Wachagga wanaofanya biashara wapo mikoani wakinga wengi wafanya biashara wapo dar na kwingineko hizo takwim zipo sahihi kabisa sidhan kama wasukuma wamesambaa sana kama wakinga wachagga
Wasukuma wamesambaa sana si Tanzania tu hadi Zambia na Zimbabwe. Wanajihusisha Kilimo na ufugaji. Zanzibar wamejaa, Mbeya, Mpanda huko Kigoma, ukanda wa Pwani. Ila ni kabila wasiopenda kujionesha.
Lakini ni kabila lenye idadi kubwa ya watu uwezi linganisha na makabila mengine. Wachaga na wakinga si wengi kiihivyo kama unavyodhani. Hata wakisambaa ni wachache wachache tu. Ujue wazi Mikoa ya Kanda ya ziwa mfano Geita, Shinyanga, na Mwanza, ni wasukuma. Mikoa hii inaonekana kushika nafasi.
Siwapendelei wasukuma ila wasukuma ni wachapa kazi, wakulima, wafugaji, wafanya biashara na hasa migodi. Wakati wakinga wengi na wachaga ni wafanya biashara wa maduka ya kariakoo, mabaa au club, hotel na biashara za nguo.
Wasukuma ukienda maeneo ya ukanda wa pwani utawakuta mashambani huko wanafanya kilimo na ufugaji. Wakati wachaga wachache utawakuta mjini na vijiduka. Uwekezaji wa wasukuma ni mkubwa kuliko wachaga. Sikatai kwamba hakuna wachaga wakulima ila kabila la wasukuma kwa ufugaji na kilimo linaongoza. Kumbuka mifugo mingi inatoka usukumani.
Thamani ya biashara za mgodi, kilimo na mifugo inathamani kubwa, ukilinganisha na hiyo biashara za vijiduka vya nguo, hotel, na club.
Mwanza ,Shinyanga, na Geita hukuti mtu kajiita billionea lakini hawa jamaa wana fedha sana, wametulia tu hawataki show off!