kutimkia Colombia.

Ilituchukua umbali wa zaid ya kilometers 160 kaskazini mwa mji wa Riohacha na kisha kuvuka jangwa dogo ndio tulifika mji mmoja wenye pwani nzuri ulioitwa Cabo de La Vela.

Ndani ya mji huo mdogo uliokua pwani tulikutana na baba mzazi wa Miguel ambaye hakujitambulisha kwa majina.

Tukiwa hapo tulikabidhi mabegi yetu yote yakiwa na documents zetu zote yaan zile hati za kusafiria na nyaraka zilizo onyesha taarifa zetu za kiafya. Hili lilikua ni kosa lingine nalifanya bila kujua baada ya lile kosa la kukubali kutumia jina ambalo halikua langu huku.

Tukiwa Cabo de La Vela tulisaini mikataba ya kazi ambayo ndani ya malipo ya kazi hiyo zaidi ya 30% ilikua inaenda kwa wakala aliyefanikisha mpango huo.

Hapa nilibaki na maswali mengi kichwani, wakala wangu alikua ni nani? Je ni McKenzie, Ally au Ras kama sio hivyo ni nani, ni Mahmoud au huyu mzee ambaye ni baba ake na Miguel.

Mkataba wangu na ule wa amobi na Obi ulikua na tofauti kubwa kwani wao walijaza mikataba kama mercenaries yaani wanajeshi wakulipwa. Kwa Colombia waliita PRIVATE MILITARY CONTRACTOR (PMC) na hapa CV yao hawa jamaa ndio iliwabeba.

Hapo baadae tutaelezana ni kwa namna gani hawa jamaa wa PMC wanaendaga kushiriki vita za huko mashariki ya kati na malipo yao kiujumla.
 
HIKI KIPANDE KIPO SEHEMU YA MWISHO YA SIMULIZI,

NIMEKILETA HAPA ILI TUSAIDIANE BAADHI YA CONCEPTS.

kama haupo interested sio lazima kushiriki au kutoa maneno ya kejeli.

Nilijifunza nini kwenye safari ile ya kwanza kuzamia majini nikiwa na pete ya shahzad?

sehemu kubwa ilikua ni concept ya energy na concept ya matter, ndio nilichokihisi na kukiona kwenye ile trip yangu ya kwanza na baada ya kuvaa pete ile. I hope wote tunajua kuwa energy sio matter.
__________________________
Lakini pia,

Nikiwa na physics yangu uchwara kichwani, niligundua mambo mengi kwenye kile nilichokiona kwenye safari ile.

Kwanza kabisa niligundua sayansi sio kila kitu, yaani kuna mambo yanafanyika nje ya sayansi ( mtanielewa tu ).

Asilimia 90 ya mambo yanayofanyika kwenye ulimwengu wa giza huvunja kanuni za kisayansi hususani physics.

( Nakaribisha mjadala kwa anaebisha kuhusu hili na uwe unazijua kweli kanuni za kisayansi )

Hivyo kwa lugha rahisi ukitaka kuitwa mchawi basi kuwa tu na uwezo wa kufikiri nje ya sayansi au kuwa na uwezo wa kuvunja kanuni za kisayansi.

Mfano, ukiwa na uwezo wa kusafiri kutoka MWAYAYA ( UKANDA WA MANYOVU ) kwenda wilaya ya NKASI MKOA WA RUKWA ndani ya sekunde tatu. Utaitwa mchawi au watasema umeyeyuka ( teleport ) lakini uhalisia ni kwamba umevunja kanuni za physics au kanuni za kisayansi. Bila shaka utakua umevunja kanuni za zilizopo kwenye mahusiano ya muda na mwendo kasi (speed) hahaha hahah haha yaani utakua umesimamisha muda kwa lugha rahisi.

Ebu tuliache hili.

Unajua kwanini ukivunja kanuni za kisayansi utaitwa mchawi?
Hii ni kwasababu sayansi imekua ikichukuliwa kama kipimo cha mwisho cha ukweli au uelewa kwenye dunia hii,

Lakini ukweli ni kwamba sayansi ni sehemu ndogo sana ya maarifa yaliyopo kwenye ulimwengu huu.................!
Kwa kutumia pete ya shahzad niliona mahali sayansi inapoishia huku asili ikienda mbali zaidi kwa kuitumia au kuzitumia energy na matter katika namna tofauti tofauti.

Tutaelewana tu.
Sayansi has many unanswered question.
( Siipingi sayansi Nisieleweke vibaya )

Kwa mfano;
Nadhani wote tunajua kuwa speed ya mwanga inakadiliwa kuwa 300,000km/s, je vipi kuhusu speed ya giza (what about the speed of dark?).[emoji848]

Najua kuna watu watakuja na kusema kwamba giza halitembei bali linatanuka, hayo sio majibu na wala hayatoshi kutetea point husika.

Anyway uwanja ni mdogo sana hili nitalileta kama somo hapo baadae tukisha maliza simulizi yetu, kikubwa tuelewe tu kuwa kile tunachoita uchawi kiko mbele ya sayansi au kimeitangulia sayansi.

Aisee concept ni energy na matter, narudia tena energy sio matter

Hapa kwenye energy na matter hizi concept mbili ndizo zinavunja kanuni za kisayansi hususani physics.

Na hapa ndipo dhana ya nguvu za giza huibuka, kwanini huibuka ni kwasababu sayansi yenyewe au wanasayansi wenyewe hutoka patupu ndio maana hukimbilia kuita nguvu za giza baada ya kuundelea kuumiza vichwa.

Kwenye ulimwengu wa roho na ulimwengu wetu wa nyama tunafahamu ya kwamba kile kinachoitwa spirit au soul kwa kawaida kina energy ndani yake na ndio maana kina uwezo wa kufanya lolote.
( Sio kila sehemu nitakua muwazi utajiongeza mwenyewe )

TUANZIE KWENYE TOFAUTI YA ENERGY YA MATTER.

kuna watu watasema rasta simulizi imemshinda amehamia kwenye physics.
Tuendelee mkuu.
 
Nashukuru kaka kwanza kwa kurejea kuiendeleza story yako ila mbona naona kama mwendelezo hauko sawa je unakumbuka mara ya mwisho ulikuwa unazungumzia jambo gani? Story ni hii hii ila tukio kama unaloliongelea leo sio mwendelezo wa mara ya mwisho
 
NILIAHIDI KUMALIZA SIMULIZI, TUENDELEE WAKUU

Maelezo ya fatemeh,

Mwaka 2011 mwezi April Iran Cyber defense agent ( haku mtaja jina) aligundua uwepo wa kirusi walichokiita stars kwenye mfumo wa kompyuta uliotarajiwa kwenda kuharibu mfumo wa kinyuklia wa Iran.

Kwa mujibu wa bwana mmoja ambae alimtaja kwa jina la Gholam Jalali ambae ndie alikua mkuu wa kitengo husika aliwataja marekani na Israel kuwa ndio wahusika wakuu.

Wataalamu wa Iran waliendelea kudai uwepo wa virusi kadhaa kwenye mifumo yao ya kikompyuta ilidhamiria kuharibu mifumo ya nyuklia. Mbaya zaidi ni programming code zake ambazo zilizotumika kwenye 2010 stuxnet attack.

Kwa kuhusisha na programming code za stuxnet attack basi huwezi kutengesha virusi hivyo na kuhusika kwa marekani na Israel kwenye tuhuma hizo.

Kirusi cha stuxnet kilianzishwa au niseme tu kili kuwa designed na wamarekani pamoja na wa Israel mwaka 2010 na kilionekana kwenye mifumo ya kompyuta huko bushehr kwenye mitambo ya nuclear.

Kirusi hicho kutokea bushehr kilisambaa kwenye compyuta zilizofikia idadi ya 30,000 na hatimae engine za IR-1 centrifuge ziliongeza speed mpaka kufikia kulipuka kwa mitambo hiyo.

Kwa uharibifu wote huu taasisi iliyojulikana kama institute of science and international security bado ilitupia lawama hizo kwa wa marekani na wa Israel kwa kuhusika na tukio hilo.

Bado tunaona uwepo wa marekani na Israel kwenye kila tukio lililo iathiri Iran kwenye upande wa ulinzi na usalama wake. Hivyo basi tunazidi kuthibitisha audui au uhasama uliopo baina ya Iran na kundi hili linalohusisha majasusi wa kimarekani na ki Israel.

Mbali na hapo bwana mmoja aliyejulikana kwa jina la Masoud Ali Mohammad profesa wa physics huko Tehran miaka hiyo hiyo ya 2010 aliuawa kwa bomu la remote control lililo tegwa kwenye gari.

Mtaalam huyo wa sayansi ya nyuklia pia anaaminika kuuawa na wale wale wanaohofiwa kuhusika na matukio mengine. Bila shaka watu hao ni wa marekani na wa Israel ambao ndio wamekua wakihusika mara zote kwenye matukio ya kufanana na hayo.

Ni kwa muda mrefu sasa Iran na Israel zinahusishwa na kile kinachoitwa kuchunguzana kiinteligensia na Israel ndio mara kadhaa amethibitisha kuvunja spy ring za Iran.

Uhasama huu utaisha lini? Nini chanzo cha uhasama huu, apo sitaki kuelezea kwakua tutakua tunatoka nje ya simulizi yetu. Hivyo basi tuendelee na kile nilichodhamiria kukieleza.

Kwa kipindi chote hiki fatemeh alikua msaada mkubwa sana kwa nchi kwa kupitia taaluma yake ambayo kwa kiasi kikubwa aliipatia huko nchini urusi.

Kabla hajapewa nafasi na kuaminika moja kwa moja kutokana na changamoto za kijinsia zilizopo nchini humo fatemeh alikua anagundua uwepo wa virusi lakini anakua amegundua akiwa nje ya muda na vinakua tayari vimesababisha madhara.

Lakini basi toka fatemeh aanze kuaminika amekua msaada sana kwenye mifumo ya nyuklia ya nchi hiyo kwa kuongezea ulinzi kwenye mifumo ya kikompyuta.

Akiwa kama ethical hacker mara kadhaa alikua makini kutafuta loopholes za mfumo wa ( kompyuta operating system) na kuuongezea ulinzi mfumo husika.

Lakini pia mbali na hapo binti huyo huyo mara kadhaa alidukua mifumo ya kiinteligensia ya Mossad kitu kilichowaumiza kichwa sana majasusi hao wa Mossad.

Uongozi wa MOIS haukua tayari kumtangaza Rasmi fatemeh kuwa ndie tegemezi kwa taasisi hiyo wakihofia aidha kuuawa au kutumiwa na mahasimu wao.

Hivyo basi kipaji cha fatemeh kinalindwa kama lulu na majamaa wa MOIS, japo ni wachache sana wanaomfahamu fatemeh na kile anchokifanya kwenye taasisi hiyo.

Fatemeh amekua akipewa ulinzi wa hali ya juu kwa kila anapoenda kiasi kwamba eneo alilopo fatemeh linakua na ulinzi kwa asilimia 100.

Japo kwa haraka haraka huwezi kugundua uwepo wa ulinzi huo lakini uwezekano wa kumdhuru fatemeh ni mdogo sana mahala popote atakapo kuwepo.

Apartment aliyokua anaishi fatemeh ilikua ni presidential suit, hahah hahaha hahahahah ebwana kumbe na mimi ni mnyama na nina unyama mwingi sababu tu nimelala room ambayo ni presidential suit

Bwana Mohamed ni mmoja miongoni mwa wale walioaminika na director kuwa kama mlinzi wa karibu sana wa fatemeh,

Kumbe basi, kila anapoenda fatemeh iwe usiku iwe mchana bwana Mohamed au mudi kibongobongo alikua yupo.

Yaani ulipo tupo

Kila ninacho kifanya na fatemeh jamaa wanajua sasa sijui kuhusu yale madudu ya chumbani kama wanayajua au vipi.

Bwana mudi au Mohamed kumbe alikuwepo kwenye ile ndege siku ile tunatoka kule Las Palmas Peruvian Air force base. Na kwa mujibu ile team tuliyokua nayo kwenye ile ndege ndio team ya ulinzi ya karibu iliyokua inamlinda fatemeh.

Fatemeh mwenyewe alikiri kutokujua lolote kuhusu uwepo wa team hiyo kwa dhumuni la kumlinda, kumbe basi ningekua makini au na kumbukumbu ningeweza kumtambua Mohamed toka siku ile kwenye ile ndege sema tatizo nilikua na wenge sana kama mnakumbuka.

Kumbe siku ile pia nikiwa na jembe langu tunatoroka zetu haullaga tunaelekea Cerro de Pasco hatukua peke yetu bwana, team ilikua nyuma na wengine wachache walikua mbele kuhakikisha tunafika salama.

Ramani aliyopewa fatemeh na mtu wa kwenye ile watch tower ndio ilikua inatuongoza kwenye njia ambayo jamaa wachache walikua mbele wakisafisha njia wakiongozwa na mudi na wengine walikua nyuma kutulinda.

Kwa mujibu wa fatemeh siku ile Javier na washirika wake alijaribu kutuma watu kutufuatilia lakini wote walikamatwa na kikosi cha bwana mudi au Mohamed kama nilivyozoea kutaja jina lake.

Kwenye maelezo hayo hayo ndipo fatemeh aliposema kwamba Mohamed au bwana mudi huyu huyu ndie aliyehusika na kifo cha fatemeh.

Lakini kifo cha Gatkuoth hakikuhusu au hakikuhusiana na Mossad au CIA kabisa zilikua ni sababu za kiusalama zilizomuhusu fatemeh ndio zilipelekea kuuawa kwa Gatkuoth.

Kwa mujibu ya maelezo yale ni kwamba kila atakae msogelea fatemeh kwa namna yoyote ile basi bwana mudi atakutoa roho aidha kwa ngumi, risasi au sumu kama ilivyo kwa Gatkuoth.

Ndio maana baada tu ya mimi kutaja aina ya sumu iliyomuua Gatkuoth fatemeh alihisi kitu, kumbe anaijua sumu ambayo mara kadhaa ilitumika kuuawa waasi au maadui wa MOIS ambayo ni strychnine.

Siku hiyo fatemeh alienda kwa director kwa dhumuni la kuwekwa sawa kwenye sintofahamu zote alizokumbana nazo kwa kipindi hicho chote.

Na kwa mujibu wa director alimueleza fatemeh mambo mengi ambayo alisema hakutaka kumueleza hapo kabla kwani aliamini muda haujafika.

Miongoni mwa mambo aliyoelezwa fatemeh ni kuhusu umuhimu wake na ni kwa namna gani amekua msaada kwa idara hiyo ambayo imekua ikitishiwa mara kadhaa na idara kama Mossad na CIA.

Hivyo uwepo wa fatemeh imekua ni kama mwiba sasa kwa majamaa wa Mossad na CIA na kwakua fatemeh hakua field agent imekua sio kazi ngumu kumuhakikishia ulinzi.

Kwanini fatemeh alipelekwa haullaga,

Baada ya kugundua weakness za Catarina waliona fatemeh atafaa sana kwenda kumaliza misheni hiyo mapema na hii ni kwasababu MOIS hawakua na field agent wa kike mpakw muda huo.

Ilionekana baada ya uchunguzi wa kina ni kwamba Catarina wakati yupo kwenye kikundi kile kilichoongozwa na Juan Carlos yani north valley cartel,

Catarina alijihusisha kwenye mpenzi ya jinsia moja na binti ambaye alikua na maumbile kama ya fatemeh hivyo MOIS wakamtumia fatemeh kwa dharula kwenye misheni hiyo.

Mpaka hapa ikumbukwe sikua nimefahamu kuhusu tatizo la kimaumbile la fatemeh na wala sikutaka kumhoji sana kuhusu changamoto hiyo.

Siku hiyo fatemeh alidai kuwa ndio kwa mara ya kwanza anajua kama director alikua anafahamu changamoto yake ya kimaumbile.

Hivyo basi haikua siri kama alivyokua anafikiria yeye, kitu kingine ni jambo lililohusu kifo cha zahra ambaye alikua ni mlezi wake.

Kwa mujibu wa director ni kwamba kifo cha zahra kilihusishwa na masuala ya kifamilia, hivyo ni zahra na ndugu zake ndio walikua na vita iliyohusu mirathi lakini aliendelea kusema Zahra sio jina halisi la mlezi huyo.

Je! Zahra alikua akiitwa nani hapo kabla, na kwanini alianza kuhudumia watoto yatima kwenye kituo kile na mwisho nani aliyemuua zahra.

Director alimwambia fatemeh kuwa file lipo na atampatia muda wowote ila kuna sababu za kiusalama za kufichwa kila taarifa iliyomuhusu Fatemeh.

Na kuhusu swala hilo ni kweli kabisa hakuna taarifa yoyote inayomuhusu mtu anayeitwa fatemeh utaweza kuipata kwa Wakati huo. Kila taarifa iliyomuhusu Fatemeh ilikua treated as a confidential ( yaani taarifa ya siri).

Kwa mujibu wa director alidai kufichwa kwa taarifa hizo kulisaidi ata wakati fatemeh yupo haullaga kwani washirika wa Javier walikua ni wa kwanza kutafuta taarifa za fatemeh japo walimfahamu kama Manuela lakini walichemka.

Ilionekana wazi wakati fatemeh anajiunga kwenye majukumu ya maabara ile ya haullaga washirika wa Javier walitaka kumtambua vilivyo kama walivyokua wakimtambua Catarina.

Catarina walimtambua kama mfanyakazi wa Juan Carlos kutoka kwenye kikundi kile kilichoitwa north valley cartel.

Wakati huo huo walimtambua Manuela kama muathirika tu wa dawa za kulevya kutokea huko Rio de Janeiro ila mbali na hapo hawakua na taarifa nyingine zozote na jambo hili liliwaaminisha kuwa alikua ni mtoto wa mtaani.

Kama bwana mudi ndio mlinzi wa karibu wa fatemeh huku fatemeh akiwa hamfahamu hapo kabla je mudi atakubali fatemeh aje bongo peke ake huku yeye aache jukumu hilo sidhani.

Aliyemuua zahra ni nani kwenye undugu wake na zahra na amefungwa gereza gani?

File la kesi ya mauaji ya zahra litakua na kitu gani ziada kuhusu fatemeh na je lina taarifa yeyote kuhusu maisha ya fatemeh?

Kikubwa ni kwamba MOIS walimtambua fatemeh kupitia kesi hii ya kifo cha Zahra na aliyekua mfuatiliaji wa kesi hiyo ni nani na kwanini alipendekeza fatemeh awe miongoni mwa watumishi wa MOIS.

Mbali na hayo pia MOIS kumshikiria fatemeh ilikua ni sehemu ya kumhakikishia usalama wake kutoka kwa wanafamilia ya Zahra ambao ata yeye hawajui.

Swali ni je wanafahamu kua fatemeh bado yupo hai, na kwanini wana hitaji kumuua pia endapo watagundua yupo hai,

Tule mtori nyama zipo chini, jana sikutoa muendelezo mnisamehe sana ila tunaendelea wakuu.
Umerudi![emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]acha tuendelee.
 
ndo shida ya stories za kuunga unga🤣😂😂😂🤣yaani mbele ya safari lazima utachemka tu
 
Uongozi wa MOIS haukua tayari kumtangaza Rasmi fatemeh kuwa ndie tegemezi kwa taasisi hiyo wakihofia aidha kuuawa au kutumiwa na mahasimu wao.

Hivyo basi kipaji cha fatemeh kinalindwa kama lulu na majamaa wa MOIS, japo ni wachache sana wanaomfahamu fatemeh na kile anchokifanya kwenye taasisi hiyo.

Fatemeh amekua akipewa ulinzi wa hali ya juu kwa kila anapoenda kiasi kwamba eneo alilopo fatemeh linakua na ulinzi kwa asilimia 100.

Japo kwa haraka haraka huwezi kugundua uwepo wa ulinzi huo lakini uwezekano wa kumdhuru fatemeh ni mdogo sana mahala popote atakapo kuwepo.
Yan unatuambia kwamba the most precious and most protected asset of the iranian intelligence ndo ilipelekwa huko huavalla sijui huvalla kwenye mashamba ya coca? Nani alikuwa anamlinda hapo shambani? Au hilo shamba ni la hao MOIS?
 
Afu sio kwa chai hii kali kabisa ya tangawizi. So mkuu wewe ukiondoka mademu huwa wanakufata tu😃😃😂😂
1.ulikuwa unatoka sengerema kuendelea mwanza mjini, merry akakuungia😂
2.ukaomba kwenda dar es salaam , merry nae akaunga
3.ilikuwa urudishwe bongo ila ukaomba kwenda iran na fatemeh akaridhia
4.mara unatoka iran kurudi bongo, fatemeh nae akaomba mje wote hahaha mamaee🤣🤣🤣🙌🏾🙌🏾🙌🏾
 
Back
Top Bottom