Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Ukwasi walionao baadhi ya mawaziri na wakuu wa mikoa na wilaya nchini umezua jambo: Watetezi wa haki za binadamu wamehoji walikopata ukwasi huo viongozi hao wa serikali.
Ni hoja iliyoibuliwa na watetezi hao jana jijini Dar es Salaam wakati wa mkutano wa tafakuri ya hali ya utetezi na uenezi wa haki za binadamu nchini kwa kipindi cha miaka 40 ya uwapo wa haki hiyo kikatiba.
Hao ni pamoja na Jenerali Ulimwengu, Askofu Emmaus Mwamakula, Shehe Ponda Issa Ponda, Mpale Mpoki, Tike Mwambipile, Hellen Kijo-Bisimba, Rugemeleza Nsala na Kaiza Buberwa.
Bila kutaja jina la waziri, mkuu wa mkoa na wilaya, Ulimwengu, mwandishi mkongwe mwenye taaluma ya sheria, aliwataka waandishi wa habari wenzake wampatie majibu kuhusu ulikopatikana ukwasi walionao baadhi ya mawaziri, wakuu wa mikoa na wilaya nchini.
"Ninyi waandishi wa habari, mmeshawahi kujiuliza mishahara ya viongozi, Mawaziri, wakuu wa mikoa na wilaya wanapata kiasi gani? Kile kipato chao halali! Masurufu anayopata yanayotokana na nini? Na akija madarakani, mali zake zinatokana na vyanzo gani? Au hii ni hela yetu ambayo ilipaswa kujenga barabara?
Chanzo: Nipashe

watakuwa walikuwa wanawafuatilia na ndio maana wameibuka leo baada ya Ukwasi wao kukua haraka kuliko uhalisia wa mishahara yao